LGE2024 Mimi na familia yangu tumeshajiandikisha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Leo tarehe 11 Oktoba, 2024 mimi na mume wangu Advocate Gwajima na watoto wetu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, tumefika kituo cha Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu kwenye daftari la mpiga kura wa serikali za mitaa kama maandalizi kuelekea kupiga kura ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba, 2024 nchini kote.

Hatua hii ni kufuatia uzinduzi rasmi kitaifa wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa uliofanywa tarehe 11 Oktoba , 2024 huko Chamwino, Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

PONGEZI kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo Ndugu Robert Ally Massawe kwa maandalizi mazuri ya utaratibu wa kujiandikisha na wepesi na umahiri wa maafisa waandikishaji kwenye kutoa huduma husika.

Mimi na familia yangu tunawahamasisha watanzania wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye serikali za mitaa yao zoezi litakalofanyika kuanzia tarehe 11-20 Oktoba, 2024.

Viongozi wenye sifa za kutumikia jamii ni matokeo ya kura yako mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura hivyo, jitokeze jiandikishe. Mimi na familia yangu, tayari tumetimiza wajibu wetu.

Tunawatakia uandikishaji na uboreshaji mwema wa taarifa zenu kwenye daftari husika.

MWISHO .
Mimi na family yangu tunajiandikisha ili kupata vitambulisho tuuu,Mambo ya uchaguzi,daaa
 
Hongereni ila washauri viongozi wenzako wenye dhamana ya kusimamia uchaguzi watende haki ,nchi inatumia fedha nyingi sana kwenye uchaguzi kuanzia uandikishaji hadi upigaji kura ,matendo ya kuiba kura au kuaanda kura za maruhani mapema ni bora kusifanyike uchaguzi muwe mnajichagua wenyewe ili hizo fedha ziende kutumika kwenye huduma za jamii.
Unafikiri huu uchaguz utakuwa na haki 😄

Ova
 
Leo tarehe 11 Oktoba, 2024 mimi na mume wangu Advocate Gwajima na watoto wetu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, tumefika kituo cha Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu kwenye daftari la mpiga kura wa serikali za mitaa kama maandalizi kuelekea kupiga kura ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba, 2024 nchini kote.

Hatua hii ni kufuatia uzinduzi rasmi kitaifa wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa uliofanywa tarehe 11 Oktoba , 2024 huko Chamwino, Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

PONGEZI kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo Ndugu Robert Ally Massawe kwa maandalizi mazuri ya utaratibu wa kujiandikisha na wepesi na umahiri wa maafisa waandikishaji kwenye kutoa huduma husika.

Mimi na familia yangu tunawahamasisha watanzania wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye serikali za mitaa yao zoezi litakalofanyika kuanzia tarehe 11-20 Oktoba, 2024.

Viongozi wenye sifa za kutumikia jamii ni matokeo ya kura yako mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura hivyo, jitokeze jiandikishe. Mimi na familia yangu, tayari tumetimiza wajibu wetu.

Tunawatakia uandikishaji na uboreshaji mwema wa taarifa zenu kwenye daftari husika.

MWISHO.

View attachment 3121584View attachment 3121585View attachment 3121586View attachment 3121587View attachment 3121588View attachment 3121589
View attachment 3121590
Nimekuwa nikiunga mkono Hoja zako nyingi sana ambazo umekuwa ukizileta hapa jukwaani ambazo kwa hakika huwa zinagusa Moja kwa Moja maslahi mapana zaidi ya umma. Lakini kwa Hoja yako hii ya leo nasikitika Sana kukujulisha ya kwamba kamwe sitaiunga mkono.
Kwa mtu mwenye akili timamu sawa sawa kabisa, LAZIMA atakubaliana na Ukweli kwamba sanduku la kura kwa hapa Tanzania linafaa kupuuzwa kabisa kwa ujumla wake.
Hakuna Uchaguzi wa Siasa hapa Tanzania, hizo ni ghiriba na geresha tu ili kuwazuga Wananchi, ni maigizo ya wanasiasa wenye hila kwa nia ovu ya kuhujumu haki za raia. I can't waste my time to participate in a such idiotic event.
 
Back
Top Bottom