Nikuweke wazi tu: una changamoto ya uelewa, unachagua kumuelewa mtu utakavyo na si alivyokusudia, nimesoma comment zako chache tu, hii ni mara ya pili unafanya hivi, ngoja nijaribu kueleza tena labda awamu hii utaelewa
JF kuwepo kumetokana/kumesababishwa na nini? Kuna kilicho nyuma ya uwepo wake "mfano: waasisi au imetokea tu kusikojulikana"? Haijalishi ni ya kwanza kuwepo, ya pili, ya mwisho au ya ngapi
Syntax za JF zilijitengeneza zenyewe? au yupo aliyezi-process akazi-execute ndo JF ikawepo? Jinsi JF inavyo-operate imetokea tu yenyewe? Hamna set ya commands wala codes ambazo ni instructions zilizo nyuma yake? Je hizo codes/commands zimetokea tu au zimeandaliwa?
Eti JF siyo unique, kutokuwa unique au kuwa unique ndo kumeifanya JF itokee au isitokee yenyewe? Halafu unathubutu kuandika 'swali halina mantiki', unafahamu nini kuhusu mantiki? Tuhamie huko?
Nimesoma nilicho-quote tu kimenitosha kukuelewa, hata ulichoandika chini yake sijasoma na sitasoma, kama utangulizi tu umejaa ufahamu mbovu hivi naamini huko chini hakuwezi kuwa salama