nyakubonga
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 5,960
- 9,978
Naomba nitoe shuhuda hapa..Kitaalamu mmea huu unaitwa Kalanchoe Marmodata Baker ,jina mama ni Kalanchoe ambapo aina zingine ni kama Kalanchoe prittwitzii Kalanchoe Pinnata Kalanchoe Densiflora Rolfe na Kalanchoe Crenata , Je kwenu unaufahamu kwa jina lipi ??
Huu mmea una maajabu yake!
■■ Kwa wanawake husaidia kusafisha mirija (kwa wenye maambukizi ya bakteria au fangasi) kwenye mirija ya uzazi na U.T.I sugu isiyotibika kwa Azuma wala sindano
■■ Hutumika pia kwa watoto wenye shida ya kupumua,
■■ Kwa wenye maumivu makali ya madonda ya tumbo hutumia kutuliza maumivu
Unachukua majani kadhaa kisha unayababua kwenye joto kisha unafikicha na kukamua, yana maji mengi, ukifikisha nusu glass ongeza maji ya kawaida (Ya Uvuguvugu) mpaka ijae kisha kunywa asubuhi na usiku pia utafanya hivyo angalau kwa siku 4 hadi 7
Maji yake hayana harufu mbaya wala hayachefui.
Siyo hivyo tu !
Kama mtoto wako mchanga alikunywa maji machafu akawa anakoroma basi hii ni dawa iinsaidia kusafisha!! Unaibabua kwenye Moto unamwekea Kila pua tone moja na mdomoni moja baada ya muda kidogo anapiga chafya uchafu unatoka hata akicheua anakuwa anatoa malenda lenda atakuwa sawa.
Kwa Miguu inayouma unyababua majani kwenye moto kishaView attachment 3225385 unachua.
Kwa wanaoumwa MASIKIO, ukibabua majani hayo kwa moto, ukaweka matone mawili au matatu kwenye sikio linaloumwa asubuhi na jioni kila siku unapona ndani ya siku 3 hadi 5
Nilisumbuliwa na sikio mda mrefu na dawa iliyoniponya hadi leo ni hii.