Mirathi ya nyumba iliyojengwa na mjane yazua balaa; ukoo wa mume na ukoo wa mke wanaigombania

Mirathi ya nyumba iliyojengwa na mjane yazua balaa; ukoo wa mume na ukoo wa mke wanaigombania

Kigezo kilichofanya akazikwa mahali Fulani ndio vigezo hivyohivyo vitakavyowapa umiliki hao wanaomiliki eneo Kaburi lake lilipo.

Unasema huoni mantiki, hujiulizi Kwa nini alizikwa Huko?
🤣🤣🤣Wachaga kwa kuteteana !! Utapeli mtaacha Lin?
 
Haki wanayo upande wa mke, kisheria mume akifariki warithi ni watoto , mke na wazazi wake kama wapo.

Hao wachaga ndugu yao kafa na mali zake zimerithiwa na mke wake pamoja na watoto .

Jiulize kama huyo mama angeolewa tena akazaa watoto wengine hao ndugu wa mume wangekuja hapo kufanya nini?

Hizo mali za huyo mama warithi ni ndugu zake hakuna kesi hapo hata wakienda mahakamani.
 
Wanadai Mtu kuolewa maana yake ni kuhamishwa ukoo.

Ile mahari waliyopokea maana yake ni mwanamke anahama ukoo wake na kuhamia ukoo wa mume.

Ndio maana hata mwili wake wameenda kuuzika moshi alipozikwa mume wake na mwanae.

Sasa kama mwili wake umzikwa kwenye makaburi ya ukoo wao. Na hata mali zake zisimamiwe na ukoo huo huo uliomzika
Hapana.
Hayo unayoeleza yangeliswihi iwapo mke angelitangulia kufariki.

Lakini baada ya mume kutangulia ikawa ndoa imevunjwa na Mungu na talaka ikawa kapewa na dunia.

Tuchukulie mfano wangelikuwa wazima, mwanamke akapewa talaka, baada ya mwanaume kufariki, je hao ndugu wa mume wangelikuwa na haki ya kufuatilia na kwenda kudai chochote toka kwa huyo mtalaka?

Tuanzie hivyo!
 
Hio uliyoquote inaongelea uhalali wa kuzikwa ukweni na sio uhalali wa ndugu wa mume kurithi mali. Mali iliyoachwa ni ya MKE ndie aliyeiendeleza mpaka ikafikia hapo. Ndugu wa Mume wanaendeshwa na tamaa tu
Hakuna uhalali. Nadhiri ya ndoa ya kikristo inasema mpaka kifo kitakapowatenga. Hivyo mojawapo anapofariki na mirathi yake ikakamilishwa, anayebaki ni single na mali zake zinawahusu watoto au ndugu zake wa karibu. Je angeolewa halafu ndo amefariki mume wake mpya si angerithi hizo mali? Huu ndio uelewa wangu.
 
Habari wadau.

Kama mnavyojua swala la mirathi linavyotolewa macho hapa Tanzania.

Jirani kwetu kuna mama amefariki na kuacha nyumba nzuri tu na hajaacha mtoto hata mmoja.

Historia ya huyu mama ( kabila mpogoro) mwaka 1991 aliolewa kwa ndoa ya kanisani na mume wake ( kabila mchaga)

Baada ya kufunga ndoa walinunua kiwanja na mume wake na kuzaa mtoto mmoja wa kiume.

Mwaka 1994 mume wa huyu mama alifariki na kumuacha mke na mtoto mmoja wakiwa hai.

Taratibu za mirathi ya mume wake zilifanyika baada ya msiba. Mama na huyo mwanae wakapewa hiko kiwanja maeneo ya tegeta kikiwa kitupu hakijaanzwa ujenzi wowote.

Maisha yakaendelea. Mama huyu hakuolewa tena . Aliendelea kuishi na mwanae kwa kupanga nyumba ya NHC keko. Na mdogo mdogo akaanza ujenzi wa nyumba katika kiwanja walichoachiwa na mumewe.

