Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Hiyo 50-50 unaitaka katika familia yako pekee au dunia nzima na katika kila kitu? Kama ni katika familia yako haina tatizo ila ni kama ulivyoandika kwenye title ya uzi wako, I have bad news for you, ni kila kitu kitacollapse na ulimwengu wote utashindwa kua normal.

50-50 inaweza kua achieved katika household tena inategemea na aina ya mwanaume uliye naye ila katika overall life situation ya sasa haiwezekani na haitokuja kuwezekana na sababu kuu ya kutokuwezekana ni huyo huyo mwanamke.
Mkuu kama hamtaki 50 50 basi hudumieni wake zenu 100%, na siku mkiachana gawaneni mali pasu kwa pasu, simple tu
 
Kabla ya kuletewa dini(kipindi cha mizimu) hilo la 50-50 halikuwepo na hata zilipokuja dini pia hazijaja na hilo jambo na mpaka tutaisha(kufa) wote duniani hilo jambo halitakaa liwepo ila wakuendelea kulipambania liwepo watazidi kuwepo.

Kiufupi suala la 50-50 halitakaa liwepo na hayo ndo maumbile halisi ya binadamu.
50-50, kiasilia haipo hiyo, mpaka wanawake wenyewe hufikia pahala wanaikataaga wenyewe, ndo ujue alilolifanya Mungu mwanadam hawezi kubishana nalo Wala kulitangua, badala yake ataishia kujitekenya mwenyewe na kucheka alafu yanajirudia pale pale kama Mungu alivotaka iwe. Ndo maana tunasema asili ni asili tuuu

You can't fight against the nature.
Hakuna lolote lidaiwalo hapo.Fedha inaleta mgagasiko kifikra na kuleta tamaa ya uporaji wa haki,uongozi na mgawanyo wa majukumu.
Feminist jadda
Mnakimbilia ndoa yakiwabana huko mnaanza kutushushia magazeti usiku....mabachela hizi porojo hazituhusu
Kuufuta mfumo dume ni ngumu sana mkuu.
Una ndoa? Ume practise ulichosema au nadharia... isije kua ndo yale kungwi mdomo mrefuuu kujishadadia unayajua mapenz na umefunzwa ukafunzika kumbe una talaka 4 no mume currently. Kwamba sa8 usiku likaja wazo tu la 50/50 kilichokukuta sitak ku imagine, pole [emoji26]
Hongera sana mkuu bandiko lako ni tamu sana maana linatupeleka kule kwetu NDOA NI UTAPELI, KATAA NDOA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfumo dume ni mfumo wa kimbingu, 59/50=1 ni mfumo wa kishetani, humo ndo kuna ushoga, usagaji na mambo mengine ya kishenzi. Sababu unajaribu kuondoa utofauti kati ya mwanaume na mwanamke. Wote wakiwa sawa kila mtu anaweza kuwa mwanamke at the sametime akawa mwanaume
Kama lengo ni kuangalia wapi kosa limefanyika basi wakufanya hivyo ni sisi wanaume

Wanaume ndio tulifanya kosa kuwapeni uhuru uliopitiliza (tukiamini kufanya hivyo ni upendo) mpaka sasa uhuru huo unaenda kuwa silaha inayoturudia wenyewe.
Sasahivi mnagombea 50 zenu na mashoga
Ndio maana LGBTQ inakua kwa kasi kubwa.....
50/50 maana yake fursa sawa kwa jinsia ya ke na me kielimu , nakadhalika haina maana nyingine sema watu hawaelewagi wanachukua maneno ya vijiweni kuwa mwanamke kuwa sawa na mwanaume kitu ambacho sio kweli.
Umeandika gazeti kabisa alafu ni pumba tupu kuanzia mwanzo hadi mwisho
kuparuana kote kule kwenye comment za watu kumbe shida yako ni 50/50
Hahahahahaha..mnavyopenda kitonga hamuwezi hii kitu
50×50 kwa hamsini ni kampeni ya kishetani, ni upuuzi unaolenga kuua familia. Wanawake hawataolewa na kuishi na waume zao maana watakuwa hawana heshima, adabu na utii kwa waume zao. Wanawake watakuwa wanazalishwa hovyo kama wanyama na kuachwa walee watoto peke yao. Itakuwa ni mtindo mpya wa maisha na umeanza kushika kasi, single mothers wanaongezeka na wanazaa watoto wasioeleweka baba zao. Watoto wa kiume wanalelewa kikikekike na madhara yake yanaonekana
Wameangamia/ameangamia mwenye kumfanya mwanamk kuwa kiongozi/kuwa kichwa kwenye banda lanaume
Mungu alianza kumuumba Adam, akaona yupo mpweke, kutoka ktk nyama na mifupa ya Adam akamtwaa mwanamke Eva ili awe msaidizi wa mume wake pia ili Adam asiwe mpweke,

