Mimi ni shabiki wa Fid Q lakini Joh Makini kashinda

Saad30

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2020
Posts
2,737
Reaction score
5,464
Fid Q namkubali sana kwa barz.

Leo baada ya kupiga mitungi nikasema nisikilize ngoma za Fid Q na Joh makini.

Lakini katika nyimbo zilizo nivutia katika mzuka ni hizi hapa.

Fid Q wimbo walk it off
Joh makini nusu nusu.

Nikasikiliza midundo inafanana kimzuka.

Lakini katika barz asee niseme ukweli tu kutoka akilini..

Joh makini wimbo wake nusu nusu umefunika.

Mzee mbuzi fareed Kubanda umekimbizwa.
 
Farid?

Tunakusubiri mitungi iishe. πŸ˜‚
Ukilinganisha ngoma moja moja kama hivyo mbona unakosea saana.

Fid muacheni kama alivyo.

Mwanza mwanza
Professional
August 13.
Neno πŸŒ‹
Ielewe mitaa πŸŒ‹
Fid. Com

Kwa uchache tu humo joh azaliwe upya ndio anaweza kujaribu kufanya kilichofanyika humo.
 
Skia mkuu fid Q nikwambie kitu moja tu.

Fid Q ngoma zote za saisa kamaliza kwenye ngoma yake na juma nature

Fid Q ft juma nature Siri ya mchezo.

Kwenye hiyo track hakuna Roma wala ney wa mitego.

Mimi ni shabiki wa fareed Kubanda kinoma.

Lakini nusu nusu amefunikwa na ile wimbo wake wa walk it off ft tazz
 
Ongezea Neno,Fresh,Ni hayo tu.
 
Joh makini kweli man? Kweli kuna muda ni wakuheshimu mitazamo ya wengine..
 
Umenikera Sana kusema ni shabiki wa Fid Q... Nimeumia Sana Kwa hizi dharau ulizofanya.... Bora ungesema humpendi fid ningekuelewa kidogo...

Tukirudi kwenye hizo Ngoma mbili ya Nusu Nusu ya Joh Makini na walk it off ya fid Q ambazo ulizisikiluza ukiwa "umelewa" .. ni aibu kusema eti fid kafunikwa kwenye barz...

Hizi hapa n baadhi ya lyrics zilizopo kwenye Ngoma ya fid walk it off.... Halafu naomba ulete lyrics Kali za kwenye nusu nusu zinazozidi hizi...

"Biashara hasara.. uko doro kimfuko/ Utasimama ka mnara ukiacha vituko/
Itakuacha imara kama mnyororo wa milupo/ Hakika giza totoro ndo ishara ya mapambazuko /..."

"AAH.. Nyumba ya njaa.. ukisizi unapata zero/
Dunia ya VICHAA, MWEHU ndo CHIZI pia ni HERO.."
 
Najua fid Q ni mkali kuliko Joh makini.

Hapo nimeongelea katika hizo ngoma mbili sababu midundo ni ya kubang

Walk it off Fid Q na nusu nusu Joh makini

Hapa ni nyimbo mbili tu ambazo tunaziongelea.
 
Mkuu Nusu Nusu ni kali acha ushabiki wa hivyo.
 
Yaani jamaa kanikera Sana Bora hata angeitaja Ngoma ya "niaje nivipi" lakini "nusu nusu" ni kumdisrespect fid
Sasa kwenye niaje ni vipi sio mdundo wa kubang mkuu elewa hilo
 
Mimi skusema nani mkali mkuu hapo tunazungumzia nyimbo mbili tu.

Walk it off na Nusu Nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…