Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Shukrani sana kwa kunielewa mkuu
 
Uwezo wa akili za mwanamke ni robo ya mwanaume ....wanawake wengi wameolewa na matajiri na hao matajiri wakafa na kuacha mitaji ya mamilioni na mabilioni ila chakushangaza wanawake ni wachache wameweza kutumia hiyo fursa vizuri na kama wanawake wange kuwa na akili basi fursa ya kuwa wakeza mabilionea wangeitumia vizuri
 
Atakwambia kugongwa na kuzaa basi, Jadda
Ndio kuzaa ongezea na kufanya kazi za nyumbani kama mnaziona rahisi mbona hamzifanyi na siyo tu kuzifanya bali hamzipendi, kwani ukitoa kuhudumia ni jukumu gani jingine mwanaume alilonalo juu ya mwanamke, kama mwanamke naye anajitafutia pesa zake jukumu la mwanaume kwa mke wake litakuwa ni lipi
 
Wanawake hawawezi kukubali kufanya majukumu yenu ikiwa ninyi hamkubali kufanya majukumu yao huku bado mnataka kupewa heshima na utii eleweni hilo
 
Hivi wewe umeshaolewa au bado?
 
Yeah wanaume wengi wa kiafrika hawajioni wanaume bila kutaka wanawake wawaheshimu na kuwatii na wawe submissive na watumwa kwao
 
Hataki KUOLEWA. Anataka 'kuoana'. [emoji41]

-Kaveli-
Ndio kama unataka nikusaidie majukumu yako ya kutafuta pesa na kuhudumia familia hapo automatically tunakuwa tumeoana mkuu
 
Mkuu kwani michepuko si wanawake pia, hauoni bado tunazidi kusambaza upendo kwa wanawake tu?
Si unaona sasa, halafu kwa hali hii ndio mnalialia wanawake wawaonee huruma na wawasaidie majukumu, wakati mnaenda kuhonga michepuko ambayo nayo haina cha kuwapa zaidi ya ngono tu
 
Usitupangie chakufanya Kila mmoja anaishi kulingana na utashi wake, vipi wewe [emoji848][emoji848]
Sasa mbona ninyi mnawapangia wanawake cha kufanya, acheni nao waishi kulingana na utashi wao, kila mtu afanye kile anachoona kinamnufaisha na kinampa furaha
 
Kwa hiyo Mwanaume ni kiumbe dhaifu kisicho na nguvu hadi Mungu akaamua kumletea msaidizi
 
binafsi jins nlivokuzwa nmekua nkiona mzee anahudumia familia na anamgawia posho extra bimkubwa japo nae alikua na kipato..naamini natakiwa kuhudumia kila kitu ndani na kum spoil mwanamke ata kama ana kipato nakiri wanaume wengi wanajisahau majukum yao. Imekua too much wamama wanatia fora kutafuta kuliko wanaume ni aibu ndo maana mnatudharau ni fedheha.
 
Upo smart sana , mumeo tukimwona kwenye chama la kataa ndoa ,tunamtimua na mapanga.

Hahaha asante rafiki….. eti lakini wanasema wachungaji wengi wanahubiri wasiyoyafanya? Wenyewe huwa wanatuambia fuata maneno yangu usifuate matendo😅

Kwahiyo siku mkimkuta chamani mpokeeni wala msimshangae.
 
Hiyo sentensi ya kugawana mali pasu kwa pasu huwa inachekesha sana.Kwani huwa hamuwezi kuondoka bila pasupasu?Au mnafidia "uchakavu wa godoro"?🤣🤣🤣🤣🤣
 
Yeah wanaume wengi wa kiafrika hawajioni wanaume bila kutaka wanawake wawaheshimu na kuwatii na wawe submissive na watumwa kwao
Kuna namna ya mwanamme kuwa na mvuto bila kulazimisha.

Kwa jinsi anavyoishi tu.

