Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Actually: With great responsibility comes great authority (powers)

Kiotomati yule anayewajibika kwa watu wengi zaidi, au kwa jukumu kubwa zaidi popote ndiye anayekuwa na uwezo mkubwa.

Ilikuwa na bado ni kweli kabisa ilipoandikwa:

"Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;"

Na sasa uliyoyaongea kwenye zote hasa ya mwisho ni bonge la logic. Ni kama simu tu, kila mmoja achague profile anayoipenda na anayoendana nayo na aishi nayo kikamilifu. Sio mtu achague silent halafu atake akipigiwa iite kwa mziki wa reggae aliouchagua whata aa......

"bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; " so yule anayefanya kazi kubwa zaidi kuijenga hiyo familia na awe kiongozi. Na kama wote wanafanya kazi sawa basi wawe partners
Shukrani sana kwa kunielewa mkuu
 
Ndio, kuna msemo unasema "with great authority comes great responsibility" yani kila mamlaka makubwa huambatana na majukumu makubwa, lakini jambo la kushangaza ni kwamba wanaume wengi hasa wa kiafrika wanayataka hayo mamlaka tu ila majukumu hawayataki

Mimi naona ifike pahala dunia iachane rasmi na mfumo dume na haki sawa ishike hatamu, kwa sababu wanaume hawataki tena majukumu hivyo hata hayo mamlaka hayawafai, wanaume wengi hawataki haki sawa ila wanataka majukumu sawa tena ikibidi mwanamke ndio afanye zaidi ya mwanaume

MImi naona kusiwe tena na mgawanyo wa majukumu yani hata kazi za nyumbani zifanywe na wote kama ambavyo kutafuta pesa limekuwa ni jukumu la wote, majukumu ya mwanamke yabaki yale ya asili na ya kimaumbile tu ambayo ni kubeba ujauzito, kuzaa na kunyonyesha, hayo tu ndio ambayo mwanaume hawezi kuyafanya ila majukumu mengine yote ya nyumbani kama kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumba, kulea watoto tangu wakiwa wachanga mfano kuwasafisha, kuwauguza wakiumwa, nk yafanywe na wote kwa usawa kabisa

Na vile vile kwa mfano mume akiweka laki mezani na mke naye aweke laki mezani mahitaji yote ya nyumbani wanunue kwa usawa bills zote walipe kwa usawa, na watoto wao wawahudumie kwa usawa ikiwemo kuwalipia ada na mahitaji yao mengine yote kwa usawa, hiyo ndio maana halisi ya 50 50 siyo mmoja anamtegea mwenzie eti mtu anataka pesa mtafute wote na bills mlipe wote, ila kazi za nyumbani na kulea watoto afanye mmoja na bado huyo mmoja amtii mwenzie na amlee kama anavyowalea watoto wake, what kind of cockamamie logic is this

Na jambo jingine naona pia tuachane na suala la mwanaume kumtawala mwanamke kila mtu ajitawale mwenyewe kusiwe na habari za kichwa cha familia, yani hakuna tena kusema kwamba mwanamke anatakiwa amtii mumewe kila mtu awe na maamuzi juu ya maisha yake mwenyewe, kusiwe na wa kumuongoza mwenzake na pia kusiwe na habari za kuoa wala kuolewa tena bali iwe ni kuoana

Mnawalaumu wanawake kuwa wanadai haki sawa halafu hawataki majukumu lakini mnasahau kwamba sababu ya wao kukataa hayo majukumu ni kwa sababu mnataka wafanye yale ya kwenu tu, ila ya kwao bado mmewaachia wenyewe hamtaki kuyafanya yani huwezi kumuambia mwanamke ajitafutie pesa zake na akusaidie majukumu, halafu hapo hapo bado unataka huyo mwanamke akufanyie majukumu ya nyumbani na bado akupe heshima na utii

Kwanza hapo huyo mke anakuwa siyo msaidizi tena bali ni kama business partner tu hivyo ondoa kichwani suala la kumlazimisha akutii, hivi mnadhani mwanamke aliambiwa amtii mwanaume kwa misingi gani kama siyo kuhudumiwa maana huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayefurahia kutawaliwa na binadamu mwenzie asiyewajibika kwa lolote juu yake na kiuhalisia ukitoa huduma zinazohusisha pesa hakuna wajibu mwingine mwanaume alionao juu ya mwanamke

