Mimi baba wa watoto watatu ratiba yangu ya asubuhi na jioni

Mimi baba wa watoto watatu ratiba yangu ya asubuhi na jioni

Uko vizuri mkuu hongera sana, wewe ni baba Bora ambao mnapigwa vita sana katika jamii ya kiafrika.

Naomba chagua siku moja ya kurudi walau tatu au saa mbili usiku nyumbani, siku hii iwe maalumu kwa kupita kijiweni, kijiwe kilicho karibu na mtaani kwako wanakoshinda vijana na wazee wa hovyo. Just to keep up na mambo ya mtaani. Au kupita baa na rafiki yako mwanaume, mkaongee ya kiume. It's healthy!
Kwahio ukituona kijiweni unatuona wazee wa hovyo? Binti umenisikitisha sana.
 
Naona umeamua kumpoteza Baba bora sasa,huko kijiweni anaweza akanogewa na akabadilika,kijiweni ni majungu tu wala hakuna la maana,

Acha niendelee kukomaa na box na hili baridi.

😎
Huku kwetu maisha yanahitaji ujanja janja sana especially kama hujawekeza kiulinzi nyumbani kwako, akikaa kijiweni lisaa once a week ataelewa mengi sana yanayoendelea mtaani kwake. Unless yuko vizuri huku kwetu tunaita “kujipata”. Hata kama umejipata kuna namna unahitaji machawa kama bodaboda guys, good for ulinzi shirikishi.

Naamini kwa aina ya utambuzi alionao hawezi pitiwa na upepo wa hovyo.

Anyways, kuhusu “hilo baridi” haujaliamulia tu 😉😅
 
RATIBA YA ASUBUHI
  • Naamka saa 11 au 12 kutegemeana na shughuli za siku.
  • Nikiamka saa 11 ujue na shughuli na mama yoyo.
  • Nikiamka saa 12 cha kwanza nachukua nguo za watoto( wawili wanafunzi) na zangu na kuzinyoosha.
  • Muda huo wife anakuwa anapambana na kuwaogesha. Akimaliza kuwaogesha nampokea kuwapaka mafuta na kuwavalisha ( muda huo wife anakuwa anawapikia breakfast).
  • Baada ya hapo naenza kujiandaa mwenyewe kwa ajili ya kwenda kwenye miangaiko. Asubuhi huwa natoka nao hadi kwenye kituo ambacho huwa wanachukuliwa na school bus.
  • Wakishachukuliwa mm ndo huwa naenda kutafuta usafiri wa kwenda kwenye mihangaiko yangu.

RATIBA YA JIONI
  • Huwa najitahidi by saa 11 niwe home.
  • Nakuta watoto wamerudi muda si mrefu, so naoga then naanza fanya nao home work.
  • Wakamimaliza homework natafuta kinywaji changu pendwa na kuanza kusip nikisubr msosi wa usiku..
  • Wadau kwa ratiba yangu hii nyie mnaionaje, ratiba yako wewe ipoje?
mwanaume hana ratiba mkuu
halafu mbona unaonekana kama unajikomba kwa wife,si bure
 
Safi kabisa ni mfano mzuri wa baba bora.Mm nilikua mzee wa kuamka sijali hata wanangu wameamka poa ama vip Jioni narudi mida mibovu mara nyingi nakuta wamelala.Kuna siku niliamua kukaa nyumbani kucheza na watoto nilikuja kugundua kuna kitu sifanyi sawa kama mzazi.Nikabadili ratiba sio siri watoto wako ukiwa nao karibu ni best friend wazuri sana yaaan sio siri nainjoi sana kuwahudumia ama kukaa nao mda mwingi.
Mungu mwenyewe alimpenda Adam na matunda ya bure bustanini lakin wapi, jamaa wakamsaliti
Wife ana rafiki yake ,huwa analalamika kuwa mumewe anakaa mno nyumbani ,why hatoki kutembea tembea ,muda wote yuko hom
 
Back
Top Bottom