Alijenga nyumba nzuri tu ya kisasa. Na zingine ndogo ndogo pembeni za kupangisha. Maana kiwanja kilikuwa kikubwa sana ( maana enzi wananunua tegeta ilikuwa pori ardhi haina thamani miaka ya 90 muuzaji anakuuzia bonge la kiwanja kwa bei ndogoo..)

Baada ya kumaliza ujenzi yeye na mwanae waliendelea kuishi nyumba ya NHC na kule tegeta walipojenga wakapangisha wapangaji kadhaa.

Mwaka 2015 mama alipata msiba mwingine wa kufiwa na mtoto wake huyo mmoja kwa ajali ya gari na hii ikamfanya mama kubaki peke yake bila mtoto wala mume.

Mama akaendelea kuishi mwenyewe mpaka na yeye mama alipofariki mwaka huu mwanzoni.

Mwili wa mama ulisafirishwa kwenda moshi kuzikwa walipozikwa mume wake na mwanae.

Shida imekuja kwenye nyumba zilizojengwa na huyo mama. Ukoo wa mume unasema ni mali zao. Na ukoo wa mke nao unasema ni mali zao maana zimejengwa kipindi mume wa huyo mama ameshafariki.

Wataalamu wa mirathi Kesi kama hii upande upi kati ya ukoo wa mume na ukoo wa mume una haki ya kurithi hizo mali za huyu mama.

Wazazi wa huyu mama wote wameshafariki pia.

Upande wa huyo mama wanazingua. Mke kama aliolewa na mahari ilishatolewa, baada ya kufiwa na mumewe hakuolewa maana yake ni kwamba kila kitu hapo ni halali ya ukoo wa mume.

Hao wapogoro waache ujinga.
 
Kuzaa watoto wengi kuna umuhimu; busara itumike tu, wakae kikao pande zote mbili na wafikie maamuzi, ya kuuza au kupangisha na kugawana kilichopo
 
Hakuna uhalali. Nadhiri ya ndoa ya kikristo inasema mpaka kifo kitakapowatenga. Hivyo mojawapo anapofariki na mirathi yake ikakamilishwa, anayebaki ni single na mali zake zinawahusu watoto au ndugu zake wa karibu. Je angeolewa halafu ndo amefariki mume wake mpya si angerithi hizo mali? Huu ndio uelewa wangu.
Upo sahihi kabisa.
 
🤣🤣🤣Wachaga kwa kuteteana !! Utapeli mtaacha Lin?

Sio Utapeli.
Kama MKE kazikwa upande wa mume, tafsiri yake bado ni Mali ya Ukoo wa mumewe.

Kama Ndoa ilivunjika au ilivunjwa, sio sababu ya kuzika MKE upande wa mumewe.

Hao Ndugu wa Mke ndio wanashida.
Sema ni vile Watu hawaelewi haya Mambo.
Mwanamke akishaolewa anakuwa hayupo Chini ya umiliki WA ukoo wake tena, anaenda kwenye umiliki wa ukoo WA mwanaume.

Ni vile kizazi cha sasa kimeshavurugwa
 
Wanadai Mtu kuolewa maana yake ni kuhamishwa ukoo.

Ile mahari waliyopokea maana yake ni mwanamke anahama ukoo wake na kuhamia ukoo wa mume.

Ndio maana hata mwili wake wameenda kuuzika moshi alipozikwa mume wake na mwanae.

Sasa kama mwili wake umzikwa kwenye makaburi ya ukoo wao. Na hata mali zake zisimamiwe na ukoo huo huo uliomzika
Hakuna Sheria kama hiyo. Nchi hii inaongozwa na Sheria ya ndoa.
Ila kama Kuna mkataba mliandikiana, ndiyo law of contract ita-supersede.
Kuhusu mirathi Kuna Sheria ya mirathi na hapo heirs wa mjane ni kaka na dada au baba na mama kama bado wapo.
Kaka/dada aombe usimamizi wa mirathi kwa kuteuliwa na ndugu zake.
Atakaejitokeza kupinga aende mahakamani.
 
