Mikutano mikubwa ya kimataifa Tanzania lazima ifanyikie Arusha na Dar tu?

Mikutano mikubwa ya kimataifa Tanzania lazima ifanyikie Arusha na Dar tu?

Mwanza ni porini??
Mwanza hakuna mahoteli makubwa ya kutosha hata mkutano wa SADC?
Miundo mbinu sio Hoteli tu, pia Barabara ni finyu saana na wabunge wa huko wameshindwa kusimamia mipango miji, wawe na mabarabara, sio barabara. Na waanze sasa . Na maegesho ya magari ya wageni na wenyeji
 
Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?
Dar ndio Kuna facilities zote ambazo zinaendana na hadhi ya Marais.

Hivyo Vijiji vingine fanyieni makongamano ya dini 😆😆

Mwisho nimewahi kutoa hoja ya Serikali kuwekeza kwenye Mikoa ambayo ni Makao Makuu ya Kanda Ili iwe vitovu vya maendeleo Kwenye Kanda husika na kuleta uwiano wa kimaendeleo ila wewe ulikuwa wa kwamba kupinga.

Nimekuwa natolea mfano wa Dar kwamba Kila kitu ni hapo tuu lakini kuna Mikoa haijaungwa na lami Mkoa kwa.mkoa.na hakuna anaejali.

Sasa hizi ndio athari zake.Tunywe hivyo hivyo maana tumetaka wenyewe
 
Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?

Ulitaka wakafanyie Lindi au Mtwara!?
 
Mwanza? Huko porini marais utawalazs wapi. Arusha na Dsm ni miji ya kimataifa. Mwanza ni mji wa washamba. Unawezaje kulinganisha Arusha na Mwanza? Arusha in mahoteli makubwa ya kimataifa ht kuliko Dar. Labda uzungumzie Zanzibar
huijui mwanza acha kuropoka ropoka
 
Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?
Usisahau Jiji la Mbeya Tena kuna Hali ya baridi kama Njombe!Ambayo inaendana na Ulaya.
 
Haina hata pa kulaza wageni wa kitaifa,let alone wa kikanda na kimataifa. Hata mikutano mikubwa ya mashirika ya kitaifa yanashindwa kufanyika Mbeya. Hakuna CEO wala wasaidizi wake wanakuelewa ukipendekeza mkutano ufanyike Mbeya. Lakn ukitaja Arusha, watu wanapiga makofi.
Usisahau Jiji la Mbeya Tena kuna Hali ya baridi kama Njombe!Ambayo inaendana na Ulaya.
 
Ni vipaumbele tu...

Arusha kwasababu ya kuhamasisha utalii...

Dar kwasababu ya kimazoea tu...

Mwanza na Dodoma zina hadhi pia ya kuandaa mikutano ya aina hiyo, kwasababu kumbi na hoteli zipo...
 
Back
Top Bottom