Kama uliumbwa ili uwe msaidizi wa Adam kwanini unataka Adam akufanyie Kila kitu wewe kazi yako itakuwa nini na utakua umeumbwa na Mungu ili iweje sasa
Wazungu wenyewe baada ya kuimplement 50-50,talaka zimeiongezeka na kwa mujibu wa CNN US ndoa zimepungua kwa asilimia zaidi ya hamsini.Manake huo mfumo hauwezekani kuongoza familia na siku hizi huko mbele sababu ya ujuaji wenu, wanawake wajuaji kama nyinyi wanaume wanaume wanapiga na kutambaa.

US huko wanaandaa mpaka single events, special tu kuwakutanisha wanawake wapate waume,ila wanao jitokeza ni wanaume wachache. Kuna single event moja US,walijitokeza wanawake 147 na wanaume watatu tu mpaka muandaaji akawa analalamika na wengi walio jitokeza type zile zile zinazo jifanya wajuaji na wasomi wasiokuwa na maadili. Msijidanganye kwamba mnaogopwa hamna mwanaume anaogopa kumtongoza mwanamke yoyote, ila akigundua ni mjiuaji unapenda mashindano plus 50 -50 kibuti kikuhusu.

Hata humu wengu wenu, mkitongozwa mkitolewa dinner siku ya kwanza tu kwenye bili hatuwasikii mkisema tutoe nusu kwa nusu au kama yupo aliye lipa nusu ya bili baada ya kutolewa out siku ya kwanza anyooshe kidole.

Mfumo dume ndio msingi na ni nguvu iliyo iongoza dunia tokea kuumbwa kwake.
Mkimaliza hili, mtaanza kuomba kuoana wenyewe kwa wenyewe.

Hamna akili hata kidogo, ni ujinga wenu tuu.
Umeandika Kama singo maza mmoja hivi!
Huo mjadala tulishaufunga

Hakuna mwanaume atakubali hilo
Afu hii 50-50 ndo imezalisha ushoga, inachochea ushoga na usagaji, mtakuja mseme mwanamke nae anahaki ya kuoa na mwanaume ana haki ya kuolewa Kwa kisa Cha 50-50, ndo unakuta mwanamke anaanza kuwasaga wanawake wenzake Kwa kujifanya kidume na mwanaume kufirwa Kwa kujifanya mwanamke Kwa kisingizio Cha 50-50 kuwa hakuna tofauti kati ya me na ke kwamba eti majukumu ya wote yawe sawa kisa mwanamke analiwa na mwanaume aliwe, na kisa mwanaume anakula na mwanamke awasage wenzake Kwa kujifanyisha kidume

Hii 50-50 ni ajenda za kupitisha ushetani
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
 
Umemaliza kila kitu Jadda, tatizo wanaume wa Kitanzania hawaitaki hiyo kisa tu wanataka mtu wa kuwatii,

Uislam umeshaweka wazi majukumu ya Mwanamke nayo ni Kuzaa tu, kazi zote za nyumbani ni za Mwanaume kama hawezi aweke msaidizi, Uislam unamtaka Mwanaume amlipe mkewe ili amnyonyeshee watoto (haya hua hawayasemi kwenye mawaidha, wanabana kimyaaa)
Yeah niliwahi kuambiwa hili kwamba kwa waislam jukumu la mwanamke ni kuzaa na kupamba nyumba, kazi za nyumbani mume anatakiwa aweke msaidizi, ila hili hutasikia wakilisema wao wanajua kutetea habari za kuoa wake wanne tu
 
Hiyo 50/50 unayotaka Mjukuu mtaweza majukumu yake?

Kwamba Mume atoe Kodi ya miezi 6 ya nyumba na Mke alipie miezi 6 iliyobaki ya Kodi.

Wanawake wenyewe ndiyo hawa ambao wanasema mshahara wao ni wao pekee ila wa Mshahara wa Mume ndiyo wa kutumika ndani ya nyumba?

Nina rafiki yangu ni Mzungu, wao ndiyo wanaiishi hiyo 50/50 ambapo wamegawana majukumu sawa sawa na Mume wake.

