Miji miwili iliyobarikiwa zaidi na Mungu Tanzania

Miji miwili iliyobarikiwa zaidi na Mungu Tanzania

Wapi nimesema ilibarikiwa na Mzungu? Kwanza sijatumia neno Baraka, halileti mantiki kabisa ktk mada hii, natumia neno "kujaliwa", nimesema kuna kipindi cha hao watawala wa kizungu, Tanzania ilikuwa Tanga na Morogoro, hata Dar haikuwepo.

Lakini pia, Morogoro si miongoni mwa mikoa masikini Tanzania. Na kwa miji huwezi fananisha Moro na Moshi, labda na Kahama huko.
Umeandika maneno mengi afu ukasahau "Amen"
 
Vijana wa mikoani mnapenda kujipendekeza ili muonekane wa mjini. Dar na Pwani ndio mikoa iliyobarikiwa ndio maana mnaona wivu ikitajwa wenyeji wa Dar/Pwani wazaramo/wandengereko. Mkimbizi wa Burundi kamwe hawezi kuwa raia wa TZ.
Soon mtasema na Mwanza kwa wasukuma kwenu. BTW Wazee/wenyeji wa Dar wapo wengi haichukui hata masaa ku-notice ingawa hawapigi kilugha kama watu wa vijijini.
Kubalini na mjivunie kwenu.
Haya... rudi nyuma ukaandike "Amen" ili upate baraka.
 
Nazungumzia
1. Mji wa Moshi.
f83839974e390f98ec071d3db7eca479.jpg


2. Mji wa Arusha...
4f98f6283005ad04e5aaf0a620a5796d.jpg


I'm telling you! Hii miji miwili ndiyo yenye baraka zaidi mpaka hiyo milima inaishuhudia.

Type Amen.
Kuibariki zaidi nawe utabarikiwa.
Niulize kwanza, umeandika ukiwa wapi?
Kwetu milima ni laana
 
Ongea kuhusu mkoa wako mkuu acha kujipendekeza au kutaka kujihusisha au kujishikiza Dar au Pwani. Hii inathibitisha kwamba huwezi kuongea kuhusu TZ bila kuitaja mikoa hiyo ambayo ni ndoto ya kila MTZ kufika au kufanya kazi.
Wazaramo kitambo walijenga mkoa wa Pwani (Dar kama mkoa ulizaliwa mwaka 1972 na ulikuwa ni sehemu ya Pwani).Hizo picha mlizoposti ni sawa na Dar ya mwaka 1930.Hiyo habari ya kuuza haina maana bali wanapangisha msio na makazi mjini na kisha wenyewe wanapanua miji yao.
Sasa nijipendekeze na Dar es Salaam.
Na wakati nimezaliwa apa downtown, tatizo lenu watu wa Arusha na kilimanjaro mnaisi kwamba iyo mikoa ni mizuri kuliko. Mje apa Dar es salaam mshangae shangae alafu muende mkawasimulie manyumbu wenu
 
Nazungumzia
1. Mji wa Moshi.
f83839974e390f98ec071d3db7eca479.jpg


2. Mji wa Arusha...
4f98f6283005ad04e5aaf0a620a5796d.jpg


I'm telling you! Hii miji miwili ndiyo yenye baraka zaidi mpaka hiyo milima inaishuhudia.

Type Amen.
Kuibariki zaidi nawe utabarikiwa.

Acha uhamnazo wewe milima nayo ni baraka siku ikichemka volcano ilioko chini ya hiyo milima na kumwaga lava utakimbilia wapi ?
Milima unasema barka. Je ingekua dhahabu, alimasi, ziwa kubwa lenye bandari, ardhi nzuri ya kilimo cha pamba na mpunga samaki watamu kwa kula na biashara, kama ilivyo Mwanza ungesemaje?
 
Kimaendeleo Arusha Moshi iko juu sana.. Kielimu ndio usiseme huwezi iweka Tanga hapo.
Tanga imebarikiwa kwa mvua nyingi ardhi pia nzuri kwa kilimo cha matunda na vitu vingi pia.
Ndo maana tangu awali nilisema ni baraka au hatulijui hili neno maana yake? Nikaanza kulitumia "kujaaliwa". Baraka huwa zinakwisha, je kesho Mungu akiwabariki watu wa Moro, milima Uluguru yaweza kuwa mirefu kuipita mt. Klm?

Elimu ni juhudi si baraka, wamasai today nao wanasoma. Jamii zote zinawekeza ktk elimu kwa viwango tofauti, maendeleo pia ni juhudi za za kuzitumia fursa, si baraka. Waha wa Kigoma ni kabila linaloibuka kwa kasi ktk kuushika uchumi wa kibiashara Tz, hizi si baraka ni juhudi.

Ni jambo la kawaida tu, kesho ikawa si wachaga tena, wakinga tena wala waarabu bali wafipa. Wakiweka tu juhudi. Angola ilishalisaidia taifa la Ureno wakati wa anguko lake la kiuchumi.
 
