HOJA Mimi ni mwajiriwa Serikalini. Nilikopa, ila nimefeli malengo nahisi ninaenda kupotea

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hua nawashangaa sana watu wanaoishi kwa kulipwa mshahara kila mwezi iwe ni mshahara mdogo au mkubwa!!!

Mtu analalamika laki 4 haitoshi!!!!

Laki4 ya uhakika kila mwezi ipo!!!!

Haitoshi!!!!!!

Kaa sasa ujiulize watu wasio na ajira wala biashara za mtaji mkubwa wanaishije??

Wewe una laki4 kila mwezi unaona hazitoshi!!! Hata kama upo dar hiyo ni hela kubwa uwe umepanga au laa hyo ni hela kubwa.
 
Angalia mazingira yako maana yake watumishi wote mna shida tumia hio Kama fursa kopesha pesa watumishi wenzio kwa riba ya 10% =800,000 kwa mwezi
Save 500,000

Uje mwakan tena na mrejesho

NB:epuka pombe za stress & mrudishe mkeo mtunze apendeze
 
Ulevi nilikuwa nakunywa nikaacha mimi nina pombe sijaiendekeza ila kwa sasa ndo nimezidisha japo kuacha ninaweza ninashukuru Mungu ananipa Hekima ya kuweza kuacha addicted yoyote ila kinachoniumiza kichwa mke wangu ni mpuuzi sana amekuwa kama mzigo
Usimuite mpuuzi mkuu. Huyo ni chaguo lako, mnaendana. Uliona anafaa ukamuoa. Nenda naye taratibu, nobody is perfect.
 
Wewe ni mzembe wajibika acha kutoa visingizio

Hela ya pombe unayo ila kulipa madeni hunq

Ushauri. Ili uwe na maisha ya amani maliza madeni

Ungefany biashara iendayo kipato chako

Acha kukopa
 
Saws huu wa sasa kuna mtu hana madeni?
kua na Akiba ya maneno kuna kesho
Madeni yawe na msingu unakopa u afanya nini?
Madeni yako unavyokopa hujamaliza nyuma yamekusaidia nini ndugu?

Acha kukopa maliza madeni figure out namna ya kufanya jambo kupitia mshahara ulionao

Ukiona una hela ya kuwa mlevi uko stressed vibaya alafu unataka kuingiq kwenye mikopo unaend kukimbiwa na mke
 
Leo nimekaa nimeona nikope kama million 8 nijilipue tena kwenye biashara.
Ni biashara gani?
Una nafasi ya kusimamia?
Wala sio mwalimu.

Kazi ninayofanya inanipa posho pia mkuu.
Kumbe kuna ziada afu unalialia?

Kwenye kipindi cha mpito (miaka 4):-
Acha pombe,
Acha (au pumzisha) michepuko yote,
Usiongeze mtoto..
 
Umeshafeli vibaya sana ndugu Kitendo cha kujiingiza kwenye mikopo ya chuma ulete yanye riba kubwa kila mwezi ndio umejichimbia kaburi.
Ila Naomba sana usacrifice mshahara wa mwezi mmoja ulipe hiyo mikopo ya chuma ulete yote . Ukimaliza Panga bajeti yako kulingana na hiyo take home ya Laki 4.
Narudia Tena Mikopo ya Chuma ulete Itakupoteza kabisa.
 
Pole sana kiongozi
 
Sahihi
 
Laki ngapi?
 
Kwahiyo ukaona umtengenezee thread mkeo humu.Kuwa na kifua mkuu mbona watu mnapenda kuwazalilisha wenza wenu.
 
Wapi nimesema laki 7 nyingi
MKuu sio kwa ubaya nadhani lengo lako upate ushauri sasa mimi nilichogundua wewe sio mlevi kama ulivosema ila una utoto utoto, na kama kweli wewe ni mlevi basi umefika mbali sana sio rahisi kuacha. Ukiweza kuliona tatizo mwenyewe harafu ukawa unalipuuza hiyo ni hatari.Lakini pia hakuna sababu ya kutaja take home yako sema tu kuna kiasi fulani ndio nachukua na sio kutaja ivo maana humu kuna watu hiyo pesa kwao ni kubwa sana hao utawaaminisha vipi kuwa umefeli maisha?
 
Hata waliofanikiwa walishafeli mara nyingi tu
 
Kum
Kuingia kwenye ulevi ndio kosa la kwanza umelifanya na kufukuza mwanamke ndio kubwa umelifanya litakugharimu. Ungeendelea kuishi na mwanamke kwanza huku unaendelea kujipanga polepole. Maisha sio ya kuyakatia tamaa hivo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…