Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 966
- 6,019
Leo tarehe 11 Oktoba, 2024 mimi na mume wangu Advocate Gwajima na watoto wetu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, tumefika kituo cha Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu kwenye daftari la mpiga kura wa serikali za mitaa kama maandalizi kuelekea kupiga kura ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba, 2024 nchini kote.
Hatua hii ni kufuatia uzinduzi rasmi kitaifa wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa uliofanywa tarehe 11 Oktoba , 2024 huko Chamwino, Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.
PONGEZI kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo Ndugu Robert Ally Massawe kwa maandalizi mazuri ya utaratibu wa kujiandikisha na wepesi na umahiri wa maafisa waandikishaji kwenye kutoa huduma husika.
Mimi na familia yangu tunawahamasisha watanzania wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye serikali za mitaa yao zoezi litakalofanyika kuanzia tarehe 11-20 Oktoba, 2024.
Viongozi wenye sifa za kutumikia jamii ni matokeo ya kura yako mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura hivyo, jitokeze jiandikishe. Mimi na familia yangu, tayari tumetimiza wajibu wetu.
Tunawatakia uandikishaji na uboreshaji mwema wa taarifa zenu kwenye daftari husika.
MWISHO.