Kama ikiwa mtoto anamtii mzazi wake kwa sababu amemzaa na amemlea, watu wa dini wanaitii miungu yao kwa sababu wanaamini imewaumba na inawapa uhai, je mwanamke anapaswa amtii mumewe kwa sababu gani, tena hata mtoto mwenyewe akishatoka kwao akaanza kujitegemea kinachobaki kwa mzazi wake ni ile heshima tu kuwa amemzaa, lakini huyo mzazi anakuwa hana mamlaka tena ya kumpangia mtoto maisha yake mfano afanye kazi gani au arudi nyumbani muda gani kwa sababu hamhudumii tena

Sasa inashangaza pale mwanaume anapotaka mkewe atafute pesa wasaidiane maisha kwa kisingizio kwamba mke naye ana mikono miwili na miguu miwili, ila huyo huyo mwanaume haoni ajabu kumtawala huyo mke mwenye mikono miwili na miguu miwili kama yeye, yani imefikia hatua wanaume wanaona uchungu kugawana mali na wake zao na wengine ndio kabisa hawataki kuoa kwa kisingizio kwamba eti wakishafanikiwa wake zao watadai talaka ili wagawane mali

Yani hawaconsider tena yale majukumu yote ambayo wake zao wanawafanyia pamoja na utii ambao wake zao wanawapa, siku hizi wanadai kwamba kila mtu ajitafutie pesa zake na ikitokea wameachana kila mtu aondoke na chake, lakini cha kushangaza kwenye majukumu mengine hawasemi kila mtu afanye kwa usawa na kwenye suala la mamlaka hawasemi kila mtu ajitawale mwenyewe

Wale waumini wa ukristo hasa wanaume kama mmeamua kufuata maandiko basi fuateni yote, na kama mmeamua kuyapuuzia basi yapuuzieni yote msichague yale yanayowanufaisha ninyi tu halafu mengine mnajifanya hamyaoni, kwa sababu maandiko yanasema mume ndio atakula kwa jasho na si mke, halafu mbele ndio yanaendelea kwamba mwanaume atamtawala mwanamke, yule mke mnayemuota wa Mithali 31 yalikuwa mawazo binafsi ya mfalme Suleiman na si maagizo ya muumba

Hivo basi ifike pahala wanaume mchague moja kati ya mwanamke mfanyakazi/mfanyabiashara au mama wa nyumbani, na aina yoyote utakayochagua hapo lazima ukubaliane na sifa zinazoambatana na aina hiyo ya mwanamke siyo unachagua mfanyakazi/mfanyabiashara mnasaidiana majukumu, halafu hapo hapo unataka awe kama mama wa nyumbani au unachagua mama wa nyumbani halafu hutaki kumhudumia unaanza kumuona golikipa
Uwezo wa akili za mwanamke ni robo ya mwanaume ....wanawake wengi wameolewa na matajiri na hao matajiri wakafa na kuacha mitaji ya mamilioni na mabilioni ila chakushangaza wanawake ni wachache wameweza kutumia hiyo fursa vizuri na kama wanawake wange kuwa na akili basi fursa ya kuwa wakeza mabilionea wangeitumia vizuri
 
Mungu alianza kumuumba Adam, akaona yupo mpweke, kutoka ktk nyama na mifupa ya Adam akamtwaa mwanamke Eva ili awe msaidizi wa mume wake pia ili Adam asiwe mpweke,

Kama uliumbwa ili uwe msaidizi wa Adam kwanini unataka Adam akufanyie Kila kitu wewe kazi yako itakuwa nini na utakua umeumbwa na Mungu ili iweje sasa
Atakwambia kugongwa na kuzaa basi, Jadda
Ndio kuzaa ongezea na kufanya kazi za nyumbani kama mnaziona rahisi mbona hamzifanyi na siyo tu kuzifanya bali hamzipendi, kwani ukitoa kuhudumia ni jukumu gani jingine mwanaume alilonalo juu ya mwanamke, kama mwanamke naye anajitafutia pesa zake jukumu la mwanaume kwa mke wake litakuwa ni lipi
 
Wazungu wenyewe baada ya kuimplement 50-50,talaka zimeiongezeka na kwa mujibu wa CNN US ndoa zimepungua kwa asilimia zaidi ya hamsini.Manake huo mfumo hauwezekani kuongoza familia na siku hizi huko mbele sababu ya ujuaji wenu, wanawake wajuaji kama nyinyi wanaume wanaume wanapiga na kutambaa.

