Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

Mikoa 10 bora ya kuishi Tanzania

Ifuatayo ndiyo orodha ya mikoa 10 bora ambayo :
Ambapo binafsi nimeipangilia kwa kuangalia
  • Upatikanaji wa chakula
  • Urahisi wa Usafiri
  • Elimu
  • Hali ya Hewa
  • Huduma za maji
  • Mitandao ya simu
  • Usalama
  • Biashara
1. Dar es Salaam
Ndiyo mkoa ulioendelea Tanzania kuliko yote.
17% ya watanzania wapo katika mkoa huu...Biashara yako ikikubalika mkoani hapa ujue nchi nzima imekukubali.
Shida pekee ya Dar ni hali ya hewa yake kuwa joto kali.
Pesa yako itakufanya uishi maisha ya kifahari ama ukaishi sehemu duni.

2. Mwanza
Unaukaribia mkoa wa Dar kwa kila sifa tajwa hapo juu. Ukiwa hapa,unakuwa karibu Kenya na Uganda.
Wingi wa vyuo,uwepo wa maji na huduma za hospitali.

3. Mbeya
Mkoa wenye utajiri wa chakula ,hali ya hewa ya kuvutia na upatikanaji rahisi wa huduma za elimu na afya.
Mita inatiririsha maji kila kona.
Shida ya huu mkoa ni usalama finyu barabarani (una ajali za kutosha).
Pia usalama finyu majira ya usiku wa manane....una Viji matukio flani hivi ya kibabe.

4. Iringa
unafuu katika chakula,una shule za kutosha na vyuo.
Shughuli za Biashara za kilimo na Mbao.
Huduma za afya nzuri zipo mijini, na nyingine zinafutwa Mbeya au Dodoma.

5. Arusha
Mkoa wenye moja ya majiji makubwa hapa nchini.Una wingi wa Hospitali, Makazi,Shule na Vyuo.
Ila gharama ya chakula katika huu mkoa ni kubwa mno.
Na hata kwenye ujenzi ,gharama ni kubwa sana
Pia kuna shida ya upatikanaji wa huduma za maji. na kuna baadhi ya maeneo katika huu mkoa ni kame.

6. Ruvuma
Huu mkoa una wingi wa chakula na bei nzuri.Una biashara na nchi jirani.Maji na umeme siyo shida.
Ila bado hakuna barabara za kutosha,upungufu wa vyuo

7. Kilimanjaro
Upo juu kwenye kiwango cha elimu na ubora wa elimu. Una huduma nzuri za afya na maji.Mzuri kwa biashara za utalii.
Ila kuna ugumu wa kupata ardhi kwa baadhi ya Wilaya, Gharama ya vyakula.


8. Dodoma
Ukiondoa Wilaya ya Dodoma ambayo kuna uboreshaji wa miundombinu kwa halia ya juu,na ujenzi wa kutosha tena wenye kupangika.
Lakini nje na hapo kuna shida ya maji,ardhi kame.

9. Njombe
Unataka biashara ya mbao,Viazi,Parachichi au Viazi nenda kwenye huu mkoa. Bado una ardhi ya kutosha ,una hali ya hewa nzuri.
Bado kuna uchache wa shule na huduma za afya.
una kiwango kikubwa cha maambukizi ya Ukimwi.

10. Unguja
Kupo vizuri kwa biashara,kuna vyuo vya kutosha na huduma za afya.
Barabara na huduma za maji.
Ila
Kwa mtu wa bara atapata ugumu kwenye
  • Aina za vyakula
  • Udini
  • Uhitaji wa vitambulisho
  • Leseni ya udereva kutokukubaliwa
  • Kubaguliwa kwenye baadhi ya huduma.

NOTES
Mikoa ambayo sijawahi fika ni Katavi,Mtwara,Geita,Rukwa,Mara,Pemba na Kigoma.
Mpangilio kulingana na niliyo yaona katika mikoa husika.
Unaweza weka orodha yako.
Morogoro iko poa sana maswala ya msosi
 
Watu mna list tu mikoa Yenu. Hakuna mkoa Bora kuishi kama A- Town. Dar ni joto na miharufu ya ovyo. Kila sehemu ni chafu. Sehemu nyingine ni njombe japo Kuna baridi lakini maisha ni rahisi. Kanda ya ziwa labda kagera ila mikoa mingine ni njaa tu, Dodoma futa kabisa kwenye list, huo mkoa si wakuishi ni ukame Kila kitu kinatoka singida, Iringa na morogoro. Hivyo maisha ya Dom ni gharama maana unaishi jangwani .
A-Town siyo mkoa ni Wilaya mkuu....
 
