Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

Morogoro iko poa sana maswala ya msosi
 
A-Town siyo mkoa ni Wilaya mkuu....
 
Dodoma is the best,,kwanza hamna milima milima inayouwa vyombo vya moto,,,hali ya hewa nzuri hamna mb'u kwasababu hamna mvua nyingi..

Dodoma imepangika sema shida kubwa ni mvua zikinyesha njia zinakua na madimbwi kinyamaa.

Miundombinu bado mingi ni mipya mipya.

Jiji lina vijana wengi mno kuliko wazee. Interaction kubwa makabila mengi wagogo washapotea uku
 
Ni mwaka jana miezi km hii monduli ilipigwa mafuriko, halafu miinuko ya Arusha haifanani na Mbeya muachage uongo,
 
Ni mwaka jana miezi km hii monduli ilipigwa mafuriko, halafu miinuko ya Arusha haifanani na Mbeya muachage uongo,
Je ,mkoa wa Mbeya mzima umeinuka....
Hata katika Jiji la Mbeya, pale mbalizi ni tambalale mpaka kule ifisi....pale Iwambi kote ni tambarale kulempaka kwenda iyunga, pale Nzonvwe kwenda Ndenyela kote ni tambalale....
Je,Kwa Mrefu ipo bondeni, pale Sakina ni bondeni, kule Baraa ni papo chini...Je,Kijenge ipo tambarare...?
Na hakuna mkoa usioathiriwa na mvua ikiwa kubwa katika nchi hii....
 
Nimezunguka na kufanya kazi mikoa kibao , chaguo langu la kwanza Tanga pili Dar basi...Sasa hivi nipo kusini ila Tanga nitarudi kuweka makazi ya kudumu,
 
duh inashangaza. meru nimeishi na ndio kwetu lakini sitaki kuishi huko kabisa. mimi naipenda sana Iringa na Kagera. sema Kagera mwisho wa dunia huko
Meru kule kuna hospital karibu na mlima nilienda huko nilipapenda sana
 
Dodoma futa kabisa kwenye list, huo mkoa si wakuishi ni ukame Kila kitu kinatoka singida, Iringa na morogoro. Hivyo maisha ya Dom ni gharama maana unaishi jangwani .
labda umeambiwa tu ila hujawahi kuishi mkoa wa Dodoma wewe😀😀 ...Mahindi na nafaka yanalimwa kwa wingi Kondoa,Itiso,Kibaigwa,Mlali,Mkoka,Kongwa huko ndio wamejengewa soko la kimataifa la mahindi Kibaigwa plus ranchi kubwa ya mifugo kuliko zote East Africa ya Narco Kongwa. Alizeti inalimwa kwa wingi katika wilaya zote(Dodoma imepitwa na Singida pekeyake kwa uzalishaji wa Alizeti Tanzania).
-Mpunga unalimwa kwa wingi wilaya ya Bahi kwenye bonde la Mto Bubu na bwawa la Sulungai(infact mchele wa Bahi ni mojawapo ya mchele bora apa Tanzania ukienda soko lolote hata beiyake ipo juu)
 
Hali ya head, maji yana chumvi unaiwekaje Dodoma,?
Hali ya hewa ya mkoa wa Dodoma ni the best kwasababu sio joto kali wala baridi kali ndiomana watumishi wengi wa serikali wakitoka mikoa yenye baridi kali wanapenda hali ya hewa ya Dodoma...na uzuri hali ya hewa ya Dodoma ni moderate imegawanyika marambili kwa mwaka kuna miezi ya joto kuanzia septemba hadi april halafu kuna miezi ya baridi kuanzia Mei hadi Agosti.
Kuhusu maji ya chumvi nadhani Dodoma wana afadhali kubwa kuliko Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo huko wakaazi wake zaidi ya asilimia 80 wameoza meno au meno kuwa ya rangirangi kutokana na maji ya chumvi+fluoride nyingi...Dodoma huwezi kukuta hiyo kitu
 
hapa kuna kitu mnaruka na nafsi zenu haziwaelewi! hivi kweli singida na Manyara hamkuona hata wale watoto wazuri ambao River Side enzi zile akiwaleta bar mwezi mmoja wote wameolewa na wanakuwa wateja wanamtuma yeye na hela zao.(anawaleta wakiwa wamechanganyika na mbuzi sasa ngoja wajue kuoga kwa foleni na ingekuwa sasa wajifunze kucheza kwaito na kunywa wine kwa kuiramba sio kama wanakunywa maji ya kunywa)
 
Kwa mkoa wa kuishi Arusha haunishauri.
Morogoro is 1000 better than Arusha in all aspects.
Maana Morogoro maisha rahisi,hali ya hewa nzuri naweza sema kuliko Arusha hususan ukitembelea Matombo,Kisaki na Mvuha huko uone matiririko ya mto Mmbezi.
Pia Morogoro ni Mkoa wa kistaarabu sio kama Arusha mji wa vijana WAVUTA BANGI,WALEVI NA WAPENDA NGONO NA WAKOROFI.
Dar ni financial hub ya Tz,kuna kila aina ya maisha.
Kuna kila aina ya makazi unayotaka wewe.
Tembelea Mbagala kuu/Kijichi,Somangira na Kisota Kigamboni uone mandhari nzuri,safi na inayovutia.
Huwenda umekaa Tandale mkuu ukasema Dar yote inanuka.
 
Dodoma ipi mkuu!?
Dodoma labda huko mjini Swaswa,Ipagala na Kigamboni.
Ila nenda Ilolo Mpwapwa,Kibaigwa ingia ndani Msisigwa na Laikani.
Kuna mbu sijawahi ona.
Umeisemea Dom mjini ila sio vijijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…