joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 17,420
- 35,765
Mara nyingi tabia mlizo kuwa nazo na matendo mnayo tendeana kipindi cha uchumba ndivyo kwenye ndoa mtatendeana hivyo hivyo,kwani tabia hujenga mazoea.Mkuu ndio maana nikasema wanawake hawawezi kuikubali hiyo 50/50 ikiwa wanaume bado mnataka kupewa heshima na utii na bado kuna majukumu ambayo mnayaona ni ya wanawake tu, ofcourse na mimi sijalazimisha watu wachague huo mfumo wa 50/50 bali nimesema mwanaume anapochagua mfumo fulani ahakikishe anakubaliana na sifa zote zinazokuja na mwanamke wa huo mfumo, sasa wewe hutaki 50/50 lakini hapo hapo hutaki kumhudumia mwanamke wako unataka ajitafutie pesa zake ajihudumie mwenyewe na pia akusaidie kuhudumia familia ambalo ni jukumu lako mwanaume
Sasa na kuuliza ww na wanawake wenzako, NANI HUENDESHA MAHUSIANO YAKE KIPINDI CHA UCHUMBA KWA MTINDO WA 50/50?
Maana kama uchumba wenu hamkuliishi hili la 50/50 husitegemee kwenye ndoa ndio utaweza.