Mzee Nyerere alisaidia sana. Kama sio yeye, kuna makabila mengi yangefutika apa Tanzania
Yangebaki makabila kutoka mikoa hiii
1. Kagera
2. Kilimanjaro
3. Mbeya
4. Mara Musoma
5. Mwanza, shinyanga (sukuma land)
6. Iringa, njombe (wanyaru)
Kwanini hukuuweka Mkoa wa Morogoro hapo? Unazijua elimu za mapri wewe? Wazijua shule mbili kuu kabisa za sekondari Tanzania, moja ya kike na nyingine ya kiume, tuliziita most high special schools?

Morogoro, walibase ktk elimu ya dini, Ila kwa wilaya kama Mahenge walizisoma zote, ukumbuke Mahenge na Moshi ni sawa kiuoto, na kimazingira. Kuliwavutia pia wazungu kusetle.

Ila la Nyerere, sawa alikuwa ni kiongozi aliyetimiza vyema dhima yake ya uongozi. Ndivyo ilivyopaswa kuwa. Kwani wasomi wa kwanza Tanzania wanatoka mikoa ipi kama si Pwani?

Pasi na wazungu leo wachaga na waarusha wasingetofautiana na wahadzabe, wangetembea uchi. Wakati huo mzalamo kwa zaidi ya miaka700 alishaanza kuvaa nguo na viatu, pia na kujifunza lugha ya maandishi.
 
Mzee Nyerere alisaidia sana. Kama sio yeye, kuna makabila mengi yangefutika apa Tanzania
Yangebaki makabila kutoka mikoa hiii
1. Kagera
2. Kilimanjaro
3. Mbeya
4. Mara Musoma
5. Mwanza, shinyanga (sukuma land)
6. Iringa, njombe (wanyaru)
We unaitaja Mara unaiacha Moro kweli? Hata historia ya nchi huijui vyema, akina Zuberi Mtemvu, chief Kunambi huijui michango yao kwa Nyerere.
 
Ndugu zangu wazaramo akiamia mtu mwenye uwezo yeye, anauza anakimbia kijijini, sehemu ambayo atapata pori la kuwaweka unyago na jando kwa watoto wa kiume.
Dar es salaam Tanzania, wazaramo wote wamekimbilia mikoa ya Pwani, na sasa ivi watu wanawafata mikoa ya Pwani, sijui watakimbilia wapi tena
Hakika nawaambieni, kwakuwa mwisho wa siku ni kifo, ktk Tanzania hakuna kabila litakalolipita la wazalamo kati ya yalioishi maisha meaningful. Free from stress. Hata hivyo, mifumo inabadilika. Nao wanachange pia.
 
Rungwe.
Kwani hujasoma jiografia Mkuu!?
Ni mlima wa volcano na udongo kwenye miguu ya mlima huo unafanana sana na udongo ulio miguuni mwa mlima K/njaro na ndio maana wanalima mazao yanayoshahabiana. Mf. Chai, kahawa na ndizi.
Watu Tz hawaijui Mkuu, hawazijui historia wala jiografia. Mi nadhani kwa maeneo machache sana yenye neema ya maisha Tukuyu kama haiongozi basi ni tatu bora.
 
Umeandika maneno mengi afu ukasahau "Amen"
Kwakuwa siamini ktk baraka Mkuu! Wakibarikiwa wa Meatu leo vichuguu vyao haviwezi badilika na kuwa milima mirefu zaidi wa KLM. Israel ilibarikiwa ilipopotota baraka zikapokwa pia. So mlima si baraka.
 
Kila mwenyeji wa mji fulani atapabariki anapotoka tena kwa majigambo ya kumshirikisha Mungu...
 
Ila hizi picha walizopost ni kama za miji ya Kilosa au Ifakara, wilaya za Morogoro. Tofauti ni milima tu hapo nionavyo.
 
We unaitaja Mara unaiacha Moro kweli? Hata historia ya nchi huijui vyema, akina Zuberi Mtemvu, chief Kunambi huijui michango yao kwa Nyerere.
Kwa iyo Mara na Morogoro ni sawa,
Mara tunazungumzia watu waliojitoa katika tasnia ya ulinzi, kama jeshini, achana na wachaga wanaoingia sasa ivi kwa ajili ya kwenda kupiga dili
 
Kwa iyo Mara na Morogoro ni sawa,
Mara tunazungumzia watu waliojitoa katika tasnia ya ulinzi, kama jeshini, achana na wachaga wanaoingia sasa ivi kwa ajili ya kwenda kupiga dili
Mara ilijitoa kuulinda Uhuru si kuupigania. Hata sapoti kubwa Nyerere sidhani kama aliipata kule, kwa kipindi walikuwa uncivilized societies kule. Wajanja wa mjini ni mikoa ya Pwani, kidogo Tabora. KLM walikuwa na Chief Mareale, lakini mwanzoni alikuwa mpinga Uhuru then akageuza gia angani akitaka apewe Uhuru wa Tanga, KLM na iliyokuwa Arusha.
 
Back
Top Bottom