LGE2024 Mimi na familia yangu tumeshajiandikisha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

LGE2024 Mimi na familia yangu tumeshajiandikisha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kazi Bure tu hapo hakuna aja ya kufanya uchaguzi
 
Yaani kwa kifupi anamaanisha.kila kitu kifanyike online, kama vile unavyo fanya miamala ukiwa uko home kwako! Sasa ila ukitaka cash [emoji389] lazima uifute kwa wakala au Bank!!
Marekani ni mkubwa kiteknolojia lakini inadaiwa uchaguzi wake ulichezeshwa.
Sisi hatutakua kwenye hiyo hatari kweli?
 
Hongera sn mama yetu hata sisi tusioipenda CCM na maovu yake lazima tukajiandikishe haraka ili tuanze kuiondoa haraka
 
Sitajiandikisha Wala kupiga kura mpaka niskie wananchi wakiri uchaguzi ulikuwa wa huru na haki! lasivyo hamnioni, na nafurahi kuona watu wengi wamesusia chaguzi kutokana na sababu hyo hyo wizi wa kura! sasa nyie endeleeni kukaza fuvu!
 
Sitajiandikisha Wala kupiga kura mpaka niskie wananchi wakiri uchaguzi ulikuwa wa huru na haki! lasivyo hamnioni, na nafurahi kuona watu wengi wamesusia chaguzi kutokana na sababu hyo hyo wizi wa kura! sasa nyie endeleeni kukaza fuvu!
Kususia inakusaidia nini? lengo la CCM ni msusie iendelee kufanya ufisadi wake, Zambia walikomaa zaidi ya miaka 6 lakini hatimaye wamepata mwanga
 
Kujiandikisha kwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa hakuna kitambulisho chochote wanatoa labda usubiri maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura linalosimamiwa na tume ya uchaguzi.
Hilo daftari la kudumu la wapiga kura Kuna namna yeyote taarifa zake zinaintergrate na huu uandikishaji unaoendelea?
 
Haki yako kikatiba sababu ni Mtanganyika mkazi wa Tanganyika. Ni Katiba inasema sio mimi..
 
Mimi nikichek huku Arusha au Mtaa ninao kaa naona kama watu wamesusia huu uchaguzi wanatubembeleza kujiandikisha
 
Wakitaka mm nijiandikishe ccm iondoke kwanza madarakani.....
Mimi nikichek tuu naona kama Wananchi wameshachoka hizi siasa hapa kuna kesi Kijana wa Chama anamwambia Mzee akajiandikishe Mzee kamtukana kijana kamkosa na Panga
 
Hilo daftari la kudumu la wapiga kura Kuna namna yeyote taarifa zake zinaintergrate na huu uandikishaji unaoendelea?
Havihusiani kabisa kwanza uchaguzi huu unasimamiwa na Tamisemi na ule wa mwakani ndiyo utasimamiwa na INEC yaani Tume ya Uchaguzi.
 
Dr Doroth nasmini umekuwa sasa umeacha kumnyanyasa mumeo .......maana kajamaa kamevumilia aseee khaaaa
Kamnyanyasa ki vp!? Alafu acha zarau za kumwita mwanaume mwenzio 'Kajamaa" wwe ndiyo unamlisha!?
 
Labda uhusiki na,wizi wa kura, lakini kama unapima upepo nadhani umeona umejionea maoni ya wana jamii/wananchi japo kwa uchache.
Wewe umeteuliwa hukugombea,lakini unaona watu walivyo na maumivu ya matendo maovu yafanywayo na ccm.
Kama wa-Tanzania wagekuwa na mamlaka ya kutoa hukumu, ccm mgeenda MOTONI wote na familia zenu. Yani ccm ni dhuluma, na ushetani. Binafsi unaweza usiwe muhusika lakini kuwa ccm tu unaonekana nawe ni muhusika wa uovu wao.
Unaheshimika wewe, lakini hili la uccm huwa linawafanya muonekane waouvu, bila sababu za msingi.
Ila nawatakia, Kila la kheri kwenye uchaguzi wenu.
 
Back
Top Bottom