Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Wanawake hawawezi kukubali kufanya majukumu yenu ikiwa ninyi hamkubali kufanya majukumu yao huku bado mnataka kupewa heshima na utii eleweni hilo
Inawezekana ww unaona hawafanyi majukumu yao,sababu ndani ya nyuma nao wanataka 50-50,hamna mwanamke anaye kubali hii 50-50 na hamuipendi,hasa ikifiki kipindi cha kuchangia hiyo 50.

Hicho unacho kitaka haiwezekani kiasili, na hakito kuja kutokea.Nchi ya Europe wameshindwa hiko ukitakacho ww, ushajiuliza why?


Hivi ushajiuliza why jamii zote pamoja na mwanzoni hazikuwa hazijuani, ila majukumu ya mwanaume yana fanana na zote ziliendeshwa na mfume dume.

Huwezi shindana asili 50-50 hata wazungu hawaitaki, ndio maana siku hizi kuna kundi kubwa la wazungu kutoka ulaya wanaitwa Passport Bro,wanaoa wanawake kutoka mataifa mengine nje na ya kwao kama Africa,Thailand, Philippines na baadhi ya nchi za Latin America. Ushajiuliza wanakimbia nini?
 
Babu kuna wazungu wengi tu ambao mke anaacha kazi ili alee familia, na mume anafanya kazi za kiuchumi, mke anafanya za nyumbani. Hapo hakuna 50/50. Tena juzi hapa kuna mtandao nilikua napita pita huko unaitwa “Tikotiko” sijui kama Babu Unaufahamu, kuna wale content creators wako mitaani wanahoji watu randomly, wakaisimamisha couple moja ya wazungu kuihoji juu ya mgawangiko wa majukumu katika familia yao, aliyejibu ni Mwanaume kuwa amemshauri mkewe aache kazi ili alee familia, yeye anasimamia show yote. Nadhani kwa nje sababu gharama za house helper ni kubwa so baadhi yao wanaona tu mke abaki home.

Mambo mengi yanategemea kipato cha wanandoa na mipango yao.

Dunia inabadilika ila haiwezi badilika 100%
 
Sasa mbona ninyi mnawapangia wanawake cha kufanya, acheni nao waishi kulingana na utashi wao, kila mtu afanye kile anachoona kinamnufaisha na kinampa furaha
Tuna mamlaka ya kuamua nini kifanyike na nini kisifanyike kwa wakati wowote na mahala popote na tutaendelea kua na hayo mamlaka hadi mwisho wa dunia na hakuna atakae weza kubadilisha hilo, huo ndio ukweli
 
Mfumo wa 50/50 binafsi nahisi ni kama umekuja kuvuruga maisha ya familia

Mimi nitaendelea ku-provide 100% Kwa familia na in return nataka anizalie watoto hata 12 akiweza 😜
 

Majukumu ni natural instict, pindi mwanaume au mwanamke anapoanza kupata akili, anafunzwa na kujifunza maarifa yenye kubainisha majukumu kulingana na utofauti wa kijinsia...

Hivyo si jambo la kutaraji kwamba mwanaume ata delege majukumu fulani afanye mwanamke na mwengine afanye yeye...

Mwanamke anapaswa ajue wajibu na majukumu yake, hivyo hivyo mwanamume pia, isipokuwa endapo mwanamke atakengeuka ndiposa mwanaume kama kiongozi anarekebisha au anaelekeza usahihi wake (lead by example)...

Mwanamke kutoka kwenda kusaka pesa kwa ajili ya familia, hili sio jukumu lake la kwanza bali ni ziada tu, ni hadi pale mwanamume akiridhia...Swali, je wanawake mpo tayari mkiolewa mkae tu nyumbani?
 
Always malaya ndiye ana demand kuhudumiwa na anaendekeza tamaa.

Mwanamke mwema hana tamaa na anaridhika na anachopewa.

Hakuna mwanamme asiyependa kumuhudumia mwanamke wake.
 
