Milembe Alivyouawa Kwenye Pagale

Milembe Alivyouawa Kwenye Pagale

Kwenye vijiwe vya gahawa walikuwa wanasemaje
Mimi nilikuwa ni jirani wa huyo marehemu milembe, sote tulikuwa tunaishi Geita mjini mtaa wa general tires (nyakalembo) barabara inayoelekea mgodi wa GGM, nilisikia story vijiweni wakimsema kuwa ni mbabe japo pia alikuwa Na mpunga wa kula bata za hapa Na pale, alitembelea gari nyeusi Aina ya hariel old model, alikuwa akiingia kwenye kumbi za starehe akiwa Na wapambe nyuma yake, alikuwa akimpenda mwanamke wako wewe sema unataka shilingi ngapi ili akulipe Na wewe upite hivi, mara nyingi kwenye kumbi za starehe alizokuwa akifika milembe siku hiyo lazima fujo zitokee Na chupa zitapasuliwa haswaaa....sehemu alipokuwa akiweka kambi marehemu milembe hasa kwenye kumbi za starehe usisogee kama wewe ni dhaifu kwa sababu muda wowote kinanuka, alipenda kuwaita wanaume "washkaji zake" akikukubali salaam yake kwa wanaume alikuwa anawapa" tano" .................. Alimiliki grossari yake pale maeneo ya shilabela.
 
Attachments

  • Screenshot_20241023-154032_YouTube.jpg
    Screenshot_20241023-154032_YouTube.jpg
    142.3 KB · Views: 5
Sehemu ya Tano

Msaada wa Mauti

WANAUME hao watatu hawakuwa na hamu ya kumsaidia tena Milembe kwa "dua". Kwani Genja alitoa panga lake, lenye makali yaliyokuwa tayari kwa kazi ya kinyama.

Iliogopesha sana. Bila kusema neno, Milembe aliinyanyua mikono yake juu kwa hali ya kama kujisalimisha, na kutii amri zao zote tangu wakati huo.

Kwani aligundua kuwa amezungukwa na watu katili. Kwa wakati huo, mwanga wa mwezi uliangazia kwa mbali, ukiwa unampa Milembe kivuli cha kifo.

Pigo la Kwanza
Pigo la kwanza lilimfanya Milembe atazame kwa mshangao. Macho yake yalifumba kwa sekunde chache.

Kabla hajapata nafasi ya kutambua kilichotokea, damu nyingi ilianza kuchuruzika kwa kasi toka kwenye jeraha la kichwa.

Milembe alijaribu kupaza sauti ya kuomba msaada, lakini pigo la pili lililopiga shingoni mwake lilikatiza yowe kabla hazijafika mbali.

Pigo hilo lililokuwa na nguvu zaidi, lilimuondoa uhai wake kwa haraka sana.

Mkono wake wa kulia ukakatwa, ukining'inia pembeni kama ishara ya mwisho ya upinzani wake wa kiutu, mwili ukapoteza nguvu.

Milembe hakuweza tena kupumua. Kilichobaki kilikuwa mwili uliojeruhiwa vibaya, ukiteleza chini kwenye sakafu ya nyumba isiyomalizika.

Mara baada ya kumuua, Genja na wenzake walitoweka haraka, wakijua wameacha alama kubwa ya kifo nyuma yao. Hakukuwa na kurudi nyuma.

Walikuwa wamepanga kila kitu kwa ustadi—kutoweka kwa simu za Milembe, kutupa ushahidi kwenye choo cha shimo, na kuficha kila ushahidi wa mauaji hayo.

Lakini, walisahau kama waliacha chupa ya Fanta kando ya mwili wa Milembe. Walifanya kosa kubwa la kiufundi.

Itaendele...

Ova
 
😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Sehemu ya Sita

Asubuhi ya Machafuko

Alfajiri ya tarehe 26 Aprili 2023, habari za kushtusha zilisambaa kwa kasi kama moto kwenye nyasi kavu.

Mwenyekiti wa mtaa, Noel Ndasa, alipokea simu ya dharura. "Kuna mauaji yametokea hapa karibu!" aliambiwa. Aliamua kwenda kuona mwenyewe.

Aliingia kwenye nyumba hiyo isiyoisha, ambapo mwili wa Milembe ulikuwa umelala uso chini, damu ikiwa imejaa chini yake.

Ndasa alihisi mwili wake ukitetemeka, macho yake yakishindwa kuamini kile alichokiona.

Mikono ya Milembe ilikuwa imekatwa, na alama za upanga zilikuwa karibu kila sehemu ya mwili wake.

Kichwa, shingo, na mikono— vyote vilikuwa ni ushahidi wa panga zito lililotumika.

Polisi waliwasili. Walifanya upekuzi, wakichunguza kila kipande cha ushahidi, na kugundua chupa ya Fanta ikiwa na kioevu cheupe ndani yake, ikitoa dalili kuwa mauaji haya yalikuwa yamepangwa kwa ustadi mkubwa.

Mara moja, polisi waligundua chupa ya Fanta ilikuwa ni mwanzo mzuri sana wa upelelezi wao, mkoko ulianza kualika maua.

Itaendelea...

Ova
 
Ndo maana tukio lolote mtu hautakiwi kukurupuka kuliongelea bila investigation,watu uwa wanakurupuka sana kuzungumzia matukio bila investigation ata lile tukio la Tanga Bara Bara ya 4,la mama mwenye nyumba na house gal wake kuuwawa watu walikurupuka kuwa mume ndo kawauwa ila baada ya siku kadhaa wakashangaa kuukuta mwili WA jamaa kauwawa .
Inasikitisha sana,jamaa kauliwa,na bado kasingiziwa yeye ndiye alieua,amekufa kifo kibaya cha masikitiko ma nyanyaso.Wapumzike kwa amani,yeye,mke wake,na dada wa kazi,hawa watu watatu yaonyesha,walikuwa wakipendana sana,wamekufa kwa siku moja,bila ajali ya gari,pikipiki,moto,sumu au yoyote ile,ni kwa kuuliwa.
 
Inasikitisha sana,jamaa kauliwa,na bado kasingiziwa yeye ndiye aliteua,amekufa kifo kibaya,masikitiko ma nyanyaso.Wapumzike kwa amani,yeye,mke wake,na dada wa kazi,hawa watu watatu yaonyesha,walikuwa wakipendana sana,wamekufa kwa siku moja,bila ajali ya fari,pikipiki,moto,sumu au youote ile,ni kwa kuuliwa.
Mauaji ya Namba hii yanaashiria kwamba kuna mkasa mzito Sana nyuma ya tukio hili. Thoroughly Crime Investigation is required here in order to uncover the story behind.
 
Back
Top Bottom