kwa wale wapenzi wa kubeti kupitia meridianbet,nina ujumbe wenu.
jamani tafadhalini,kama una hela na unataka kubeti kupitia meridianbeti,sikushari ufanye hivyo maana ghafla wamekuwa matapeli,nime deposit 30000 ili niweke timu zangu za uhakika tokea tarehe 3/11 pesa ikapotea.
nikawasiliana na vodacom,wakajibu wao walishawafikishia hiyo pesa meridian,niwatafute meridian.nikawatafuta instagram,imail,wakaniambia niwatumie sms za uthibitisho nikatuma,nisubiri saa 72 sikuona pesa.nikaanza upya kuwataarifu wakaniambia tena nitume sms kwa kisha nisubiri saa 72,nikatekeleza na kusubiri saa 72,sijaona hela mpaka leo.
ikabidi nitumie simu ya mkononi,hawapokei simu,nimejiunga dakika 30 nasikilizishwa matangazo mpaka zinaisha simu hawapikei.nikaongeza nyingine 30 labda wametingwa na wateja bado hawakupokea,hapa ndipo mzee mzima nikajua ni rasmi sasa nimetapeliwa hela yangu.
kama kuna njia nyingine za kudai hiyo pesa tusaidiane jaman makamalia wenzangu,nadhani mnafahamu ni jinsi gani shilingi mia 200 ni kubwa kwenye huu mchezo achia mbali elfu 30.