Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

We chizi kweli!!!!🤣🤣🤣🤣
 
Wewe bado hujatembea. Ulishawahi kusikia kuna mtu ameenda kutafuta maisha Kilimanjaro?
 

Kwahiyo dsm inawatu 17% yawatanzania!?.
 
Nafkiri bado haujajua matukio ya Kanda ya Ziwa....Sumbawanga ni jina ...
Ila kuna maeneo ni watabe...
 
Hiyo mbeya mnaisifiaga sijui kwa kipi..mara Mia hata songwe
Well,Mbeya
  • Ya tatu kwa uchangiaji katika pato la Taifa
  • Ina chakula kingi
  • Wilaya zote zimeunganishwa kwa rami
  • Ina vyuo vikuu takribani 6
  • Ina miundombinu ya aina zote :Meli,Mabasi Barabarani,Reli,Ndege,
  • Ina Miji mikubwa miwili :Mbeya Jiji,Kyela
  • Ina shule nyingi na zenye kuongeza kitaifa katika ufaulu
  • Ina vyuo vikuu takribani vitano
  • Ina Hospitali kubwa 3
  • Makao makuu ya Kanda
  • Ina Uchimbaji wa madini
  • Ina Viwanda vingi
  • Ina soko kubwa la mazao
  • Ina stendi kubwa ya mabasi
Katika hivyo vyote nilivyotaja,wapi Songwe imeipita Mbeta
 
Wewe bado hujatembea. Ulishawahi kusikia kuna mtu ameenda kutafuta maisha Kilimanjaro?
Yeah,,,
Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa ambayo kuna ujenzi wa kutosha wa nyumba za kifahari....watu wa tasnia ya ujenzi wengi wanapiga pesa kule....

Kwenye utalii,,Rombo Kuna mlima Kilimanjaro na maji moto,maporomoko ya maji,Same napo hivyohivyo ...watu wa Sekta ya utalii wengi wameenda huko....

Kilimanjaro imeajili walimu wengi mana ni moja ya mikoa mi5 yenye shule nyingi nchini
 
Karatu juzi tu hapo nimepita kuna mafuriko mpaka barabara zimefungwa au karatu ipi!!?
 
Wilaya zipi hizo mkuu maaba nataka nikimbilie huko
Tanga ipo vizuri sana kwa Kilimo....inalima
Mazao ya matunda ya citrus (machungwa,chenza,ndimu,limau),mahindi na inalima mazao ya viungo vya chakula,mkonge....
Handeni,Pangani,na Lushoto....
Ila
Tanga mjini pamepoa sanaaaa....yani kama wagosi walivyoimba....
 

Mkuu, Wengi wenye chuki na Zanzibar ni wanaotoka Kaskazini na kanda ya ziwa. Hata hapa DSM wanajifanya kuvimba sana
 
Wewe bado hujakaa Arusha wewe. Yani Arusha hakuna maji? Chakula gharama? Yani ilitakiwa Arusha ndio iwe ya kwanza. Dar inaongoza kwa wingi wa watu na mzunguko wa pesa basi. Vingine vyote ni kizungumkuti. Maji shida, usafiri tabu, joto kama tanuru, we mzima kweli kichwani?
 
Karatu juzi tu hapo nimepita kuna mafuriko mpaka barabara zimefungwa au karatu ipi!!?
Sasa barabara kufungwa kisa maji,,,inatokeaga kila mkoa...
Sasa hivi hapa :Barabara ya Mtwara kwenda Lindi kuna kipande kimesombwa maji...ukarabati waendelea.

Mwaka juzi kuna kipande cha Barabara kwenda Moshi kilisombwa na maji, pale Korogwe......

Kila kipindi cha mvua kuna kipindi cha barabara kwenda Dodoma mjini kutoka Gairo huwa hakipitiki kisa barabara kujaa maji.....

Pale Babati,,mvua zikiwa kubwa Ziwa Babati hujaa maji mpaka kupeleka maji kwenye barabara ya kuingia Babati,pale kabla ya Mahakamani....

Yani ,hauwezi ukasema Arusha prone to Mafuriko,itakuwa masihala....
Lazima uelewe kuwa mvua za safari hii zimezidi kipimo.
 
Mzee ingia youtube andika mafuriko karatu ujionee maana mimi siwezi kuandika aya ndefu kitu ambacho hata kwenye vyombo vya habari walionyesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…