Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

Kwa nini unakuja kwa mtu kama hujaweza kujithibitisha wewe upo?
Sema wewe kwamba mtu ni nani au ni nini ndipo ili tujue tunaanzaje kuthibitisha kulingana na vigezo utakavyosema maana umeipuuzia tafsiri yangu na uthibitisho wangu.

Kiranga tunatofautiana kitu kimoja tu. Ni kwamba mimi kwangu wazo ni 'kitu halisi' kabisa ila kwako sina hakika kama unaamini hivyo.

Maana mimi nilipojithibitisha kwa kusema kuwa nilipogundua ninawaza kuwa mimi ni nani nikagundua kuwa mimi nipo maana mtu ni wazo hai.

Uthibitisho wake ni kule kuwepo kwa hilo wazo hai linalowaza hayo yote. Wazo ni 'kitu halisi' kwangu. Kama ambavyo wewe unasema hili ni gari, huyu ni panzi. Na mimi hivyohivyo ninasema mtu ni lile wazo la yeye.

Tena hata tunaposema kitu halisi inaonesha tu upungufu wa lugha inayojitosheleza ya kuelezea vitu visivyoshikika. Mimi kwangu kitu kiwe kinashikika, kiwe hakishikiki ikiwa kinaonesha athari kwa maisha na vitu hicho ni kitu halisi kabisa
 
Kuna kitu unasahau au unakikwepa makusudi. Tatizo la kuinvoke idea ya mungu unaleta maswali yasiyo na majibu au maelezo yenye mantiki. Nasema huyo mungu umemuibua tu (invoke) kwa sababu hakuna ushahidi au mfano halisi wa nafasi yake dunian na ulimwenguni. Mawazo ya umungu yana uhalali mmoja tu unaoelezeka na kueleweka. Yametokana na sisi binadamu. Kwa vile sisi binadamu tunaweza kuathiri Jamii zetu na mazingira kwa matendo yetu, dini na imani zinakuwa na indirect effect pasipokuwa na weledi au ukweli ndani yake. Hapa unavyotandaza nadharia ya mungu ndio kuupa uhai imani hiyo. Lakini ukweli ndani yake hamna. Mawazo na dhana ya mungu yamekuwepo na itaendelea kuwepo kwa muda mwingi zaidi,japo kwa namna tofauti kulingana na vipindi vya muda. Watu wengi sana bado wanazichukulia kama zina ukweli kamili ndani yake.

Mababu zetu walilazimika kuamini hizo dini zilizokuja na vyombo vya majini kutoka uarabuni, ulaya na mashariki ya kati kulingana na hali ilivyokuwa. Walikuwa na imani zao kabla, kiukweli nazo pia haziponi kwenye kipimo cha kuhakiki uhalisia na ukweli ndani yake. Hali ya ukoloni, biashara na kutawaliwa ilikuwa ni lazima, kwa risasi, viboko au kupata elimu dini zililazimishwa kwenye makoo ya waliotawaliwa. Again it was an example of evolution. Kivipi? Walioakubali hali waliendelea na waliokataa na kupinga jumla walitoweka au vizazi vyao kubaki nyuma. Hawakuzikubali tu. Imani hazina ukweli ndani yake kwahiyo bila ushawishi hazina mtaji mwingine(kama ukweli au maana yoyote ya msingi). Hali ni tofauti kabisa na dhana za ukweli na zilizothibitishwa kisayansi. Huhitaji kuzipenda, kuelewa au kuzitungia nyimbo kuzipa uhai!

Imani potofu kama hizo za mungu zinadondoka zenyewe ukihoji tu, hazifiki mbali. Tunajua hadithi na maneno yake hayana ukweli. Tunajua hata kuomba mungu hakuna manufaa yoyote. Kinachobaki ni nini? Sielewi unataka nikwepeshe vipi huu ukweli ili tu kurefusha mada.
 
Unataka nikurupuke kwa mshangao au butwaa nione uwepo wa kitu kisichokuwepo? Yaani kwa vile kuna mpangilio fulani uliowezesha kuwepo vitu fulani nilipuke tu kusema lazima mungu amefanya hivi. Huoni kasoro kwenye mtiririko huo wa mawazo?

Unaandika vitu vya uongo. Eti vinavyoshikika tu! Unaweza kushika sauti au mwanga? Be serious.

Mambo ya kutungatunga ni kujidanganya. "And let there be light" seriously?