Ana watoto 2 na Mume wake, mtoto mmoja ana msomesha na kumgharamia yeye matibabu/mavazi na Kila kitu kuanzia alipozaliwa hadi Chuo Kikuu na mtoto mwingine ana gharamiwa yote hayo na Mume wake.

Nieleze kama Kuna Mwanamke Bongo hii ataweza kuyafanya hayo.

Ubunge wenyewe mnapewa bure bure na Chama
Haha babu kwani mnaishi sayari gani mbona huku nje kuna wanawake wengi wameachiwa majukumu yote ya kina baba huku wanaume wameamua kuwa wazinzi na walevi tu, ukiuliza utasikia tatizo huyu mwanamke mjeuri sana anataka kunipanda kichwani acha afanye kila kitu mwenyewe, ukweli ni kwamba nyumba nyingi siku hizi wanawake ndio wanasimamia show nzima ila wengi wameamua kukaa kimya tu sababu hata wakisema wataambiwa chanzo ni wao wenyewe kwa kuwa na viburi na kuwapanda waume zao vichwani
 
Achana na haya mafurushi, hata hayajui nini yanataka.
Ila wanaume halisi wanajua na walaa hawalalamiki.
Yani tuna kizazi cha ajabu sana, mtu anataka mamlaka ila majukumu hayataki ukimuuliza anaanza kutafutiza majukumu ambayo hayapo au yale ambayo siyo ya kila siku, eti mbona ikitokea vita hamuendi au mbona wezi wakivamia hampambani nao sasa unajiuliza hiyo nyumba gani ambayo wezi wanavamia kila siku
 
Mtoa mada upo sahihi kabisa hii 50/ 50 ikienda kama inavyotakiwa hakika mambo yatakua mazuri sna , itapungaza vifo vya wanaume wengi wanaojifanya kichwa cha familia kupambania mke na watoto peke yake , mwisho wa siku anarisk maisha yake kwenye kazi hatarishi bila usaidizi kwa mwenza wake .

50/ 50 kwa apa duniani bado haifanyi kazi kama inavyotakiwa kuna namna inategemea upande mmoja , na hii ya kuegemea upande mmoja ipo makusudi kabisa kwa nia ya kumlinda mwanamke na madhara ya mfumo wa haki sawa .

Mfumo dume ni mfumo ulio tumika kumlinda mwanamke na kumpa heshima yake kama mama wa dunia, ukitoa mapungufu yake kama kumnyima mtoto wa kike haki ya kusoma , na haki ya kuchagua mwenza wake , hakuna shida nyingne kabisa ,labda tu mwanaume awe mjinga na asie tumia akili.
 
Mkuu siyo kweli kwamba wanaume wote wanaowaambia wake zao watafute pesa basi sababu ni kwamba mwanamke anahitaji zaidi kuliko kilichopo, wanaume wengine ni kwamba hawataki kabisa kuhudumia wake zao hata kwa zile basic needs tu yani inshort hawataki mwanamke anayekaa ndani kusubiri kuletewa lakini hapo hapo wanataka mke atimize majukumu ya nyumbani na bado ampe heshima na utii, na ukiona mwanamke anataka zaidi ya kile kilichopo basi ujue huyo anakijua kipato cha mumewe na anajua kabisa kuwa kuna pesa mumewe anabania na mara nyingi wanaume huwa wanahonga michepuko au wanafanyia mambo mengine yasiyo ya msingi
Mkuu kwani michepuko si wanawake pia, hauoni bado tunazidi kusambaza upendo kwa wanawake tu?
 
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
Usitupangie chakufanya Kila mmoja anaishi kulingana na utashi wake, vipi wewe 🤔🤔
 
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
Mi nadhani hao wanaosema hawataki wanawake magoli kipa kuna nukta muhimu unakuwa unaisahau.

Sidhani kama wanaosema hivyo humaanisha mwanamke aka hustle mwenyewe bila assist ya mumewe.

Wengi wanaosema hivyo utakuta wanawapa mitaji wake zao wajishuhulishe kwenye biashara ndogondogo zitazoweza kumfanya aweze kutatua ishu ndogondogo za pale nyumbani bila kuomba hela kwa mumewe.

Ila modern women wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya. Wengi wakipata hiyo nafasi huitumia kujiimarisha wao kiuchumi bila mume kujua na mwisho wa siku wakiona wamefikia malengo yao wanaanza kudai talaka.
 
