Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Mkuu kama hamtaki 50 50 basi hudumieni wake zenu 100%, na siku mkiachana gawaneni mali pasu kwa pasu, simple tu
 
Hakuna lolote lidaiwalo hapo.Fedha inaleta mgagasiko kifikra na kuleta tamaa ya uporaji wa haki,uongozi na mgawanyo wa majukumu.
Feminist jadda
Mnakimbilia ndoa yakiwabana huko mnaanza kutushushia magazeti usiku....mabachela hizi porojo hazituhusu
Kuufuta mfumo dume ni ngumu sana mkuu.
Hongera sana mkuu bandiko lako ni tamu sana maana linatupeleka kule kwetu NDOA NI UTAPELI, KATAA NDOA

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama lengo ni kuangalia wapi kosa limefanyika basi wakufanya hivyo ni sisi wanaume

Wanaume ndio tulifanya kosa kuwapeni uhuru uliopitiliza (tukiamini kufanya hivyo ni upendo) mpaka sasa uhuru huo unaenda kuwa silaha inayoturudia wenyewe.
Sasahivi mnagombea 50 zenu na mashoga
Ndio maana LGBTQ inakua kwa kasi kubwa.....
50/50 maana yake fursa sawa kwa jinsia ya ke na me kielimu , nakadhalika haina maana nyingine sema watu hawaelewagi wanachukua maneno ya vijiweni kuwa mwanamke kuwa sawa na mwanaume kitu ambacho sio kweli.
Umeandika gazeti kabisa alafu ni pumba tupu kuanzia mwanzo hadi mwisho
kuparuana kote kule kwenye comment za watu kumbe shida yako ni 50/50
Hahahahahaha..mnavyopenda kitonga hamuwezi hii kitu
Wameangamia/ameangamia mwenye kumfanya mwanamk kuwa kiongozi/kuwa kichwa kwenye banda lanaume
Mkimaliza hili, mtaanza kuomba kuoana wenyewe kwa wenyewe.

Hamna akili hata kidogo, ni ujinga wenu tuu.
Umeandika Kama singo maza mmoja hivi!
Huo mjadala tulishaufunga

Hakuna mwanaume atakubali hilo
Mimi sijasema kwamba hapo kuna mfumo mbaya au mzuri bali nimewaambia wanaume wachague mfumo mmoja na mfumo wowote watakaochagua wakubaliane na sifa zake, kama hamtaki 50/50 basi hudumieni wake zenu kwa asilimia 100 siyo tena mnaanza kusema hamtaki wanawake ombaomba na magolikipa mara oo hamuwezi kuhudumia watu wazima wenye viungo vyote nao wajitafutie zao wajihudumie wenyewe, na pia ikitokea mmeachana kwenye ndoa mkubali kugawana mali pasu kwa pasu bila kujali mmetafuta wote au la na hiyo ndio maana halisi ya mfumo dume
 
Yeah niliwahi kuambiwa hili kwamba kwa waislam jukumu la mwanamke ni kuzaa na kupamba nyumba, kazi za nyumbani mume anatakiwa aweke msaidizi, ila hili hutasikia wakilisema wao wanajua kutetea habari za kuoa wake wanne tu
 
Haha babu kwani mnaishi sayari gani mbona huku nje kuna wanawake wengi wameachiwa majukumu yote ya kina baba huku wanaume wameamua kuwa wazinzi na walevi tu, ukiuliza utasikia tatizo huyu mwanamke mjeuri sana anataka kunipanda kichwani acha afanye kila kitu mwenyewe, ukweli ni kwamba nyumba nyingi siku hizi wanawake ndio wanasimamia show nzima ila wengi wameamua kukaa kimya tu sababu hata wakisema wataambiwa chanzo ni wao wenyewe kwa kuwa na viburi na kuwapanda waume zao vichwani
 
Achana na haya mafurushi, hata hayajui nini yanataka.
Ila wanaume halisi wanajua na walaa hawalalamiki.
Yani tuna kizazi cha ajabu sana, mtu anataka mamlaka ila majukumu hayataki ukimuuliza anaanza kutafutiza majukumu ambayo hayapo au yale ambayo siyo ya kila siku, eti mbona ikitokea vita hamuendi au mbona wezi wakivamia hampambani nao sasa unajiuliza hiyo nyumba gani ambayo wezi wanavamia kila siku
 
Mtoa mada upo sahihi kabisa hii 50/ 50 ikienda kama inavyotakiwa hakika mambo yatakua mazuri sna , itapungaza vifo vya wanaume wengi wanaojifanya kichwa cha familia kupambania mke na watoto peke yake , mwisho wa siku anarisk maisha yake kwenye kazi hatarishi bila usaidizi kwa mwenza wake .

50/ 50 kwa apa duniani bado haifanyi kazi kama inavyotakiwa kuna namna inategemea upande mmoja , na hii ya kuegemea upande mmoja ipo makusudi kabisa kwa nia ya kumlinda mwanamke na madhara ya mfumo wa haki sawa .