US huko wanaandaa mpaka single events, special tu kuwakutanisha wanawake wapate waume,ila wanao jitokeza ni wanaume wachache. Kuna single event moja US,walijitokeza wanawake 147 na wanaume watatu tu mpaka muandaaji akawa analalamika na wengi walio jitokeza type zile zile zinazo jifanya wajuaji na wasomi wasiokuwa na maadili. Msijidanganye kwamba mnaogopwa hamna mwanaume anaogopa kumtongoza mwanamke yoyote, ila akigundua ni mjiuaji unapenda mashindano plus 50 -50 kibuti kikuhusu.

Hata humu wengu wenu, mkitongozwa mkitolewa dinner siku ya kwanza tu kwenye bili hatuwasikii mkisema tutoe nusu kwa nusu au kama yupo aliye lipa nusu ya bili baada ya kutolewa out siku ya kwanza anyooshe kidole.

Mfumo dume ndio msingi na ni nguvu iliyo iongoza dunia tokea kuumbwa kwake.
Wanawake hawawezi kukubali kufanya majukumu yenu ikiwa ninyi hamkubali kufanya majukumu yao huku bado mnataka kupewa heshima na utii eleweni hilo
 
Ndio kuzaa ongezea na kufanya kazi za nyumbani kama mnaziona rahisi mbona hamzifanyi na siyo tu kuzifanya bali hamzipendi, kwani ukitoa kuhudumia ni jukumu gani jingine mwanaume alilonalo juu ya mwanamke, kama mwanamke naye anajitafutia pesa zake jukumu la mwanaume kwa mke wake litakuwa ni lipi
Hivi wewe umeshaolewa au bado?
 
Haya mengine ni matatizo ya uwezo kiakili na afya ya akili.

Kuna watu ni sadistic tu wanataka ku control wengine kuwafanya kama watumwa wao.

Sasa kama mtu unajielewa na hutaki huo ujinga, unawakwepa tu.

Na mara nyingine wanakuwa very charming kwanza, lakini basically ukiwa muangalifu utawajua tu.
Yeah wanaume wengi wa kiafrika hawajioni wanaume bila kutaka wanawake wawaheshimu na kuwatii na wawe submissive na watumwa kwao
 
Hataki KUOLEWA. Anataka 'kuoana'. [emoji41]

-Kaveli-
Ndio kama unataka nikusaidie majukumu yako ya kutafuta pesa na kuhudumia familia hapo automatically tunakuwa tumeoana mkuu
 
Mkuu kwani michepuko si wanawake pia, hauoni bado tunazidi kusambaza upendo kwa wanawake tu?
Si unaona sasa, halafu kwa hali hii ndio mnalialia wanawake wawaonee huruma na wawasaidie majukumu, wakati mnaenda kuhonga michepuko ambayo nayo haina cha kuwapa zaidi ya ngono tu
 
Usitupangie chakufanya Kila mmoja anaishi kulingana na utashi wake, vipi wewe [emoji848][emoji848]
Sasa mbona ninyi mnawapangia wanawake cha kufanya, acheni nao waishi kulingana na utashi wao, kila mtu afanye kile anachoona kinamnufaisha na kinampa furaha
 
Mungu alianza kumuumba Adam, akaona yupo mpweke, kutoka ktk nyama na mifupa ya Adam akamtwaa mwanamke Eva ili awe msaidizi wa mume wake pia ili Adam asiwe mpweke,

Kama uliumbwa ili uwe msaidizi wa Adam kwanini unataka Adam akufanyie Kila kitu wewe kazi yako itakuwa nini na utakua umeumbwa na Mungu ili iweje sasa
Kwa hiyo Mwanaume ni kiumbe dhaifu kisicho na nguvu hadi Mungu akaamua kumletea msaidizi
 
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
binafsi jins nlivokuzwa nmekua nkiona mzee anahudumia familia na anamgawia posho extra bimkubwa japo nae alikua na kipato..naamini natakiwa kuhudumia kila kitu ndani na kum spoil mwanamke ata kama ana kipato nakiri wanaume wengi wanajisahau majukum yao. Imekua too much wamama wanatia fora kutafuta kuliko wanaume ni aibu ndo maana mnatudharau ni fedheha.
 
Upo smart sana , mumeo tukimwona kwenye chama la kataa ndoa ,tunamtimua na mapanga.

Hahaha asante rafiki….. eti lakini wanasema wachungaji wengi wanahubiri wasiyoyafanya? Wenyewe huwa wanatuambia fuata maneno yangu usifuate matendo😅

Kwahiyo siku mkimkuta chamani mpokeeni wala msimshangae.
 
