Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Wanawake hawawezi kukubali kufanya majukumu yenu ikiwa ninyi hamkubali kufanya majukumu yao huku bado mnataka kupewa heshima na utii eleweni hilo
Inawezekana ww unaona hawafanyi majukumu yao,sababu ndani ya nyuma nao wanataka 50-50,hamna mwanamke anaye kubali hii 50-50 na hamuipendi,hasa ikifiki kipindi cha kuchangia hiyo 50.

Hicho unacho kitaka haiwezekani kiasili, na hakito kuja kutokea.Nchi ya Europe wameshindwa hiko ukitakacho ww, ushajiuliza why?


Hivi ushajiuliza why jamii zote pamoja na mwanzoni hazikuwa hazijuani, ila majukumu ya mwanaume yana fanana na zote ziliendeshwa na mfume dume.

Huwezi shindana asili 50-50 hata wazungu hawaitaki, ndio maana siku hizi kuna kundi kubwa la wazungu kutoka ulaya wanaitwa Passport Bro,wanaoa wanawake kutoka mataifa mengine nje na ya kwao kama Africa,Thailand, Philippines na baadhi ya nchi za Latin America. Ushajiuliza wanakimbia nini?
 
Hiyo 50/50 unayotaka Mjukuu mtaweza majukumu yake?

Kwamba Mume atoe Kodi ya miezi 6 ya nyumba na Mke alipie miezi 6 iliyobaki ya Kodi.

Wanawake wenyewe ndiyo hawa ambao wanasema mshahara wao ni wao pekee ila wa Mshahara wa Mume ndiyo wa kutumika ndani ya nyumba?

Nina rafiki yangu ni Mzungu, wao ndiyo wanaiishi hiyo 50/50 ambapo wamegawana majukumu sawa sawa na Mume wake.

Ana watoto 2 na Mume wake, mtoto mmoja ana msomesha na kumgharamia yeye matibabu/mavazi na Kila kitu kuanzia alipozaliwa hadi Chuo Kikuu na mtoto mwingine ana gharamiwa yote hayo na Mume wake.

Nieleze kama Kuna Mwanamke Bongo hii ataweza kuyafanya hayo.

Ubunge wenyewe mnapewa bure bure na Chama
Babu kuna wazungu wengi tu ambao mke anaacha kazi ili alee familia, na mume anafanya kazi za kiuchumi, mke anafanya za nyumbani. Hapo hakuna 50/50. Tena juzi hapa kuna mtandao nilikua napita pita huko unaitwa “Tikotiko” sijui kama Babu Unaufahamu, kuna wale content creators wako mitaani wanahoji watu randomly, wakaisimamisha couple moja ya wazungu kuihoji juu ya mgawangiko wa majukumu katika familia yao, aliyejibu ni Mwanaume kuwa amemshauri mkewe aache kazi ili alee familia, yeye anasimamia show yote. Nadhani kwa nje sababu gharama za house helper ni kubwa so baadhi yao wanaona tu mke abaki home.

Mambo mengi yanategemea kipato cha wanandoa na mipango yao.

Dunia inabadilika ila haiwezi badilika 100%
 
Sasa mbona ninyi mnawapangia wanawake cha kufanya, acheni nao waishi kulingana na utashi wao, kila mtu afanye kile anachoona kinamnufaisha na kinampa furaha
Tuna mamlaka ya kuamua nini kifanyike na nini kisifanyike kwa wakati wowote na mahala popote na tutaendelea kua na hayo mamlaka hadi mwisho wa dunia na hakuna atakae weza kubadilisha hilo, huo ndio ukweli
 
Babu kuna wazungu wengi tu ambao mke anaacha kazi ili alee familia, na mume anafanya kazi za kiuchumi, mke anafanya za nyumbani. Hapo hakuna 50/50. Tena juzi hapa kuna mtandao nilikua napita pulita unaitwa “Tikotiko” sijui kama Babu Unaufahamu, kuna wale content creators wako mitaani wanahoji watu randomly, wakaisimamisha couple moja ya wazungu kuihoji juu ya mgawangiko wa majukumu katika familia yao, aliyejibu ni Mwanaume kuwa mke amemshauri mkewe aache kazi ili alee familia, yeye anasimamia show yote. Nadhani kwa nje sababu gharama za house helper ni kubwa so baadhi yao wanaona tu mke abaki home.