Hakuna uhalali. Nadhiri ya ndoa ya kikristo inasema mpaka kifo kitakapowatenga. Hivyo mojawapo anapofariki na mirathi yake ikakamilishwa, anayebaki ni single na mali zake zinawahusu watoto au ndugu zake wa karibu. Je angeolewa halafu ndo amefariki mume wake mpya si angerithi hizo mali? Huu ndio uelewa wangu.

Uelewa wako ungepaswa uanzie kwenye hoja ya Kwa nini huyo mjane hakuzikwa kwao badala yake akazikwa upande wa mumewe.

Hapo ndipo uanzie
 
Ungejaribu kufafanua kidogo utata uliopo hapo, kumbuka hao wote ni "third parties"

Kama issue ni mahari nafikiri alielipa ni mume, ambaye ni marehem pia.

Wewe ukioa, Kati yako na MKE wako Nani anahamia ukoo WA Mwenzake?
Unafikiri ni Kwa nini mum akifa hazikwi Upande wa Mkewe, lakini MKE akifa huzikwa upande wa mumewe?

Maana kizazi cha sasa kinatabia ya kujizima Data.
 
Kama wazazi wa mke na mume wapo ndio watakaorithi kwa kugawana hizo mali….na kama hawapo basi kaka dada wa marehemu watagawana hizo mali na kama hawapo pia watagawana watoto wa ndugu kwa ratio sawa.
 
Sio Utapeli.
Kama MKE kazikwa upande wa mume, tafsiri yake bado ni Mali ya Ukoo wa mumewe.

Kama Ndoa ilivunjika au ilivunjwa, sio sababu ya kuzika MKE upande wa mumewe.

Hao Ndugu wa Mke ndio wanashida.
Sema ni vile Watu hawaelewi haya Mambo.
Mwanamke akishaolewa anakuwa hayupo Chini ya umiliki WA ukoo wake tena, anaenda kwenye umiliki wa ukoo WA mwanaume.

Ni vile kizazi cha sasa kimeshavurugwa
Hakuna kitu kama icho ...Ndoa inatenganishwa na kifo hamna Tena ndo hapo.

Nyi ni matapeli hakuna asiye tambua kila siku nyie tu kwani mkiacha izo Mali mtakufa? Eti kaacha kiwanja mnataka nyumba zote
 
Hakuna kitu kama icho ...Ndoa inatenganishwa na kifo hamna Tena ndo hapo.

Nyi ni matapeli hakuna asiye tambua kila siku nyie tu kwani mkiacha izo Mali mtakufa? Eti kaacha kiwanja mnataka nyumba zote

🤣🤣🤣
Acha hasira sasa Mkuu.
Wewe unasema ndoa imekufa alafu muda huohuo mjane kazikwa alipozikwa mumewe na mtoto wao Huko Moshi.

Huoni ninyi ndio matapeli?
 
Hakuna kitu kama icho ...Ndoa inatenganishwa na kifo hamna Tena ndo hapo.

🤣🤣🤣
Acha hasira sasa Mkuu.
Wewe unasema ndoa imekufa alafu muda huohuo mjane kazikwa alipozikwa mumewe na mtoto wao Huko Moshi.

Huoni ninyi ndio matapeli?
Ndoa imekufa sio kila mpogolo wa morogora atazikwa huko.

Mbona huyo Tarimo wa juzi kazikwa mbeya yule aliyekufa Ukraine.

Huyu mliomzika bagamoyo mbona bado mnataka na Mali za marehemu na hamjamzikq huko Moshi?

Acheni utapeli mnauwana wenywe Vibinti vidogo vikatili ..huko machame wana sura za kijangili demu ana ngeu za uso kama jambazi .
 
Uelewa wako ungepaswa uanzie kwenye hoja ya Kwa nini huyo mjane hakuzikwa kwao badala yake akazikwa upande wa mumewe.

Hapo ndipo uanzie
Haijalishi kazikwa wapi. Ukweli ni kuwa alikuwa single na no longer wife wa late husband.
 
Kwa kuzikwa kwao mwanaume, kiwanja kilikuwa cha wote mke na mume, mume akafariki mama akakiendeleza,, hii mali wafaidika ni upande wa kiumeni
 
Back
Top Bottom