DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Miili hiyo ilisafirishwa hadi Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa uchunguzi zaidi na baadaye, wazazi na ndugu waliweza kuitambua miili hiyo ya vijana wanne kuwa ni wakazi wa Dar es Salaam, ambao ni Mikidadi Abbas Mikidadi (21), Hassan Juma Jumanne (21), Fadhili Patrick Hiyola (19) na Abdalla Fadhil Nyanga (21).
Jeshi la Polisi limesema miili hiyo imekabidhiwa kwa familia kwa taratibu za mazishi baada ya uchunguzi wa kitabibu kukamilika huku uchunguzi wa kina kubaini mazingira na wahusika wa mauaji hayo unaendelea.
Jeshi la Polisi mkoani Pwani limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa yoyote inayoweza kusaidia kufichua ukweli wa tukio hilo na kusisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni muhimu ili kubaini kilichotokea na kuwachukulia hatua kwa waliosababisha vifo hivyo.