Masculine ni provider na kiongozi, feminine ni receiver na ana nurture kile masculine ame kitafuta. Sasa wanawake wanataka wawe provider which will never work. Hata ukifikiria kawaida et mwanaume mzima umekaa home unalea watoto how will you feel? Haimek sense kbs. Hii generation bana🤣🤣🤣
 
Yeah nimekuelewa vizuri my dear na mimi sijacondemn mfumo wowote ule na sina tatizo kabisa mtu akichagua mfumo wowote ule, tatizo ni pale mwanaume anapotaka mfumo fulani halafu anataka mwanamke mwenye sifa za mfumo mwingine, something whichi is illogical yani

Na kwa huo mfano wako ambao mwanaume kamzidi mwanamke wake kipato that much, basi nina uhakika hapo mwanaume ndio atakuwa anasimamia show kwa asilimia kubwa, na pia kwa asilimia fulani atakuwa anamhudumia mke wake and that is not 50 50

Mimi wanaume ninaowasemea ni wale wanaotaka mke wa kusaidiana naye majukumu ya kiuchumi, halafu hapo hapo mke ahangaike mwenyewe na majukumu ya nyumbani yani hata akiweka dada wa kazi ni kosa wengi tunajua kitakachofuata, whatever the case ila tusitengeneze mfumo ambao mwanamke ndio atafanya majukumu mengi kuliko mwanaume
 
Mkuu achana na ambao wanawafungulia biashara wake zao hao wala hawana shida kabisa, hujawahi kusikia kuna wanaume wao wakiwa wanatafuta wanawake wa kuoa kigezo cha kwanza ni mwanamke awe na shughuli inayomuingizia kipato, yani hawataki kabisa kusikia kuhusu suala la kuhudumia au kutunza mwanamke
 
Mkuu mimi naona hiyo ilikuwa zamani ila miaka hii ya utandawazi wapo wanawake ambao wako tayari kuchukua majukumu ya 50/50, ila shida ni wanaume wanakuwa hawako tayari kukubaliana na sifa ambazo zinakuja na mwanamke wa aina hiyo, hivyo wanawake nao wanaona hamna haja ya kujiingiza mazima kwenye huo mfumo ikiwa wanaume wenyewe hawako tayari
 
Napenda kukukosoa Kwa kauli Yako Mbaya kuwa "mwanaume hana wajibu mwingine Kwa mwanamke zaidi ya Pesa"

Kwanza inatakiwa kutuomba msamaha wanaume wote Kwa kututukana ikiwemo Baba Yako maana naye pia mwanaume aliyemuoa Mama Yako.
 
Hapana sijawahi kuona mwanaume wa hivyo.

Kwanza binafsi yangu siwezi kupendezewa kumuoa mwanamke ambaye nimemkuta yuko na biashara ambayo haina mkono wangu.

Kwasababu najua ili heshima iwepo ndani inatakiwa njia zote za uingizaji kipato ziwe created na mimi.

Naamini ndoa hudumu sababu ya woga kwa maana upendo kuna muda huisha.

Mwanamke akiwa na biashara ambayo alijitafutia yeye mtaji kwa nguvu zake maana yake mimi siwezi kuwa na sauti yeyote kwenye hiyo biashara (kitu ambacho mimi binafsi siwezi kukubaliana nacho)

Kukosa sauti ni kukosa mamlaka, kukosa mamlaka ni kupoteza control kama kichwa cha familia.

Automatically mpaka hapo unaona kabisa ugumu wa hiyo ndoa.

Ndio maana mimi nasema kwenye kipaumbele cha kuoa naweza kuwapa nafasi kubwa wanawake ambao sio waajiriwa na hawana kazi kuliko wale walio ajiriwa.
 
Mkuu kwani hakuna wanaume ambao wameachiwa utajiri na wazazi au ndugu zao na wakashindwa kuuendeleza au hili linakuwa tatizo likifanywa na mwanamke tu, kwahiyo unataka kusema kwamba wanaume wote ni intellectually superior kuliko wanawake wote na umetumia vigezo gani, kwamba other factors being constant hata kama mwanaume ni kibaka wa mtaani basi ana akili kuliko mwanamke ambaye ni boss wa kampuni fulani
 
Hivi wewe umeshaolewa au bado?
Huwa sijibu personal questions mkuu, kama una hoja inayohusiana na mada wasilisha tujadiliane, kama huna basi nafikiri utakuwa umekosea njia
 
Yeah mkuu kama mwanaume anatimiza majukumu yake yote bila kumtegemea mke basi hapo hakuna haja ya 50/50, tena huyo mwanamke atakayedai 50/50 katika mazingira hayo atakuwa hana akili kabisa, shida ipo kwa wanaume wasiotaka kutimiza majukumu yao halafu wanataka mamlaka hapo ndipo shida inapoanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…