Leo tarehe 11 Oktoba, 2024 mimi na mume wangu Advocate Gwajima na watoto wetu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, tumefika kituo cha Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu kwenye daftari la mpiga kura wa serikali za mitaa kama maandalizi kuelekea kupiga kura ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika 27 Novemba, 2024 nchini kote.
Hatua hii ni kufuatia uzinduzi rasmi kitaifa wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wa serikali za mitaa uliofanywa tarehe 11 Oktoba , 2024 huko Chamwino, Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.
PONGEZI kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu wa Salasala, Kata ya Wazo Ndugu Robert Ally Massawe kwa maandalizi mazuri ya utaratibu wa kujiandikisha na wepesi na umahiri wa maafisa waandikishaji kwenye kutoa huduma husika.
Mimi na familia yangu tunawahamasisha watanzania wote wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye serikali za mitaa yao zoezi litakalofanyika kuanzia tarehe 11-20 Oktoba, 2024.
Viongozi wenye sifa za kutumikia jamii ni matokeo ya kura yako mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura hivyo, jitokeze jiandikishe. Mimi na familia yangu, tayari tumetimiza wajibu wetu.
Tunawatakia uandikishaji na uboreshaji mwema wa taarifa zenu kwenye daftari husika.
Hongera sana Mheshimiwa.
Binafsi sitashiriki maana huwa naona uchaguzi ni michezo kama ya mazingaombwe iliyokuwa inafanyika kipindi nipo shule ya msingi 🤣🤣.
Walio na vifua wakishiriki inatosha.
tunaomba muwe na utaratibu wa kuandikisha watu kwa kuwafuata katika maeneo yao ya kazi kama mnavofanya kwenye sensa vinginevyo % kubwa ya watu hawatojiandikisha nikiwemo mimi
Hongereni ila washauri viongozi wenzako wenye dhamana ya kusimamia uchaguzi watende haki ,nchi inatumia fedha nyingi sana kwenye uchaguzi kuanzia uandikishaji hadi upigaji kura ,matendo ya kuiba kura au kuaanda kura za maruhani mapema ni bora kusifanyike uchaguzi muwe mnajichagua wenyewe ili hizo fedha ziende kutumika kwenye huduma za jamii.