Mimi ni Mkristo mlokole, nimeanza kukosa Imani na ukristo nahisi Uislam ndiyo dini ya kweli



Ujawahi kuufaham Ukristo, maana Biblia yako imetabiri yote hayo unayolalamikia kwamba yatatokea siku za mwisho.

Hakuna mwanadam aliyeonja kwa ukweli vipawa vya roho mtakatifu na kuvielewa anayeweza kuongelea swala la kuwa Mwislam.
 
Mmmmh kama ukristo wako,unaujenga kwa kuangalia watu na "wachungaji wa mchongo" Waliojaa kila Kona, utapotea, bongo hakuna mahubiri ni utapeli mtupu, wanahubiri sadaka tu,
Nenda YouTube, msikilize Myles
Munroe, John hagee, na wengine wa USA, harafu uje utoe mrjesho,
 
Huwa navurugwa sana nikiingia kanisani mambo mengi yamebadilika! Kanisa la Sasa imekuwa sehemu ya disco ,dance na mitindo ya hovyo ya mavazi,wanawake wanavaa nguo ambazo hata kwenye baadhi ya bar hawavai na wachungaji wako busy na mapato na

 
Yesu Hana kanisa ,kanisa linaongozwa na mchungaji Kila muumini ana mchungaji wake ,mchungaji akipotoka kanisa lote linapotoka !
Hapo sio kweli wakati WA Nuhu dunia nzima ya wakati wake ilipotea lakini Nuhu peke yake alikuwa mkamilifu mbele za Bwana

Wakati WA sodoma na Gomora mji mzima walikuwa wameharibika lakini Lutu pekee alikuwa amemempendeza Mungu

Wakati WA Musa Wana waisraeli wote walimuhasi Mungu lakini Musa alikuwa upande wa Mungu ni maamuzi yako kumchagua Mungu ni uchaguzi pia ukiona wengi wape ni Sawa pia lakini Mimi na Nyumba yangu tatamtumikia Bwana
 
kwa kifupi, wewe sio mkristo, na sio mlokole, na kama ulishawahi kuwa mlokole basi ulikuwa mlokole wa dini haujawahi kukutana na Mungu moyoni mwako na bado ulikuwa unaelekea motoni kama wapagani wengine tu. hakuna mlokole wa kweli aliyewahi kukutana na Yesu moyoni aliyewahi kutamani uislam, Yesu Kristo ni Nuru ya Ulimwengu, huwezi kupenda giza kama ulishawahi kuonja nuru.
 
Wewe siyo mkristo uliyeokoka brother Bali ulikuwa unafuata mkumbo. Ungekuwa mkristo ungefuata maandiko maana hayo yote yapo katika maandiko.

Wewe unaangalia watu wanafanya nini na siyo neno la Mungu linasema Nini. Ukisoma mathayo 24 utaelewa.
 
Hama tu mkuu,wote tunabahatisha ukitaka kuwa atheist pia sawa bado kidogo sana tutaenda kuujua ukweli.

Kama leo unapumua kesho unaweza ukaamkia sehemu tofauti ukiwa tayari na jibu mkononi unasubiri nini?goodluck!
 
Uchaguzi ni wako,ila fuata nini maandiko yanasema maana ,yanasema jihadharani na roho zidanganyazo na mtawatambua kwa matunda yao.
 
Huko Vatican walijifungia siku 26 na mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini duniani
Wamekuja na mkakati gani siku zote hizo
Vatican na huyu ni maji na mafuta hapa ni vitu viwili tofauti vinazungumzwa
 
Hata Roman Catholic hapa nchini ni kizinguzungu tu. Utamsikia mtu akitamka Kristu/kristo, Yosefu/yusufu n.k. ilimradi vurugu tu siku hizi.
 
Uko sahihi kabisa baada ya miaka 10 ukristo utakuwa sawa na fiesta.
Ona ibada za siku hizi za akina amsanja vijana wanapenda vitu rahisi rahisi.
Manabii sasa ndio usiseme.
Ukristo unajifia
Nilimsikia nabii mkuu na mtume mkuu dr Geordavie kwamba yeye anafanya mambo makuu kuliko Yesu! Sababu yeye anatoa hela na misaada ya fedha na mitaji wakati Yesu hakutoa fedha wala mitaji. Waumini walishangilia na kuweka hela miguuni mwa mtume mkuu!
 
Kwani ulivyokuwa mkristo uliomba ushauri?
Kila mtu ana haki ya kuabudu dini anayoitaka hata ukiamua kuwa kwenye dini ya mashetani nenda tu.
Mna dini zenu unajificha na kujifanya mkristo wakati ukweli siyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…