Haha babu kwani mnaishi sayari gani mbona huku nje kuna wanawake wengi wameachiwa majukumu yote ya kina baba huku wanaume wameamua kuwa wazinzi na walevi tu, ukiuliza utasikia tatizo huyu mwanamke mjeuri sana anataka kunipanda kichwani acha afanye kila kitu mwenyewe, ukweli ni kwamba nyumba nyingi siku hizi wanawake ndio wanasimamia show nzima ila wengi wameamua kukaa kimya tu sababu hata wakisema wataambiwa chanzo ni wao wenyewe kwa kuwa na viburi na kuwapanda waume zao vichwani
Hao ni non responsible father's ambao hawakuwa tayari kuwa Wazazi

Ukiitwa Baba ni lazima ujue kusimama na kuendesha familia yako, sio kumuachia Mwanamke.

Sisi wengine tuko radhi tusivae ila familia ivae

Tuko radhi kutokulala Usingizi ili familia zipate mahitaji muhimu

Na huo ndiyo uanamme tuliofundishwa tukiwa jandoni miaka ile ya giza.

Kuhitimisha hoja yako ni kuwa, hao Wanawake wa kukubali majukumu ya 50/50 Tanzania bado hawapo.
 
Jadda my girl, mi nadhani tatizo halipo kwa wanaume tu, Hata kwa wanawake. Jamii yetu inatatizo la kuvamia mambo ambayo hatuyaelewi vizuri. Wanaume baadhi wanakwepa majukumu wakati huo wanataka mamlaka 100% na wakati huo huo wanawake, baadhi wanakwepa majukumu yao ya kike halafu wanataka huduma 100. Jamii kama hii lazima iwe na mvutano, ndio huu mtifuano tunao ushuhudia sasa.

Jamii imebadilika sana, 50/50 haikwepeki, Binafsi naiona iko very practical. Ni mfumo rahisi sana kuuadapt kuliko ule mfumo kale.

Swali ni je, Kwa sisi ambao wanaume zetu wametuzidi vipato mara 70, hii 50/50 tunawezaje kuipractice? Tukumbuke kwa hapa Tz, mara nyingi mwanaume mwenye kipato kikubwa ni mtu busy sana, 80% unavailable kwa mambo ya nyumbani/familia. (Someone can share her/his experience)

However , its important each family to customize their life style which accommodates them, To each their own. 🥂
 
Jadda umeandika andiko refu lakini hali reference au citations ili kutetea hoja zako...

Mahusiano ya kindoa kati ya mtu mwanaume na mtu mwanamke sio partnership au mahusiano yaliyojengwa kwa mlinganyo wa kiasilimia...

Mahusiano ya kindoa kati yetu wanaume na wanawake, yamejengwa kwenye mtazamo wa utofauti wa kiutaratibu na kiutawala/nafasi...

Reference #1 Kiutawala au Nafasi
Mwanzo 2
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Mwanzo 2
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

Mwanamke ni msaidizi wa mwanamume ambaye aliumbwa kwa kufananishwa naye ili aweze kupokea majukumu toka kwa mwanamume...Mungu angeweza hata kuamua wanyama ndio wawe wasaidizi wa mwanaume, lakini hao viumbe wengine hawakuwa wamefanana na mwanaume.

Hivyo basi, mathalani wewe unapokuwa kazini na una bosi wako, je bosi wako hawezi kukukasimisha baadhi ya majukumu yake kwa nia ya kutoa usaidizi kwake kwa kutambua kuwa wewe pekee ndiye mwenye ujuzi wa majukumu ayafanyayo?

Inakuaje nongwa kwa mwanaume ambaye kapewa msaidizi wa asili, na asimjukumishe baadhi ya majukumu?


Reference #2 Kiutaratibu

Sasa utaratibu uliobainishwa kuelezea namna viumbe hawa wawili watavyoishi umeelezwa kama ifuatavyo.
#1
Mwanzo 2
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
#2
Waefeso 5
22 Enyi wake, watiini waume zenu (nimeukatisha kutoa maudhui ya kiimani)
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe (nimeukatisha kutoa maudhui ya kiimani)

Waefeso 5
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
Mkuu nimekuelewa vizuri sana lakini kwenye suala la ndoa hiyo delegation inayofanywa na mwanaume kwa mkewe lazima iwe na uhalisia na lazima izingatie uwezo na muda wa huyo anayepewa hayo majukumu, huwezi kumtwika msaidizi wako majukumu mengi kuzidi uwezo na muda alionao kwa sababu haiwezekani mwanamke atoke kuenda kutafuta pesa na bado afanye majukumu ya nyumbani kikamilifu, na hata hivyo kiongozi anatakiwa kudelegate majukumu kwa msaidizi pale tu anapoona majukumu aliyonayo yanamzidia sasa kama mwanamke anafanya majukumu yote ya kwake na ya mume wake je mume atakuwa anafanya majukumu gani
 