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
Hiyo sentensi ya kugawana mali pasu kwa pasu huwa inachekesha sana.Kwani huwa hamuwezi kuondoka bila pasupasu?Au mnafidia "uchakavu wa godoro"?🤣🤣🤣🤣🤣
 
Yeah wanaume wengi wa kiafrika hawajioni wanaume bila kutaka wanawake wawaheshimu na kuwatii na wawe submissive na watumwa kwao
Kuna namna ya mwanamme kuwa na mvuto bila kulazimisha.

Kwa jinsi anavyoishi tu.

Inakuwa mpaka watu wanakuheshimu na kukupenda effortlessly, mpaka mara nyingine mwanamme anakuwa hataki makuu, hataki kujionesha sana, hataki hata kutongoza, lakini wanawake wanavutiwa tu na mwanamme. Kwa sababu huyo mwanamme anakuwa na qualities za uongozi na anavutia kama sumaku pengine bila hata yeye kujijua.

Huyo hahitaji kulazimisha watu wamuheshimu au wampende, watu watamuheshimu na kumpenda naturally tu. Yani hata akitaka kuwa low key kufanya mambo yake tu, watu watamtafuta wenyewe tu.

Wanaume wa hivyo ni kama wanasema "Hatutongozi. Tunaongoza".
 
Ndio kama unataka nikusaidie majukumu yako ya kutafuta pesa na kuhudumia familia hapo automatically tunakuwa tumeoana mkuu

Sihitaji msaada wako kimajukumu kwenye familia. Mie ndiyo nakuoa, wewe unaolewa. NATURE shall always prevail.

Habari za 'kuoana' ni kwenda against nature of which mahusiano ya kijinsia yapo likely to collapse kwenye hiyo ndoa.

N.B: Sio kila mwanamke 'anaoleka' despite mwanaume anatimiza majukumu yote fully kwenye familia.

Some women wameumbwa 'kuvutia' tu, siyo 'kuolewa'. 😎

-Kaveli-
 
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
Hakuna mwanaume aliyeoa akamwita mke wake omba omba ,labda awe na matatizo ya akili !! Omba omba ni vidada ambavyo havijaolewa vinavyotaka kutunzwa kama mke ! (hii issue tuwaachie mabachela ) Pia haimaanishi mwanamke akiolewa anafungwa mikono au akae abweteke na awe mvivu hapo maana ya msaidizi haipo tena sasa. kitabu cha mithali 31 kimeeleza vizuri mwanamke anavyotakiwa kuwa mchapakazi

10 Mke hodari ni nani anaweza kumpata? Thamani yake ni zaidi kuliko vito.

11 Moyo wa mume wake humwamini, na hatakuwa masikini.
12 Humtendea mambo mema na wala si mabaya siku zote za maisha yake.
13 Huchagua sufu na kitani, na hufanya kazi yake ya mikono kwa furaha.
14 Yupo kama meli za wafanyabiashara; huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Huamka wakati wa usiku na kuwapa chakula watu wa kaya yake, na kugawa kazi kwa watumishi wake wa kike.

16 Hulifikiria shamba na kulinunua, kwa tunda la mikono yake hupanda shamba la mizabibu.
17 Yeye mwenyewe hujivika nguvu na kuimarisha mikono yake.
18 Huangalia ni kipi kitaleta faida nzuri kwake; usiku wote taa yake haizimishwi.
19 Mikono yake huiweka kwenye mpini wa kisokotea nyuzi na hushikilia kisokotea nyuzi.
20 Mkono wake huwafikia watu masikini; mikono yake huwafikia watu wahitaji.
21 Haogopi theluji kwa ajili ya kaya yake, kwa maana nyumba yake yote imevika kwa nguo nyekundu. 22 Hutengeneza matandiko ya kitanda chake, na huvaa nguo za kitani ya dhambarau safi.
23 Mume wake anajulikana malangoni, anapoketi na wazee wa nchi.
24 Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, na naleta mishipi kwa wafanyabiashara.
25 Amevaa nguvu na heshima, na wakati ujao huucheka.
26 Anafumbua kinywa chake kwa hekima na sheria ya ukarimu ipo kwenye ulimi wake.
27 Huangalia njia za nyumba yake na hawezi kula mkate wa uvivu.
28 Watoto wake huinuka na kumwita heri na mume wake humsifia, akisema,
29 “Wanawake wengi wamefanya vizuri, lakini wewe umewapita wote.”
30 Madaha ni udanganyifu, uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Yehova, atasifiwa.
 
Back
Top Bottom