Mimea tiba kupitia mimea ya majumbani

Mimea tiba kupitia mimea ya majumbani

Kitaalamu mmea huu unaitwa Kalanchoe Marmodata Baker ,jina mama ni Kalanchoe ambapo aina zingine ni kama Kalanchoe prittwitzii Kalanchoe Pinnata Kalanchoe Densiflora Rolfe na Kalanchoe Crenata , Je kwenu unaufahamu kwa jina lipi ??

Huu mmea una maajabu yake!

■■ Kwa wanawake husaidia kusafisha mirija (kwa wenye maambukizi ya bakteria au fangasi) kwenye mirija ya uzazi na U.T.I sugu isiyotibika kwa Azuma wala sindano

■■ Hutumika pia kwa watoto wenye shida ya kupumua,

■■ Kwa wenye maumivu makali ya madonda ya tumbo hutumia kutuliza maumivu

Unachukua majani kadhaa kisha unayababua kwenye joto kisha unafikicha na kukamua, yana maji mengi, ukifikisha nusu glass ongeza maji ya kawaida (Ya Uvuguvugu) mpaka ijae kisha kunywa asubuhi na usiku pia utafanya hivyo angalau kwa siku 4 hadi 7

Maji yake hayana harufu mbaya wala hayachefui.

Siyo hivyo tu !

Kama mtoto wako mchanga alikunywa maji machafu akawa anakoroma basi hii ni dawa iinsaidia kusafisha!! Unaibabua kwenye Moto unamwekea Kila pua tone moja na mdomoni moja baada ya muda kidogo anapiga chafya uchafu unatoka hata akicheua anakuwa anatoa malenda lenda atakuwa sawa.

Kwa Miguu inayouma unyababua majani kwenye moto kishaView attachment 3225385 unachua.

Kwa wanaoumwa MASIKIO, ukibabua majani hayo kwa moto, ukaweka matone mawili au matatu kwenye sikio linaloumwa asubuhi na jioni kila siku unapona ndani ya siku 3 hadi 5
Naomba nitoe shuhuda hapa..

Nilisumbuliwa na sikio mda mrefu na dawa iliyoniponya hadi leo ni hii.
 
Kuna watu hawajui Mbilimbi, hasa ndugu zangu Wasukuma na Wakurya..huu ndio mti wa Mbilimbi na hayo ndio matunda yake..

mbilimbi ni tunda chachu sana....huwa inatumika kutengeneza chachandu...na wengine huwa wanaweka Mbilimbi mbichi kwenye maji ya kunywa ili kuongeza ladha

Sasa kama Kuna mtu unamfahamu anasumbuliwa na Maumivu ya mgongo, magoti au kiuno na anateseka saana huyu ana machaguo mawili ya kutibu UGONJWA wake

CHAGUO LA KWANZA

Chuma majani ya Huo mti WA mbilimbi osha vzr Kisha yachemshe Kwa mda WA dakika 5 hadi 10 baada ya hapo unaweza kunywa glass Moja asubuhi nyingine mchana na yatatu usiku Kwa mda WA siku 14 hapo utakua umetibu tatizo Hilo Maumivu ya joint za mifupa UGONJWA huu kitaalam huitwa Arthritis

CHAGUO LA PILI

La hasha una kipato kzr basi nenda duka la dawa tafuta dawa inaitwa Meloxicam caps au Ibuprofen tabs itakusaidia kukupa nafuu Kwa mda au yakaisha kabisa pia

Ukishapona kabisa njoo inbox unishuru nawafumbua macho na akili mzijue Siri zilizofuchika kwenye mimea na tiba za kisayansi
1738849986988.jpg
 
DAWA TIBA ASILI

DAWA YA MENO

Naam wanandugu Leo tupate faida ya mchanganyiko huu 👇

1-KARAFUU
2-MANJANO
3-NDIMU
4-CHuMVI
5-MAFUTA YA ZAITUNI

Huu mchanganyiko unatatua changamoto zote za meno

✔Unaondoa maozo ya meono (kuoza kwa meno)
✔Unaondoa rangi ya njano,weusi au ukungu kwenye meno
✔Unaondoa ganzi ya meno
✔Unaondoa maumivu ya meno
✔Unaimalisha meno na kung'alisha nk

MATAYALISHO
-Karafuu ya unga vijiko 3
-Manjano ya unga vijiko 3
-Chumv kidogo
-matone machache.ya mafuta ya zaituni
-Kamulia ndimu kidogo

Baada ya hapo changanya kwa pamoja ichanganyike vizur

MATUMIZI
👉Tumia huu mchanganyiko kuswakia yani kupigia mswaki (kubrash meno) sungua meno yako aswaaa

Hii inatumika x1 au x2 kwa Sikh

Unaweza kutumia kwa kufululiza kila siku au unaweza kutumia x1 au x2 kwa wiki

Haina dozi tumia mpaka tatizo lako litakapo malizika

Mukawe na afya njema

Mw/amungu ndiye mjuzi zaidi

Kwenye maombi yako kwa muumba na Mimi usisahau kuniombea 🙏🙏🙏🙏

Masagala BRAZA CHOGO
 
Shida ya dawa hizi wakati mwingine zinapelekea kumaliza Figo.Ingependeza pakawa na kipimo kinachooleweka vinginevyo tunaenda kuanzisha tatizo lingine kwa mtu atakayetumia
Na kama una utaalam nazo tafuta mwenye ujuzi nazo akusimamie
 
Back
Top Bottom