Dodoma is the best,,kwanza hamna milima milima inayouwa vyombo vya moto,,,hali ya hewa nzuri hamna mb'u kwasababu hamna mvua nyingi..

Dodoma imepangika sema shida kubwa ni mvua zikinyesha njia zinakua na madimbwi kinyamaa.

Miundombinu bado mingi ni mipya mipya.

Jiji lina vijana wengi mno kuliko wazee. Interaction kubwa makabila mengi wagogo washapotea uku
 
Nafkiri bado haujawahi izunguke Arusha...
Wilaya ya Longido na Monduli,kamwe haiwezi kumbwa na mafuriko, mana ni kame sana.
Wilaya ya Karatu sahau,,,
Hapo
Arusha mjini sehemu zenye kujaa maji ni chache sana,,,yaani sana
labda Wilayani Meru
Yani unavyoina Mbeya mjini na miunuko, ndiyo sawa na Arusha mjini....
Ni mwaka jana miezi km hii monduli ilipigwa mafuriko, halafu miinuko ya Arusha haifanani na Mbeya muachage uongo,
 
Ni mwaka jana miezi km hii monduli ilipigwa mafuriko, halafu miinuko ya Arusha haifanani na Mbeya muachage uongo,
Je ,mkoa wa Mbeya mzima umeinuka....
Hata katika Jiji la Mbeya, pale mbalizi ni tambalale mpaka kule ifisi....pale Iwambi kote ni tambarale kulempaka kwenda iyunga, pale Nzonvwe kwenda Ndenyela kote ni tambalale....
Je,Kwa Mrefu ipo bondeni, pale Sakina ni bondeni, kule Baraa ni papo chini...Je,Kijenge ipo tambarare...?
Na hakuna mkoa usioathiriwa na mvua ikiwa kubwa katika nchi hii....
 
Hakuna mkoa bora wa kuishi kama tanga
Vyote ulivyotaja vipo, bandari, mpaka na inchi jirani, ardhi safi, viwanda, matunda, chakula na kila chema
Sema ni serikali iiwache tu, isiibane kwa sababu wanazozijua za kudhoofisha.

tanga itakuwa mbali sana

Zamani ilikuwa ndio kimbilio la wengi kabla ya kuminywa kiaina kutokana na... au basi acha tu
Nimezunguka na kufanya kazi mikoa kibao , chaguo langu la kwanza Tanga pili Dar basi...Sasa hivi nipo kusini ila Tanga nitarudi kuweka makazi ya kudumu,
 
duh inashangaza. meru nimeishi na ndio kwetu lakini sitaki kuishi huko kabisa. mimi naipenda sana Iringa na Kagera. sema Kagera mwisho wa dunia huko
Meru kule kuna hospital karibu na mlima nilienda huko nilipapenda sana
 
Nyie nao punguzeni ushamba hyo Dar ina nn cha ziada sasa
1715094805889.png
 
Dodoma futa kabisa kwenye list, huo mkoa si wakuishi ni ukame Kila kitu kinatoka singida, Iringa na morogoro. Hivyo maisha ya Dom ni gharama maana unaishi jangwani .
labda umeambiwa tu ila hujawahi kuishi mkoa wa Dodoma wewe😀😀 ...Mahindi na nafaka yanalimwa kwa wingi Kondoa,Itiso,Kibaigwa,Mlali,Mkoka,Kongwa huko ndio wamejengewa soko la kimataifa la mahindi Kibaigwa plus ranchi kubwa ya mifugo kuliko zote East Africa ya Narco Kongwa. Alizeti inalimwa kwa wingi katika wilaya zote(Dodoma imepitwa na Singida pekeyake kwa uzalishaji wa Alizeti Tanzania).
-Mpunga unalimwa kwa wingi wilaya ya Bahi kwenye bonde la Mto Bubu na bwawa la Sulungai(infact mchele wa Bahi ni mojawapo ya mchele bora apa Tanzania ukienda soko lolote hata beiyake ipo juu)
 