Ukifika ukomo wa uelewa sema tu sijui. Usianze kukumbatia imani na maandiko ya watu wa kale(ambao umewazidi sana ufahamu wa mambo mengi). Ni uongo mtupu!

Unaanzaje kuangalia dunia na ulimwengu halafu uhoji nani kaumba? Sio lazima kitu kiumbwe ili kiwepo, kinaweza kutokea tu. Mara kwann tuko hapa? Sio lazima kuwe na nia yoyote ya sisi kuwepo hapa. Tukifa tunaenda wap? Sio lazima kuwe na maisha baada ya kufa. Unaweza kuweka "hakuna ushahidi" kwenye 'sio lazima'.


Mtazamo wako unatia mashaka mwanabailojia.
 
Kutilia shaka ndio dini kama ingekuwa nayo ni dini. Hata hilo Jina la atheist linatia ukakasi. Niko skeptical about everything. Kama ningekuwa kiongozi wa hii dini gospel yangu ingekuwa "I don't know". Kila muumini yuko huru kudadisi kila kitu na kujifunza. Kila kitu kinaweza kupingwa au kujadiliwa. Demokrasia ya mawazo ndio amri pekee. Hatuchukui kauli au jambo na kumeza tu kama lilivyo!

Ni rahisi kuelewa taaluma za sayansi kwa sababu hazijinasibu kujua kila kitu. Kila kinachoelezwa ni kwa undani na kisichoelezeka kinawekwa wazi. Ni kawaida kukuta constants kwenye kanuni za kitaalamu. Kama kungekuwa na mtazamo wa imani na zikaruhusiwa kushamiri kungekuwa na miungu mingi maana kila constant ni kama unknown determining factor (a.k.a mungu, by your analogy). Sayansi zina lengo la kujifunza sio kukuelekeza, kukaririsha na kukupa ukweli wake mkuu kuu. Kila mtu anaweza kuchunguza na kufikia tamati kwa utaratibu. Kupingana sio haramu. Ruksa kurekebisha missteps. Sio mtu anaibuka tu na hoja isiyo na mashiko. Mwanasayansi lazima aelezee kafikiaje kauli yake.

Kama hauna doubt hata kidogo, basi amini hizo mambo mwanabaiolojia sio kesi.
 
Unaandika vitu vya uongo. Eti vinavyoshikika tu! Unaweza kushika sauti au mwanga? Be serious.

Mambo ya kutungatunga ni kujidanganya. "And let there be light" seriously?

Umemuelewa ndivyo sivyo, ameeleza vema kwenye paragraph yake ya mwisho, namnukuu "mimi kwangu kitu kiwe kinashikika, kiwe hakishikiki ikiwa kinaonyesha athari kwa maisha na vitu hicho ni kitu halisi kabisa". Kujua nini maana ya kitu halisi, rejea alipoeleza maana ya "wazo hai", kwa minajili hiyo hata hivyo ulivyovitaja kwake ni mawazo hai

Hakuishia hapo, akagusia na mapungufu ya lugha katika kuelezea baadhi ya vitu au hali fulani mfano: wazo hai na wazo mfu

Soma kuelewa na si kujibu au kutafuta dosari ambazo hazipo
 
Unaanzaje kuangalia dunia na ulimwengu halafu uhoji nani kaumba? Sio lazima kitu kiumbwe ili kiwepo, kinaweza kutokea tu

Haya hebu jaribu kutuelewesha kwamba "Jamii Forum" imetokea tu yenyewe haina muasisi?

Unaeleza kwa kukwepakwepa weee matokeo yake unapingana na ukweli wa dhahiri

Ila huenda si kosa lako, yawezekana hujui nadharia za kisayansi zinazozungumzia masuala haya
 
Mkuu kama hutaki kuamini kwamba jamii forum haiwezi Tu kutokea yenyewe bila muasisi

Pia utakataa ukiambiwa dunia imetokea tu yenyewe na haina muasisi,

Sasa swali linakuja, je kinachofanya tuamini kuwa Mungu ametokea Tu na hana muasisi ni nini? Kama yeye ameweza kutokea Tu bila kuwa na muasisi kwanini vingine ishindikane?
 
Wazo ni kitu halisi katika framework ya mawazo, lakini, kama unataka kuvuka daraja kwenye mto, ukasema hapa hapana daraja, na mimi nataka kuvuka mto, na wazo ni kitu halisi, hivyo nikiwaza daraja lipo, litakuwepo kwa uhalisi, halafu nitavuka mto, utazama mtoni.

Ukishaanza na "Mimi nilipo..." tayari ushafanya a priori argument kwamba wewe upo.

