Mikutano mikubwa ya kimataifa Tanzania lazima ifanyikie Arusha na Dar tu?

Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?
Tena inapaswa kufanyika Arusha na sio huko Dar kwenye hali mbaya ya hewa, joto na msongamano wa magari na watu.
 
Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?
Uwanja wa ndege wa kimataifa,kumbi za mikutano na hotel za kutosha za nyota tano utapata wapi kwingine?
 
Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?
Waje wafanyie mikutano yao na huku kwetu kizimkazi maana kwa sasa tuna kila kitu
 
Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?
Mara ijayo pendekeza kijiji unachotoka alafu wasikilizie wafanya maamuzi,unaweza ukaokota dodo kijiji chenu kikageuka kama Chato au Kizimkazi
 
Mwanza na mbeya hazijafikia hadhi ya kuitwa jiji.arusha tu inajikongoja.mwanza ni manispaa
Arusha huwezi kuifananisha na Mwanza.
Kila kilichopo Arusha Mwanza pia kipo na zaidi.
Mikutano hupelekwa Arusha kwa sababu ya hali ya hewa, ukumbi mkubwa wa mikutano wenye hadhi ya kimataifa AICC na pia kupromoti utalii.
Lakini kwa ukubwa na hadhi, jiji la Mwanza liko mbali zaidi ya Arusha.
 
Mwanza imekaa kishamba sana. Uwanja ndege uko sawa na wa Singida. Hotel za maana hakuna, watu wachafuwachafuuu
 
Mwanza Airport ni sawa KIA,
Marais wa nchi masikini za Africa hawawezi kulala hotel za nyota 3 ?
Kuna protocoll. Huwezi kuwalaza Wakuu wa Nchi kwenye hoteli za nyota 3.
 
Mwanza imekaa kishamba sana. Uwanja ndege uko sawa na wa Singida. Hotel za maana hakuna, watu wachafuwachafuuu
Wachafu kivipi? Wewe una dhana ya Ukabila na ujinga!
Mwanza iko hapo kwa juhudi kubwa ya wakazi wake!
Dar es Salaam ,Arusha na Dodoma zimejengwa na serkali ila Mwanza inapambana kivyake na bado ina ukubwa wa kufata Dar es Salaam!
 
Arusha huwezi kuifananisha na Mwanza.
Kila kilichopo Arusha Mwanza pia kipo na zaidi.
Mikutano hupelekwa Arusha kwa sababu ya hali ya hewa, ukumbi mkubwa wa mikutano wenye hadhi ya kimataifa AICC na pia kupromoti utalii.
Lakini kwa ukubwa na hadhi, jiji la Mwanza liko mbali zaidi ya Arusha.
Sijawahi ona upuuzi kama huu.kwamba watu wa mikutano unawajua wakoje?? Wanamuda na utalii wamekuja kusuluhisha majanga ya vita? Mwanza bado sana hata hotel za kubeba watu 5000 wazungu hakuna ,arusha kuna hotel kama grand meria kuna hadi vyumba vya mil 10 kwa siku ,vyumba vya mil 2 hadi 5 mwanza nzima ukihesabu havifiki 40 ,ila arusha huwa zinashuka ndege za marais hata 50 na wote wanalala 5star hotel ,level hiyo ya hotel mwanza ziko nne tuu.au unadhani mtu wa kimataifa anaweza kulala pake malaika pachafu.mwanza nzima viwanja vya golf vinazidi vinne??? Eti hali ya hewa si wangeenda iringa??kwanza mwanza ina hali ya hewa mbaya???
Mm nakuja sana mwanza nakaa hata mwezi huwa bado ni kijijin hata moro imechangamka zaidi afu mwanza mjini padogo unaimaliza skuiyo iyo.mwanza migahawa ya kahawa ya maana inazidi 40 kweli?.
Utoto mwingine et ili kusapot utalii yaani uache kusaport utalii mwanza kwenye vivutio vya kutosha watalii hawavijui upeleke ambako wazungu wanapajua na wazungu ni wakazi wa arusha tunaishi nao njiro.
Kingine mwanza wakazi hawajasoma wengi wao mpaka leo mwanza mjini wanaongea kisukuma .wakati arusha vijana wanaongea kifaransa,kijerumani skuizi wanabidii wanajifunza kichina.
Niliwahi kuwa casky show ya rayvan asee nilikuwa nashangaa watu wanamuona rickross.wakati arusha tuko nae baa na kina mafidoo kila siku
Kaka nakiri mwanza ina rasilimali na ardhi ya kutosha kuipiku hata dar ila nakuhakikishia kwa sasa bado sana sana sisi huwa tukijanhuko tunaona tuko kijijini
 
