King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Kwanin hukumu wanaziandika kwa kiingereza?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mwenye picha ya huyu dayfath tuioneBaada Agosti 27, 2024 mahakama kutoa hukumu ya kesi tukio kuuawa kwa Milembe Maunga, na watuhumiwa watatu kukutwa na hatia, wakihukumiwa kunyongwa, kwa sasa napata fursa ya kulielezea tukio hilo kwa kina namna lilivyokuwa.
Yatakuwa maelezo marefu kidogo, ila nitajitahidi kulielezea lote kwa awamu hadi nifikie mwisho. Hivyo, nitakuwa nikiendelea kwenye eneo la maoni.
Naanza...
Mauaji ya Siri: Mapenzi, Wivu, na Kifo
USIKU ulikuwa umetulia sana huko Mwatulole, wilaya ya Geita, mnamo Aprili 25, 2023.
Milembe Suleiman Hungwe alikuwa amepanga mipango ya siku inayofuata, lakini hakujua kwamba huo ulikuwa usiku wake wa mwisho duniani.
Akilini mwake, hakukuwa na wasiwasi wowote. Kila kitu kilionekana kikiwa kawaida, lakini nyuma ya pazia, jambo kubwa lilikuwa linapangwa dhidi yake.
Ndani ya kuta za nyumba isiyoisha kujengwa, yaani pagale, iliyomilikiwa na Milembe, palikuwa na siri nzito. Siri iliyogubikwa na wivu wa kimapenzi.
Twende pamoja
Milembe, ni mwanamama imara aliyefanikiwa sana kazini kwake, nyuma ya maisha yake ya siri kulikuwa na jambo moja alilolificha kwa uangalifu mkubwa—uhusiano wake wa kimapenzi.
Milembe na Dayfath Suleiman Maunga hawakuwa tu marafiki wa kawaida. Kwa muda mrefu, walikuwa wapenzi wa jinsia moja (lesbian), uhusiano ambao waliishi nao kwa siri kubwa.
Katika jamii yao, uhusiano kama huo ulikuwa kinyume katika mila na desturi, jambo lililowalazimu kuficha hisia zao.
Dayfath alikuja kwenye maisha ya Milembe kwa njia ya kawaida—alianza kama mfanyakazi wake katika biashara ya duka la vipodozi la Milembe.
Lakini muda ulivyopita, hisia za kimapenzi zilianza kuchanua kati yao. Wakianza kuishi kinyumba maeneo ya Usagara, Mwanza, wakiishi na mama yake Milembe, msaidizi wa kazi za nyumbani, na baadhi ya ndugu.
Ulimwengu wao ulikuwa ni wa siri sana, lakini ni ulimwengu ambao siku moja binti wa Milembe, Grace Evarist Gervas, aligundua kitu kuhusu mama yake na Dayfath ambacho kilimshangaza sana.
Itaendelea...
Ova
Umeandika kitaalam sana b… Nimependa kila kitu, fanya umalize leo.Sehemu ya Nne;
Ndoa ya Siri yawa Shimo la Kifo
Maisha ya Milembe na Dayfath yalikuwa ni mafumbo. Uhusiano wao ulikuwa umevunjika, lakini hisia zilitawala zaidi.
Upendo wa Dayfath kwa Milembe ulibadilika kuwa wivu usio na mipaka. Alianza kuhisi kuwa Milembe anamwacha, akihofia kuwa alikuwa akipoteza nafasi yake.
Lakini badala ya kuachilia, alichukua uamuzi mgumu—wa kutafuta njia ya kumtoa Milembe kwenye maisha yake, kwa njia ya giza na kifo.
Baada ya majibizano na wivu uliokomaa, Dayfath alizungumza na Safari Lubingo, rafiki yake wa zamani, na wakapanga kutafuta wauaji.
Safari akampata Genja na Mussa—watu waliokuwa na mikono ya damu. Walipanga na kuamua kuwa siku ya tarehe 25 Aprili, 2023 ingekuwa ndiyo mwisho wa Milembe.
Baada ya kufika kwenye "site", Milembe aliagana na wanaume hao watatu; Genja, Mussa, na Safari, wakiwa wamejiandaa kwa kazi yao ya mwisho.
"Nitawaita baadaye, baada ya kumaliza mazungumzo." Milembe alisema, akiwa na matumaini kwamba kila kitu kitatendeka kama kawaida.
Lakini, asilokuwa akilijua, tayari mawimbi ya hatari yalikuwa yameanza kupiga chini ya maji, yasiyoonekana.
Muda ulipofika, Milembe aliwapigia simu. Wakajitokeza kwa kasi na kuingia kwenye eneo la ujenzi. Na ghafla kitu cha ajabu kikatokea.
Itaendelea...
Ova
Itakuwa ume-overlook MkuuMuwe mnasoma na kuelewa kilichoandikwa
Yeah! Saguda47 himself! Niaje mkuuSaguda de 47
Darling! Nimeumia kwa ajili ya huyo mtoto jamani!Tunaumiza sana watoto. Watoto wataishi na maumivu maisha yao yote.
Imagine mtoto kukua akiwa anajua mama alikuwa anatembea na KE mwenzie au baba alikuwa anatembea na ME mwenzie!
MmmmhhhUmeandika kitaalam sana b… Nimependa kila kitu, fanya umalize leo.
Nitakupa muda, japo jana umeniibia…
Nakupenda we hapo, and I miss you so much.
Nimecheka mno!PDF ina kila kitu ila imeandikwa katika ile lugha ambayo inatupiga chenga, ukizingatia Kiingereza chetu ni cha "She took my book, Tookn't she?".
Angalia asije na jamaa akakutafutia watu wa kuzindika nyumba yako na wewe.😀😀Umeandika kitaalam sana b… Nimependa kila kitu, fanya umalize leo.
Nitakupa muda, japo jana umeniibia…
Nakupenda we hapo, and I miss you so much.
Salama kabisaNiko fresh sana, vipi wewe hujambo
Babu hebu tupumzishe jamani, we tuition ya nini saa hizi? Au ndio ng’ombe hazeeki maini?Nilikuwa na mtazamo kwamba mabinti wa Mbeya hawana maajabu Kwa bed, ila wewe unataka kufanya nibadiri mtazamo...
Naomba nilipie hela ya Tuition ili uanze kunipa darasa ili kilaza Mimi nianze kuelewa somo 😜
Kwenye vijiwe vya gahawa walikuwa wanasemajeNilikuwa Geita kipindi huu ushenzi unatokea
Okay vizuri!Salama kabisa
There is no perfect forgery.Every crime leaves a trail behind