Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Hivi mnalijua vumbi la kahama - kakola, kahama - Nyanghwale, kuna kakipande ukikaribia kahama inabidi uwashe taa hata kama ni mchana maana mnaweza gongana, hala road ina rasta kama matuta ya viazi

Ila komesha ya yote ni Kasulu, kule kwa vumbi ni balaa
 
Boma ngo,mbe mbona Amna vumbi kule sema jua tu ndo Kali ila ardhi ya kule ni ngumu mwamba Kwa Moshi vumbi lipo Majengo kule lekunduu kama la karatu
 
Niliposoma title mji wa kwanza kuja kichwani ni makambako

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Makambako yes, lakini kuna vumbi na vumbi linalokera. Kiukweli Karatu, Nachingwea na Kasulu zina vumbi linalokera. Makambako, Dodoma, Kahama, Arusha, Himo/ Holili na maeneo mengine yana vumbi kali lakini angalau ni himilivu.
 
Mto wa mbu hatuna vumbi baya aisee. Umetuonea sana. Vumbi letu linafanana na rangi ya silva. Sio jekundu aisee
Kigongoni pale niliwahi kupita kuna vumbi la hatari, jua nalo linachoma kama pasi..uelekeo wa ile barabara ya loliondo ndo kabisaaaa

Sehemu nyingine yenye vumbi ni simanjiro na mererani, kwa kifupi ukitoka nje ya manispaa ya arusha jiandae kukutana na poda la nguvu
 
Yote tisa kumi..vumbi jekundu ni baya sanaa, mm eneo lolote lenye undongo mwekundu sipendi kuishi hapo
 
Sitoa sahau vumbi ndani ya treni kipande cha moshi to arusha,aisee na vile behewa letu lilikua mwisho,sijawahi kula vumbi kama hilo toka nizaliwe,fikiria ndani ya behewa huwezi muona jirani yako kisa vumbi[emoji28].
 
Back
Top Bottom