Inakuwa mpaka watu wanakuheshimu na kukupenda effortlessly, mpaka mara nyingine mwanamme anakuwa hataki makuu, hataki kujionesha sana, hataki hata kutongoza, lakini wanawake wanavutiwa tu na mwanamme. Kwa sababu huyo mwanamme anakuwa na qualities za uongozi na anavutia kama sumaku pengine bila hata yeye kujijua.

Huyo hahitaji kulazimisha watu wamuheshimu au wampende, watu watamuheshimu na kumpenda naturally tu. Yani hata akitaka kuwa low key kufanya mambo yake tu, watu watamtafuta wenyewe tu.

Wanaume wa hivyo ni kama wanasema "Hatutongozi. Tunaongoza".
 
Ndio kama unataka nikusaidie majukumu yako ya kutafuta pesa na kuhudumia familia hapo automatically tunakuwa tumeoana mkuu

Sihitaji msaada wako kimajukumu kwenye familia. Mie ndiyo nakuoa, wewe unaolewa. NATURE shall always prevail.

Habari za 'kuoana' ni kwenda against nature of which mahusiano ya kijinsia yapo likely to collapse kwenye hiyo ndoa.

N.B: Sio kila mwanamke 'anaoleka' despite mwanaume anatimiza majukumu yote fully kwenye familia.

Some women wameumbwa 'kuvutia' tu, siyo 'kuolewa'. 😎

-Kaveli-
 
Hakuna mwanaume aliyeoa akamwita mke wake omba omba ,labda awe na matatizo ya akili !! Omba omba ni vidada ambavyo havijaolewa vinavyotaka kutunzwa kama mke ! (hii issue tuwaachie mabachela ) Pia haimaanishi mwanamke akiolewa anafungwa mikono au akae abweteke na awe mvivu hapo maana ya msaidizi haipo tena sasa. kitabu cha mithali 31 kimeeleza vizuri mwanamke anavyotakiwa kuwa mchapakazi

10 Mke hodari ni nani anaweza kumpata? Thamani yake ni zaidi kuliko vito.

11 Moyo wa mume wake humwamini, na hatakuwa masikini.
12 Humtendea mambo mema na wala si mabaya siku zote za maisha yake.
13 Huchagua sufu na kitani, na hufanya kazi yake ya mikono kwa furaha.
14 Yupo kama meli za wafanyabiashara; huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Huamka wakati wa usiku na kuwapa chakula watu wa kaya yake, na kugawa kazi kwa watumishi wake wa kike.

16 Hulifikiria shamba na kulinunua, kwa tunda la mikono yake hupanda shamba la mizabibu.
17 Yeye mwenyewe hujivika nguvu na kuimarisha mikono yake.
18 Huangalia ni kipi kitaleta faida nzuri kwake; usiku wote taa yake haizimishwi.
19 Mikono yake huiweka kwenye mpini wa kisokotea nyuzi na hushikilia kisokotea nyuzi.
20 Mkono wake huwafikia watu masikini; mikono yake huwafikia watu wahitaji.
21 Haogopi theluji kwa ajili ya kaya yake, kwa maana nyumba yake yote imevika kwa nguo nyekundu. 22 Hutengeneza matandiko ya kitanda chake, na huvaa nguo za kitani ya dhambarau safi.
23 Mume wake anajulikana malangoni, anapoketi na wazee wa nchi.
24 Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, na naleta mishipi kwa wafanyabiashara.
25 Amevaa nguvu na heshima, na wakati ujao huucheka.
26 Anafumbua kinywa chake kwa hekima na sheria ya ukarimu ipo kwenye ulimi wake.
27 Huangalia njia za nyumba yake na hawezi kula mkate wa uvivu.
28 Watoto wake huinuka na kumwita heri na mume wake humsifia, akisema,
29 “Wanawake wengi wamefanya vizuri, lakini wewe umewapita wote.”
30 Madaha ni udanganyifu, uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Yehova, atasifiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…