Miradi yote mikubwa iliyoanzishwa kwa pupa na Hayati Magufuli sioni hata mmoja utakaokuwa na ufanisi

Miradi yote mikubwa iliyoanzishwa kwa pupa na Hayati Magufuli sioni hata mmoja utakaokuwa na ufanisi

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,283
Reaction score
9,925
1. Bwawa la Nyerere, ndiyo hilo lililojengwa bila kangalia madhara yake kwenye mazingira. Matokeo yake mtambo mmoja tu uliowashwa kwa wiki 2 tu umeleta mafuriko ya kutisha, na Sasa umezimwa. Failure asubuhi na mapema.

2. Madege:-
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG iliyotolewa karibuni madege haya yametuingizia hasara ya mabilioni kama inavyoonekana hapa:-

Screenshot_20240404-120936.png

3. SGR: Hii ndiyo pasua kichwa kweli kweli. Imesababisha hasara ya mabilioni ya shilingi kama inavyoonekana hapo namba 2. Mpk sasa kipande cha Dar -Moro kinashindwa kuanza kufanya kazi kwasabb zifuatazo:-
a. Vichwa vilivyoletwa ni chakavu.
b. Spidi ya treni ni 160kmph, na umbali toka Dar mpk Moro ni km 300. Sasa kwa speed hiyo, treni ikienda bila kusimama itatumia saa 1 na dak 52 (sawa na masaa 2). Lkn kwa kuwa itakuwa inapakia na kushusha itatumia masaa 3 na kitu.

Sasa nani atapanda hiyo treni ? Ufanisi wake uko wapi?

4. Ujenzi wa makao makuu Dodoma.

Hivi Kuna kipya kimeongezeka ktk utoaji wa huduma kwa wananchi baada ya makao makuu kuhamia Dodoma. Faida gani imepatikana ambayo tungeikosa kama makao makuu yangerndelea kuwa Dar?. Ni uendawazimu tu.

Acha niishie hapa, msinichoshe mie!
 
Kuweni makini na matumizi yenu ya akili.

Mama yenu alikuwa na nafasi ya kukataa kila kitu kwakuwa aliowateua walipinga miradi yote tangu enzi za Chuma.

Mnataka tutoe maoni yetu ya kweli kabla hamjasajili vikundi?
 
Ununuzi wa ndege na kuhamia Dodoma ndiye miradi isiyokuwa na tija, SGR na bwawa la Nyerere ni miradi mizuri kama ingefanywa kwa utaratibu mzuri na ikapata watu sahihi wa ikasimamiwa vyema.
 
Ununuzi wa ndege na kuhamia Dodoma ndiye miradi isiyokuwa na tija, SGR na bwawa la Nyerere ni miradi mizuri kama ingefanywa kwa utaratibu mzuri na ikapata watu sahihi wa ikasimamiwa vyema.
ununuzi wa ndege alichemka sana JPM. kuhamia Dom namuunga mkono.
sgr na bwawa ni makusudi ya upigaji awamu hii ndio wameleta upumbavu ktk hiyo miradi 2.
 
kila lenye mwanzo lin mwisho wake jiwe alizingua ila miyeyusho inaendelea na itaendelea mpka tanzania iwe nchi maskini yenye miundombinu mibovu na watawala wenye maisha mazuri.....

mwananchi akishabanwa sana atajua namna ya kujikomboa
 
Ndege hata mamako huyu nanunua! Moja imewasili juzi tu hapa.

Hiyo miradi itafeli sababu inaendeshwa na akili visoda!


Nitajie mradi mmoja tu wa selikali nje ya hii ya JPM unaoendeshwa kwa ufanisi?
 
Kwa hasara izo hapo juu bila kukopa unadhani tutatoboa
Mmesha jipromote, sasa mmeanza tena.

Utawala huu umefanya kitu gani chenye Ufanisi?

Kuangamiza Wamasai?

Kuuza Bandari?

Kukopa matrilioni ya fedha?


Teua Tengua?
hasara
 
Back
Top Bottom