Jadda my girl, mi nadhani tatizo halipo kwa wanaume tu, Hata kwa wanawake. Jamii yetu inatatizo la kuvamia mambo ambayo hatuyaelewi vizuri. Wanaume baadhi wanakwepa majukumu wakati huo wanataka mamlaka 100% na wakati huo huo wanawake, baadhi wanakwepa majukumu yao ya kike halafu wanataka huduma 100. Jamii kama hii lazima iwe na mvutano, ndio huu mtifuano tunao ushuhudia sasa.

Jamii imebadilika sana, 50/50 haikwepeki, Binafsi naiona iko very practical. Ni mfumo rahisi sana kuuadapt kuliko ule mfumo kale.

Swali ni je, Kwa sisi ambao wanaume zetu wametuzidi vipato mara 70, hii 50/50 tunawezaje kuipractice? Tukumbuke kwa hapa Tz, mara nyingi mwanaume mwenye kipato kikubwa ni mtu busy sana, 80% unavailable kwa mambo ya nyumbani/familia. (Someone can share her/his experience)

However , its important each family to customize their life style which accommodates them, To each their own. [emoji1635]
Upo smart sana , mumeo tukimwona kwenye chama la kataa ndoa ,tunamtimua na mapanga.
 
Kazi za nyumbani ndio kigezo kikubwa cha kutaka 50/50?

Nikatika tu kufikiria wapi kuna huo ugumu kwenye hizo kazi za nyumbani. (Maana hata kabla hajakuoa naye hizo kazi alikuwa akifanya)

So labda uniambie

Inawezekana home kila siku lazima ujaze Simtank la lita 10,000 za maji, maji ambayo unayafuata kilomita 30 kwa mguu tena ukiwa peku kwenye njia yenye miba, majabali na miamba kiasi kazi hizo zionekane ngumu kwako?

Au kwenye kupiga deki huwa unapiga deki stadium kama ya Mkapa?
Ndio kazi za nyumbani pamoja na kutaka mume amtawale mke ndio kigezo cha kudai 50/50, sasa kama kazi za nyumbani mnaziona rahisi kwanini ninyi hamtaki kuzifanya tena hakuna kazi wanaume hamzipendi kama kuosha vyombo na kufanya usafi, ila mnataka wanawake wazifanye na mnataka wao wazione rahisi
 
Kabisa.
Hata nchi za Ulaya na Amerika ambapo ndugu zetu hawa wanatolea mifano 50-50 wanatumia katika baadhi ya majukumu tu kwenye kulipa bill, kazi za nyumbani n.k...

Lakini ikitokea vita 50-50 haipo, wanaume ndio wapo front kumaliza, wanawake wapo lakini sio kama wanaume.
Wakati vita ya Ukraine inaanza nilisikia raisi wa Ukraine akitoa tamko kuwa wanawake na wazee wote wasafirishwe kupisha vita.

Mimi nikahoji kwanini wale wanaharakati wa haki za wanawake wakae kimya huku haki ya mwanamke ya kuoigana vita ikidhulumiwa?

Kwanini wasijitokeze na sera yao ya 50/50 kwa msukumo uleule ambao tumekuwa tukiwaona kwenye mambo ya mgawanyo wa mali nk?

Na wanawake wenyewe kwanini walikuwa kimya kuona haki zao zinadhulumiwa?

Hata humu JF sikuona feminist yeyote akilaani kile kitendo.

Sasa kama hapo nini maana ya 50/50 kama kwenye mambo magumu wanawake wanawekwa nyuma?
Hapa tunaongelea majukumu ya kila siku ya kwenye maisha ya mwanadamu hatuongelei vita au other man made disasters hayo siyo majukumu ya kila siku, ninyi ndio wale mnatolea mifano eti mwizi akivamia nyumbani mke hatoki kupambana kwani wezi kuvamia nyumbani ni suala linalotokea kila siku kwenye kila nyumba, wanaoanzisha hizo vita ni wanaume badala ya watu kukemea hizo vita mnakomaa eti na wanawake nao wawe ni sehemu ya vita na kuweka hilo kama sehemu ya majukumu
 
Back
Top Bottom