So nadhani mambo mengi yanategemea kipato cha wanandoa na mipango yao.

Dunia inabadilika ila haiwezi badilika 100%
Mfumo wa 50/50 binafsi nahisi ni kama umekuja kuvuruga maisha ya familia

Mimi nitaendelea ku-provide 100% Kwa familia na in return nataka anizalie watoto hata 12 akiweza 😜
 
Mkuu nimekuelewa vizuri sana lakini kwenye suala la ndoa hiyo delegation inayofanywa na mwanaume kwa mkewe lazima iwe na uhalisia na lazima izingatie uwezo na muda wa huyo anayepewa hayo majukumu, huwezi kumtwika msaidizi wako majukumu mengi kuzidi uwezo na muda alionao kwa sababu haiwezekani mwanamke atoke kuenda kutafuta pesa na bado afanye majukumu ya nyumbani kikamilifu, na hata hivyo kiongozi anatakiwa kudelegate majukumu kwa msaidizi pale tu anapoona majukumu aliyonayo yanamzidia sasa kama mwanamke anafanya majukumu yote ya kwake na ya mume wake je mume atakuwa anafanya majukumu gani

Majukumu ni natural instict, pindi mwanaume au mwanamke anapoanza kupata akili, anafunzwa na kujifunza maarifa yenye kubainisha majukumu kulingana na utofauti wa kijinsia...

Hivyo si jambo la kutaraji kwamba mwanaume ata delege majukumu fulani afanye mwanamke na mwengine afanye yeye...

Mwanamke anapaswa ajue wajibu na majukumu yake, hivyo hivyo mwanamume pia, isipokuwa endapo mwanamke atakengeuka ndiposa mwanaume kama kiongozi anarekebisha au anaelekeza usahihi wake (lead by example)...

Mwanamke kutoka kwenda kusaka pesa kwa ajili ya familia, hili sio jukumu lake la kwanza bali ni ziada tu, ni hadi pale mwanamume akiridhia...Swali, je wanawake mpo tayari mkiolewa mkae tu nyumbani?
 
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
Always malaya ndiye ana demand kuhudumiwa na anaendekeza tamaa.

Mwanamke mwema hana tamaa na anaridhika na anachopewa.

Hakuna mwanamme asiyependa kumuhudumia mwanamke wake.
 
Masculine ni provider na kiongozi, feminine ni receiver na ana nurture kile masculine ame kitafuta. Sasa wanawake wanataka wawe provider which will never work. Hata ukifikiria kawaida et mwanaume mzima umekaa home unalea watoto how will you feel? Haimek sense kbs. Hii generation bana🤣🤣🤣
 
Jadda my girl, mi nadhani tatizo halipo kwa wanaume tu, Hata kwa wanawake. Jamii yetu inatatizo la kuvamia mambo ambayo hatuyaelewi vizuri. Wanaume baadhi wanakwepa majukumu wakati huo wanataka mamlaka 100% na wakati huo huo wanawake, baadhi wanakwepa majukumu yao ya kike halafu wanataka huduma 100. Jamii kama hii lazima iwe na mvutano, ndio huu mtifuano tunao ushuhudia sasa.

Jamii imebadilika sana, 50/50 haikwepeki, Binafsi naiona iko very practical. Ni mfumo rahisi sana kuuadapt kuliko ule mfumo kale.

