Naona vita ya waomba buku na waombwaji imeanza.
Kuomba sio kitu kibaya ila huwezi kumparamia mtu ambaye hamjuani ukamwomba, mtu wa karibu ndio solution namba 1.
Kingine mtu akikuomba kama hauna unasema tu hauna, kama unayo na hautaki kumpa unanyamaza tu. Ukimkashifu anajisikia vibaya hasa wakikumbuka wana vyeti kabatini tena walikuwa mawaziri huko walikopata vyeti, huku wanajaribu kutafuta bahati tu.
Kuna vijana wanaishi kwa kutegemea betting kitu ambacho sio sahihi. Ni vema ukawa na kazi ya kukuingizia kipato hata kama ni kidogo kwa siku halafu ukawa unatengeneza matreni yako ya 100 huko betpawa.