Hali ya head, maji yana chumvi unaiwekaje Dodoma,?
Hali ya hewa ya mkoa wa Dodoma ni the best kwasababu sio joto kali wala baridi kali ndiomana watumishi wengi wa serikali wakitoka mikoa yenye baridi kali wanapenda hali ya hewa ya Dodoma...na uzuri hali ya hewa ya Dodoma ni moderate imegawanyika marambili kwa mwaka kuna miezi ya joto kuanzia septemba hadi april halafu kuna miezi ya baridi kuanzia Mei hadi Agosti.
Kuhusu maji ya chumvi nadhani Dodoma wana afadhali kubwa kuliko Arusha,Manyara na Kilimanjaro ambapo huko wakaazi wake zaidi ya asilimia 80 wameoza meno au meno kuwa ya rangirangi kutokana na maji ya chumvi+fluoride nyingi...Dodoma huwezi kukuta hiyo kitu
 
Singida
  • Kielimu ipo nyuma:vyuo vichache, hata wenyeji kielimu pia muamko mdogo
  • Ardhi kane
  • Maji shida
  • Hali ya hewa mh....
  • Huduma za Afya bado
  • Shughuli za uchumi ndogo
Manyara
Babati ni Wilaya nzuri ina potential kwa miaka ijayo...na hali ya hewa safi sana...
Ila kanakwamba huduma ya ku-print A3 ya rangi ipo sehemu moja tu,jua bado maendeleo...
Wilaya ya Simajiro ni kame sana ...
hapa kuna kitu mnaruka na nafsi zenu haziwaelewi! hivi kweli singida na Manyara hamkuona hata wale watoto wazuri ambao River Side enzi zile akiwaleta bar mwezi mmoja wote wameolewa na wanakuwa wateja wanamtuma yeye na hela zao.(anawaleta wakiwa wamechanganyika na mbuzi sasa ngoja wajue kuoga kwa foleni na ingekuwa sasa wajifunze kucheza kwaito na kunywa wine kwa kuiramba sio kama wanakunywa maji ya kunywa)
 
Watu mna list tu mikoa Yenu. Hakuna mkoa Bora kuishi kama A- Town. Dar ni joto na miharufu ya ovyo. Kila sehemu ni chafu. Sehemu nyingine ni njombe japo Kuna baridi lakini maisha ni rahisi. Kanda ya ziwa labda kagera ila mikoa mingine ni njaa tu, Dodoma futa kabisa kwenye list, huo mkoa si wakuishi ni ukame Kila kitu kinatoka singida, Iringa na morogoro. Hivyo maisha ya Dom ni gharama maana unaishi jangwani .
Kwa mkoa wa kuishi Arusha haunishauri.
Morogoro is 1000 better than Arusha in all aspects.
Maana Morogoro maisha rahisi,hali ya hewa nzuri naweza sema kuliko Arusha hususan ukitembelea Matombo,Kisaki na Mvuha huko uone matiririko ya mto Mmbezi.
Pia Morogoro ni Mkoa wa kistaarabu sio kama Arusha mji wa vijana WAVUTA BANGI,WALEVI NA WAPENDA NGONO NA WAKOROFI.
Dar ni financial hub ya Tz,kuna kila aina ya maisha.
Kuna kila aina ya makazi unayotaka wewe.
Tembelea Mbagala kuu/Kijichi,Somangira na Kisota Kigamboni uone mandhari nzuri,safi na inayovutia.
Huwenda umekaa Tandale mkuu ukasema Dar yote inanuka.
 
Dodoma is the best,,kwanza hamna milima milima inayouwa vyombo vya moto,,,hali ya hewa nzuri hamna mb'u kwasababu hamna mvua nyingi..

Dodoma imepangika sema shida kubwa ni mvua zikinyesha njia zinakua na madimbwi kinyamaa.

Miundombinu bado mingi ni mipya mipya.

Jiji lina vijana wengi mno kuliko wazee. Interaction kubwa makabila mengi wagogo washapotea uku
Dodoma ipi mkuu!?
Dodoma labda huko mjini Swaswa,Ipagala na Kigamboni.
Ila nenda Ilolo Mpwapwa,Kibaigwa ingia ndani Msisigwa na Laikani.
Kuna mbu sijawahi ona.
Umeisemea Dom mjini ila sio vijijini.
 
Back
Top Bottom