Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Karatu msimu wa Mvua Kuna kuwa na tope la Hatari sana, Unashindwa kunyanyua mguu kutoka chini, Haswa hayo maeneo ya CCM , uwanja Mboe Hadi kupandisha Maeneo ya Jublate Mnyenye, NMB, Kwa Lekashu, Kadtuli Hadi Peter Ombay , Crater Rim, upande police na TRA shuka mitaa ya NBC kote ni tope ama Vumbi
Lakini niliona mtandaoni wanaweka lami. Hayo maeneo uliyotaja yana unafuu.. ukisema utoke nje tu ya hapo utajuta.
 
Aloo sio mchezo karatu baba lao. Nilienda msibani kurudi wife anauliza kwani walikugeuza maksai nn maana nguo zinachafuka vumbi la maana. Lile vumbi la karatu unaweza ombea hata mkopo bank.
hahahahah.. lakini inasemekana ile ardhi ndo ina rutuba zaidi kwa kilimo kwa sababu hata madawa hawatumii na wanavuna.
 
Hii ni miji kumi inayoongoza kwa vumbi nyakati za kiangazi nchini Tanzania. Ukienda huko achana na habari ya nguo nyeupe. Pendelea rangi nyeusi, brown au kijivu.

1. KARATU
2. KASULU
3. BOMANG'OMBE, Hai
4. SONGEA
5 TUNDUMA
6. ORKESMET, Simanjiro.
7. DODOMA
8. MERERANI
9. KIBONDO
10. MTO WA MBU
Mto wa mbu hatuna vumbi baya aisee. Umetuonea sana. Vumbi letu linafanana na rangi ya silva. Sio jekundu aisee
 
Back
Top Bottom