Mfumo dume ni mfumo ulio tumika kumlinda mwanamke na kumpa heshima yake kama mama wa dunia, ukitoa mapungufu yake kama kumnyima mtoto wa kike haki ya kusoma , na haki ya kuchagua mwenza wake , hakuna shida nyingne kabisa ,labda tu mwanaume awe mjinga na asie tumia akili.
 
Mkuu kwani michepuko si wanawake pia, hauoni bado tunazidi kusambaza upendo kwa wanawake tu?
 
Usitupangie chakufanya Kila mmoja anaishi kulingana na utashi wake, vipi wewe 🤔🤔
 
Mi nadhani hao wanaosema hawataki wanawake magoli kipa kuna nukta muhimu unakuwa unaisahau.

Sidhani kama wanaosema hivyo humaanisha mwanamke aka hustle mwenyewe bila assist ya mumewe.

Wengi wanaosema hivyo utakuta wanawapa mitaji wake zao wajishuhulishe kwenye biashara ndogondogo zitazoweza kumfanya aweze kutatua ishu ndogondogo za pale nyumbani bila kuomba hela kwa mumewe.

Ila modern women wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya. Wengi wakipata hiyo nafasi huitumia kujiimarisha wao kiuchumi bila mume kujua na mwisho wa siku wakiona wamefikia malengo yao wanaanza kudai talaka.
 
Hao ni non responsible father's ambao hawakuwa tayari kuwa Wazazi

Ukiitwa Baba ni lazima ujue kusimama na kuendesha familia yako, sio kumuachia Mwanamke.

Sisi wengine tuko radhi tusivae ila familia ivae

Tuko radhi kutokulala Usingizi ili familia zipate mahitaji muhimu

Na huo ndiyo uanamme tuliofundishwa tukiwa jandoni miaka ile ya giza.

Kuhitimisha hoja yako ni kuwa, hao Wanawake wa kukubali majukumu ya 50/50 Tanzania bado hawapo.
 
Jadda my girl, mi nadhani tatizo halipo kwa wanaume tu, Hata kwa wanawake. Jamii yetu inatatizo la kuvamia mambo ambayo hatuyaelewi vizuri. Wanaume baadhi wanakwepa majukumu wakati huo wanataka mamlaka 100% na wakati huo huo wanawake, baadhi wanakwepa majukumu yao ya kike halafu wanataka huduma 100. Jamii kama hii lazima iwe na mvutano, ndio huu mtifuano tunao ushuhudia sasa.

Jamii imebadilika sana, 50/50 haikwepeki, Binafsi naiona iko very practical. Ni mfumo rahisi sana kuuadapt kuliko ule mfumo kale.

Swali ni je, Kwa sisi ambao wanaume zetu wametuzidi vipato mara 70, hii 50/50 tunawezaje kuipractice? Tukumbuke kwa hapa Tz, mara nyingi mwanaume mwenye kipato kikubwa ni mtu busy sana, 80% unavailable kwa mambo ya nyumbani/familia. (Someone can share her/his experience)

However , its important each family to customize their life style which accommodates them, To each their own. 🥂
 
Mkuu nimekuelewa vizuri sana lakini kwenye suala la ndoa hiyo delegation inayofanywa na mwanaume kwa mkewe lazima iwe na uhalisia na lazima izingatie uwezo na muda wa huyo anayepewa hayo majukumu, huwezi kumtwika msaidizi wako majukumu mengi kuzidi uwezo na muda alionao kwa sababu haiwezekani mwanamke atoke kuenda kutafuta pesa na bado afanye majukumu ya nyumbani kikamilifu, na hata hivyo kiongozi anatakiwa kudelegate majukumu kwa msaidizi pale tu anapoona majukumu aliyonayo yanamzidia sasa kama mwanamke anafanya majukumu yote ya kwake na ya mume wake je mume atakuwa anafanya majukumu gani
 
Upo smart sana , mumeo tukimwona kwenye chama la kataa ndoa ,tunamtimua na mapanga.
 
Ndio kazi za nyumbani pamoja na kutaka mume amtawale mke ndio kigezo cha kudai 50/50, sasa kama kazi za nyumbani mnaziona rahisi kwanini ninyi hamtaki kuzifanya tena hakuna kazi wanaume hamzipendi kama kuosha vyombo na kufanya usafi, ila mnataka wanawake wazifanye na mnataka wao wazione rahisi
 
Hapa tunaongelea majukumu ya kila siku ya kwenye maisha ya mwanadamu hatuongelei vita au other man made disasters hayo siyo majukumu ya kila siku, ninyi ndio wale mnatolea mifano eti mwizi akivamia nyumbani mke hatoki kupambana kwani wezi kuvamia nyumbani ni suala linalotokea kila siku kwenye kila nyumba, wanaoanzisha hizo vita ni wanaume badala ya watu kukemea hizo vita mnakomaa eti na wanawake nao wawe ni sehemu ya vita na kuweka hilo kama sehemu ya majukumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…