Swali ni je, Kwa sisi ambao wanaume zetu wametuzidi vipato mara 70, hii 50/50 tunawezaje kuipractice? Tukumbuke kwa hapa Tz, mara nyingi mwanaume mwenye kipato kikubwa ni mtu busy sana, 80% unavailable kwa mambo ya nyumbani/familia. (Someone can share her/his experience)

However , its important each family to customize their life style which accommodates them, To each their own. [emoji1635]
Yeah nimekuelewa vizuri my dear na mimi sijacondemn mfumo wowote ule na sina tatizo kabisa mtu akichagua mfumo wowote ule, tatizo ni pale mwanaume anapotaka mfumo fulani halafu anataka mwanamke mwenye sifa za mfumo mwingine, something whichi is illogical yani

Na kwa huo mfano wako ambao mwanaume kamzidi mwanamke wake kipato that much, basi nina uhakika hapo mwanaume ndio atakuwa anasimamia show kwa asilimia kubwa, na pia kwa asilimia fulani atakuwa anamhudumia mke wake and that is not 50 50

Mimi wanaume ninaowasemea ni wale wanaotaka mke wa kusaidiana naye majukumu ya kiuchumi, halafu hapo hapo mke ahangaike mwenyewe na majukumu ya nyumbani yani hata akiweka dada wa kazi ni kosa wengi tunajua kitakachofuata, whatever the case ila tusitengeneze mfumo ambao mwanamke ndio atafanya majukumu mengi kuliko mwanaume
 
Mi nadhani hao wanaosema hawataki wanawake magoli kipa kuna nukta muhimu unakuwa unaisahau.

Sidhani kama wanaosema hivyo humaanisha mwanamke aka hustle mwenyewe bila assist ya mumewe.

Wengi wanaosema hivyo utakuta wanawapa mitaji wake zao wajishuhulishe kwenye biashara ndogondogo zitazoweza kumfanya aweze kutatua ishu ndogondogo za pale nyumbani bila kuomba hela kwa mumewe.

Ila modern women wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya. Wengi wakipata hiyo nafasi huitumia kujiimarisha wao kiuchumi bila mume kujua na mwisho wa siku wakiona wamefikia malengo yao wanaanza kudai talaka.
Mkuu achana na ambao wanawafungulia biashara wake zao hao wala hawana shida kabisa, hujawahi kusikia kuna wanaume wao wakiwa wanatafuta wanawake wa kuoa kigezo cha kwanza ni mwanamke awe na shughuli inayomuingizia kipato, yani hawataki kabisa kusikia kuhusu suala la kuhudumia au kutunza mwanamke
 
Hao ni non responsible father's ambao hawakuwa tayari kuwa Wazazi

Ukiitwa Baba ni lazima ujue kusimama na kuendesha familia yako, sio kumuachia Mwanamke.

Sisi wengine tuko radhi tusivae ila familia ivae

Tuko radhi kutokulala Usingizi ili familia zipate mahitaji muhimu

Na huo ndiyo uanamme tuliofundishwa tukiwa jandoni miaka ile ya giza.

Kuhitimisha hoja yako ni kuwa, hao Wanawake wa kukubali majukumu ya 50/50 Tanzania bado hawapo.
Mkuu mimi naona hiyo ilikuwa zamani ila miaka hii ya utandawazi wapo wanawake ambao wako tayari kuchukua majukumu ya 50/50, ila shida ni wanaume wanakuwa hawako tayari kukubaliana na sifa ambazo zinakuja na mwanamke wa aina hiyo, hivyo wanawake nao wanaona hamna haja ya kujiingiza mazima kwenye huo mfumo ikiwa wanaume wenyewe hawako tayari
 
........Kwanza hapo huyo mke anakuwa siyo msaidizi tena bali ni kama business partner tu hivyo ondoa kichwani suala la kumlazimisha akutii, hivi mnadhani mwanamke aliambiwa amtii mwanaume kwa misingi gani kama siyo kuhudumiwa maana huwezi kukitawala kiumbe usichokihudumia, hakuna binadamu mwenye akili timamu anayefurahia kutawaliwa na binadamu mwenzie asiyewajibika kwa lolote juu yake na kiuhalisia ukitoa huduma zinazohusisha pesa hakuna wajibu mwingine mwanaume alionao juu ya mwanamke.......
Napenda kukukosoa Kwa kauli Yako Mbaya kuwa "mwanaume hana wajibu mwingine Kwa mwanamke zaidi ya Pesa"

Kwanza inatakiwa kutuomba msamaha wanaume wote Kwa kututukana ikiwemo Baba Yako maana naye pia mwanaume aliyemuoa Mama Yako.
 