Eleza unavyoweza kuwaza bila kukubali kwamba wewe upo "a priori".
 
Mkuu kama hutaki kuamini kwamba jamii forum haiwezi Tu kutokea yenyewe bila muasisi

Pia utakataa ukiambiwa dunia imetokea tu yenyewe na haina muasisi

Tueleweshe kwamba "Jamii Forum" imetokea tu yenyewe pasina kuwa na muasisi au mechanism ya kuifanya ikawepo
 
Mkuu kama hutaki kuamini kwamba jamii forum haiwezi Tu kutokea yenyewe bila muasisi

Pia utakataa ukiambiwa dunia imetokea tu yenyewe na haina muasisi,

Nikushauri tu kwa wema, tafiti kwanza maoni/misimamo ya wanasayansi na wanafalsafa ambao ni atheists kuhusu nadharia za aina hiyo
 
Sasa swali linakuja, je kinachofanya tuamini kuwa Mungu ametokea Tu na hana muasisi ni nini? Kama yeye ameweza kutokea Tu bila kuwa na muasisi kwanini vingine ishindikane?

Wewe na nani mnayeamini kwamba Mungu ametokea tu? Changamoto ni lugha katika kulielezea au ufahamu 'uelewa'? yamkini hilo halipo hivyo, ila huo ufahamu unachangiwa na hayo mawili niliyoyataja

Jawabu: Ni kwa sababu Mungu hana sifa hiyo. Tangu lini Mungu akawa na sifa za vitu? Zisome sifa za Mungu kisha jifunze kutofautisha sifa zake na vitu
 
Sasa swali linakuja, je kinachofanya tuamini kuwa Mungu ametokea Tu na hana muasisi ni nini? Kama yeye ameweza kutokea Tu bila kuwa na muasisi kwanini vingine ishindikane?

Hivi tunavyosoma kwamba atoms ni indestructible "neither created nor destroyed" huwa ina maana gani? Naomba nifafanulie tafadhali

Kama kila kitu kimeundwa na atoms, kwa nini vitu vyenyewe havina hiyo sifa ya atom?
 
Ni nani ambae ametujuza sifa za Mungu? Ni Mungu mwenyewe alijiongelea au ni sifa ambazo anapewa na ambao hawana sifa za uungu?
 
Ni nani ambae ametujuza sifa za Mungu? Ni Mungu mwenyewe alijiongelea au ni sifa ambazo anapewa na ambao hawana sifa za uungu?
Mungu mwenyewe alijiongelea kupitia wajumbe - ufunuo 'wahy' 'mapokeo'

Na hata baadhi ya wasio na sifa za Uungu na wasioamini uwepo wa Mungu katika kueleza misingi/kanuni/sheria/nadharia mbalimbali wamejikuta wakieleza sifa zisiyemsadifu yeyote isipokuwa divine 'Elohim/Allah'
 
Unanishangaza: Hamna ulilojibu kati ya niliyouliza wala niliyohitajia ueleze, wakati huohuo unaniuliza na unategemea nikujibu

[emoji3544]
 
Nashkuru Kwa majibu yako mkuu, nilitaka kufahamu hayo Tu
 
Unajua taaluma ya sayansi asilia sio kama sayansi zingnine kama hayo mambo ya lugha. Alipoanza kwa kujitambulisha "Mimi mwanabaiolojia" hatuwezi kupokea kirahisirahisi hoja zisizona uhalisia kama hizo mawazo hai sijui mfu. Kwenye sayansi asilia ukianza mambo ya roho tayari umeharibu kwa sababu ni uzushi. Uzushi ni sumu ya ukweli kwenye tafiti yoyote ile.

Sijui unataka nimueleweje kuhusu nadharia ya roho wakati tunamtazama kama mwanabaiolojia.
 
Singularity au spontaneous generation?

Unamfahamu Richard Dawking? Unajua alisema nini kuhusu nadharia za aina hiyo [emoji23]
Prof Dawkins ana mtazamo wake kulingana na fani aliyobobea. Hapo nimejibu nikielemea kwenye nadharia ya nje kidogo na biology. Hasa physics. Kuna kitabu kilitoka miaka kadhaa cha Laurence Krauss... ndani amejaribu kidogo kuelezea kidogo jinsi kitu au hata ulimwengu ulitokea tu!

Unajua sio kila sehemu utaielewa kupitia kila tawi la sayansi asilia[emoji28]Sijui alisema nini Dawkins au pengine nimesahau. Tueleze tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…