LGE2024 Mimi na familia yangu tumeshajiandikisha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Hata mimi nashauri tuandikishiwe nyumbani kama sensa
 
Hongera Dr. Gwajima , ila kungekuwa na options ya kuwafuata watu majumbani/ makazini ingependeza zaidi
 
Maendeleo ndio yanapaswa kuhamasisha watu kujiandikisha, kupiga kura na kuchagua viongozi na wala sio kampeni kama za kutokomeza surua, mabusha na matende...
 
Wewe ni kati ya mawaziri uliye karibu na Watanzania. Kila Waziri, Waziri, mkuu, Rais, Makamu wa Rais, NW, makatibu wakuu, Mkuu wa Mkoa, Wakurugenzi, wakuu wa wilaya, kata, vijiji, mitaa, watumishi wote wa umma wangekuwa kama wewe tungepiga hatua. Mtu kama wewe,Jerry Slaa, Lukuvi mtaishia kutumbuliwa na serikali hii.
 
Maendeleo ndio yanapaswa kuhamasisha watu kujiandikisha, kupiga kura na kuchagua viongozi na wala sio kampeni kama za kutokomeza surua, mabusha na matende...
Mkwe kajiandikishe.
 
Mheshimiwa, mimi hapa kijana shupavu nimefanikiwa kumuona mwanao.
Nauliza tu, je itapendeza na mimi nikiwasiliana nae ili siku moja mimi pia nikae nae kwenye dawati la kuboresha taarifa za uchaguzi kama wewe na advocate hapo..?
 
Dah! Sasa sisi wengine tukiacha kwenda kazini siku hiyo tumelala njaa, endeleeni kutuwakilisha kwanza hata sijui faida ya kupiga kura.
 
Kwa wateule wa rais lazima wajiandikishe Kwa sababu ndiyo sehemu Yao inayowapatia kula Yao na maisha Bora .Sasa Mimi ambaye siyo mteule ambaye miaka mingi nimepiga kura lakini Kuna hujuma ambazo zinaonekana wazi kabisa kuwa Kuna chama kinasaidiwa na polisi kuiba kura ili kishinde Sasa hapo Kuna faida gani ya kujiandikisha ili kupiga kura?
 
nimejiandikisha leo,ila ntapga kura ya ya mwenyekiti tu huko kwingine sina habari maana hakuna haki.
 
Je ? Umejiandikisha?
 
Tusidanganyane, nyie mmeboresha taarifa zipi zaidi ya kuandikisha jina lako na umri basi. Mimi mtaani kwangu wanaandika jina na umri tu, hakuna taarifa za ziada wanazochukua. Machawa msituchanganye wananchi tuone kuwa tulichoandikishwa si sahihi.
Ndiyo kuboresha mwenyewe huko, umefanya vema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…