Wewe hata kuwasilisha mawazo yako kwa kuandika tu changamoto utaweza kujua mambo mazito kama hayo!.
Arusha unayoisema ina hotel nyingi kubwa wakati huo Mwanza haina na umefikia hatua ya kusema Malalika Beach Resort ni chafu na haina hadhi ya kufikia Wageni!
Mji wa Arusha kutokana na hali yake na ukaribu na hifadhi ndo maana serkali ilionelea kujenga Arusha International Conference Center na kufanya kitovu cha utalii kwa kanda ya Kaskazini!
Mambo hayo yasikufanye kuidharau Mwanza huku ukiwasimanga wana Mwanza kuwa bado wanaongea Kisukuma mjini na Arusha wanaongea Kingereza,Kichina na Kifaransa!
Ila najiuliza mara ngapi naenda Arusha sikuwahi kuona mtu wa kawaida anaongea kingereza tofauti na kuwaona Waarusha na Wamasai wamebeba kuni na mashuka yao machafu mjini hapo!
Watu wengi humu mna presha kubwa sana na Mwanza kwa maana mnajua fika Mwanza ikipata Kumbi kubwa na International Airport itawabinya kwenye mambo mengi!
Mwanza ni giant kwa Arusha iwe kwenye GDP na ukuaji wa uchumi,hela ya Arusha kwa sehemu kubwa unakusavywa na wenye makampuni ya Utalii huku wananchi wa kawiada wakiwa hohehahe!
 
Mwanza imekaa kishamba sana. Uwanja ndege uko sawa na wa Singida. Hotel za maana hakuna, watu wachafuwachafuuu
Jiji lina watu milioni 3 na ushee utasemaje la kishamba!!
Arusha yenye watu laki 6 ndiyo ya kishamba zaidi.
Arusha imefika hapo pachache kwa msukumo wa Jumuiya ya Afrika mashariki, lakini kwa ushamba wa wana Arusha wameshindwa kutumia fursa hiyo kuimarisha jiji hilo kuizidi Mwanza.
Tambua mzunguko pesa Arusha unategemea msimu utalii, lakini Mwanza ni kama Dar hakuna msimu.
Mwanza inatumainiwa na mikoa yote mitano ya kanda ya ziwa, Arusha inategemewa mkoa gani zaidi ya Manyara?
 
Dodoma Ni Eneo La Wajumbe Wa CCM
Kuna Chumba Cha Giza Kufanya Maamuzi Yao
 
Sijawahi ona upuuzi kama huu.kwamba watu wa mikutano unawajua wakoje?? Wanamuda na utalii wamekuja kusuluhisha majanga ya vita?
We ndiyo mpuuzi zaidi,
Mkutano unafanyika Dar na si Mwanza wala Arusha.
Hoja yako kwamba Arusha ni jiji na Mwanza ni kijiji ndiyo niliyoijibu.
Ukumbi pekee wa mikutano AICC hautoshi kushusha hadhi ya Mwanza.
Mwanza bado sana hata hotel za kubeba watu 5000 wazungu hakuna
Nyie watu wa Arusha inaonyesha ni washamba sana.
Kwamba kwakuwa mnawaona wazungu wengi hapo basi inatosha kufanya Arusha iwe jiji na Mwanza ni kijiji?
Nenda Zanzibar ukaone wazungu.
Kingine mwanza wakazi hawajasoma wengi wao mpaka leo mwanza mjini wanaongea kisukuma .wakati arusha vijana wanaongea kifaransa,kijerumani skuizi wanabidii wanajifunza kichina
Wewe ni mshamba mpaka unatia kinyaa.
Kisukuma ni lugha kama kichina.
Tembea duniani ukaone.
Kila mmoja anajiheshimisha kwa lugha yake.
Mimi nitaongea lugha yangu, ni jukumu lako wewe mgeni kujua mimi nimeongea nini.
Mnakimbilia lugha za watu wakati hata kiswahili hamkijui, kwa kuwa nyi washamba.
Kaka nakiri mwanza ina rasilimali na ardhi ya kutosha kuipiku hata dar ila nakuhakikishia kwa sasa bado sana sana sisi huwa tukijanhuko tunaona tuko kijijini
Kwa kumalizia, mimi nimezaliwa Dar, naishi Dar, lakini nimefika Arusha na pia nimefika Mwanza.
Mwanza haitaifikia Dar kwa siku za karibuni, lakini pia Arusha haitaifikia Mwanza hivi karibuni.
Wana Arusha endeleeni kubebishana na vikongwe walioshindwa maisha ulaya.
 
Kwa nini mikutano mikubwa ya kimataifa inayofanyikia Tanzania haifanyikii mikoa tofauti kama Dodoma au Mwanza bali mara zote ni Dar es Salaam na Arusha tu?
Dodoma hakuna hoteli, Mwanza changamoto ni uwanja wa ndege, na Mbeya hakuna hoteli kubwa, Tanga ni kwa waswahili tupu huwezi kupeleka wageni wataanza kuwaloga
 
Mwanza? Huko porini marais utawalazs wapi. Arusha na Dsm ni miji ya kimataifa. Mwanza ni mji wa washamba. Unawezaje kulinganisha Arusha na Mwanza? Arusha ina mahoteli makubwa ya kimataifa ht kuliko Dar. Labda uzungumzie Zanzibar
Sema watu wa Arusha wanapasifia sana kwao, fika sasa ukajionee 😃
 
Back
Top Bottom