Mkuu achana na hao ambao wanawafungulia biashara wake zao hao wala hawana shida kabisa, hujawahi kusikia kuna wanaume wao wakiwa wanatafuta wanawake wa kuoa kigezo cha kwanza ni huyo mwanamke awe na shughuli inayomuingizia kipato, yani hawataki kabisa kusikia kuhusu suala la kuhudumia mwanamke
Hapana sijawahi kuona mwanaume wa hivyo.

Kwanza binafsi yangu siwezi kupendezewa kumuoa mwanamke ambaye nimemkuta yuko na biashara ambayo haina mkono wangu.

Kwasababu najua ili heshima iwepo ndani inatakiwa njia zote za uingizaji kipato ziwe created na mimi.

Naamini ndoa hudumu sababu ya woga kwa maana upendo kuna muda huisha.

Mwanamke akiwa na biashara ambayo alijitafutia yeye mtaji kwa nguvu zake maana yake mimi siwezi kuwa na sauti yeyote kwenye hiyo biashara (kitu ambacho mimi binafsi siwezi kukubaliana nacho)

Kukosa sauti ni kukosa mamlaka, kukosa mamlaka ni kupoteza control kama kichwa cha familia.

Automatically mpaka hapo unaona kabisa ugumu wa hiyo ndoa.

Ndio maana mimi nasema kwenye kipaumbele cha kuoa naweza kuwapa nafasi kubwa wanawake ambao sio waajiriwa na hawana kazi kuliko wale walio ajiriwa.
 
Uwezo wa akili za mwanamke ni robo ya mwanaume ....wanawake wengi wameolewa na mattajiri na hao matajiri wakafa na kuacha mitaji ya mamilioni na mabilioni ila chakushangaza wanawake ni wavmchache wameweza kutumia hiyo fursa vizuri na kama wanawake wangekuwa na akili basi fursa ya kuwa wakeza mabilionea wangeitumia vizuri
Mkuu kwani hakuna wanaume ambao wameachiwa utajiri na wazazi au ndugu zao na wakashindwa kuuendeleza au hili linakuwa tatizo likifanywa na mwanamke tu, kwahiyo unataka kusema kwamba wanaume wote ni intellectually superior kuliko wanawake wote na umetumia vigezo gani, kwamba other factors being constant hata kama mwanaume ni kibaka wa mtaani basi ana akili kuliko mwanamke ambaye ni boss wa kampuni fulani
 
Hivi wewe umeshaolewa au bado?
Huwa sijibu personal questions mkuu, kama una hoja inayohusiana na mada wasilisha tujadiliane, kama huna basi nafikiri utakuwa umekosea njia
 
binafsi jins nlivokuzwa nmekua nkiona mzee anahudumia familia na anamgawia posho extra bimkubwa japo nae alikua na kipato..naamini natakiwa kuhudumia kila kitu ndani na kum spoil mwanamke ata kama ana kipato nakiri wanaume wengi wanajisahau majukum yao. Imekua too much wamama wanatia fora kutafuta kuliko wanaume ni aibu ndo maana mnatudharau ni fedheha.
Yeah mkuu kama mwanaume anatimiza majukumu yake yote bila kumtegemea mke basi hapo hakuna haja ya 50/50, tena huyo mwanamke atakayedai 50/50 katika mazingira hayo atakuwa hana akili kabisa, shida ipo kwa wanaume wasiotaka kutimiza majukumu yao halafu wanataka mamlaka hapo ndipo shida inapoanzia
 
Back
Top Bottom