Mimi ni Mkristo mlokole, nimeanza kukosa Imani na ukristo nahisi Uislam ndiyo dini ya kweli

Ulikua Mkristo ukiwa unamfuta nani? Mchungaji au Kristo Yesu? Kama mchungaji una haki ila kama ni Yesu mwana wa Mungu aliyehai basi mfuatr barabara. Hana makandokando
Huko kanisa linapokwenda sio kwa ajili ya wakristo waenda kanisani kwa ajili ya wazazi, au wachungaji au kuabudu wasichokijua. Kanisa imevamiwa na mbwa mwitu wakali wenye ngozi za kondoo only wakristo ambao ni watu wazima kiroho ambao zimekula neno lisilo ghoshiwa wanaweza ku survive. Mungu atusaidie sana.
 
Ila mkibusu jiwe na kuvaa ka kanga bila chupi (waume kwa wake pamoja) sio fiesta 😂😂
mimi si mwislamu so, siwezi kuzungumzia hayo. mimi nazungumzia dhehebu langu ambalo linapotea limeondoka kwenye misingi yake. hata gospel haina tofauti na nyimbo za club. kama huelewi lugha utahisi ni nyimbo za akina marioo. na muda mwingine unaelewa lugha ila unahisi ni bongo fleva mpaka pale mtu labda unasikia kaimba goodluck gosbert ndipo unasema basi itakuwa gospel maana goodluck ni mpendwa lakini wimbo wote umekaa kibongo fleva.
Huo ndio ukweli hata tukiukana. Hebu tazama kipindi cha jpili cha church on fire, niambie ile ni ibada au ni tamasha la wasanii kama ilivyo fiesta?
 
mtanziko wako wa kifikra ni jambo la kawaida,muhimu fata moyo wako unavyokuongoza
 
Hao wasabato na mafunzo yenu ya yule mchungaji na mwalimu wenu mwanamama anayewafundisheni kwamba mwanaume hatakiwi kula wali?
Good thing kuhusu wasabato ni kulana kwenye Makambi tu.

Yule mama anayesema wanaume wa sile wali ni mpumbafu sijawahi kuona,kama ni suala la sex na kuzaana aende nchi za asia mashariki aone watu wanaokula wali wanavyo zaana kama panya.
 
Mkristo halisi ni mwanafunzi na mfuasi wa Bwana wetu YESU KRISTO na sio mfuasi wa WACHUNGAJI !!!

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Asiione Faziza Foxy.
 
Umeena vyema.
Kama anadhani kipimo cha Ukristo ni Mchungaji, au mwanadamu anapotea sana.
Mtume Paulo anaasa kuwa "Nifuate Mimi kama ninavyomfuata Kristo"
Kwenye Ukristo sijasikia wala kupata ushuhuda wowote unaotumia mapanga kuufuata. Ni Imani na kuamini kwako kunakokufanya mfuate Kristo.
Nu kweli mavazi Ni sehemu ya heshima na kujisitiri mahali popte. Lakini moyoni je?!
Wewe Ni miongoni mwa Mafarisayo wanafiki mnaopaka rangi makaburi kumbe ndani mmejaa mifupa.
Ila jiulize, dhamira ya moyo wako inakutuma Nini juu ya kumtafuta Mungu?
Kila la heri kwa safari yako ya upande ule. Huku mtu unahubiriwa, ukiamini unakaa, hutatishwa, hutashikiwa jamvia wala fimbo.
 
Hoja ni kuharibika kwa maadili ndani ya ukristo hoja sio ukristo niliupata wapi
 
Kinachozungumzwa hapa sio kristo ni ukristo kwamba ukristo unapotea kimaadili na utetezi wako hapa ni kristo Mimi nazungumzia ukristo
 
Hoja nadhani hujaielewi Sina tatizo na kristo ninaliona tatizo kwenye ukristo
 
Hama tu Kama umegundua hivyo au waweza kufungua kanisa lako linalofanana na Hilo la mwaka 80 au 90 huko ili wakengeufu wote waige mfano kutoka kwako.
Hahahaha
 
Kwani biblia inaposema ninyi ni chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu inamaanisha nini?
Kama wewe unahisi unaweza kumtafuta mungu mwenyewe bila kutegemea kanisa acha kusali umtafutie hata nyumbani kwako
 
Warudi kanisa mama,waliambiwa mkishaanza kujitenga mtaendelea mtajitenga
 
Nikushukuru kwanza kwa kulitambua Hilo. Ila nikushauru kitu kimoja kabla hujaamua kuhamia kwa waislamu. Chunguza vizuri dhehebu la waadventista wasabato utagundua kitu
Nimekuelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…