Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Watanganyika Wote Waandishi Wa Habari?
 
Basi baada ya Bashite mwana wa Kaisari kusikia habari kwamba kuna mtu kutoka mashariki ya mbali jina lake kimepewa kitongoji kimoja cha Galilaya basi haraka haraka akawatuma mafalisayo waende wakashuhudie kama ni kweli.Basi Mafalisayo wakaenda wakashuhudia na kurudi kwa mwana wa mfalme wakasujudu wakasema "Tumepata kuona kibao kimeandikwa VICTORIA CHUI"Ndipo akawauliza kwa gadhabu "Ni nani aliyefanya hivyo? Mimi nimekuwa mwana wa mfalme lakini jina langu halijapewa hata banda la mbwa wa Tiro na Sidoni(Manzese na Gomz)" Ndipo kuhani mmoja akamjibu. "Ni mzee wa baraza la hapa Galilaya ndo kafanya hivyo" basi Bashite akauliza tena. "Naweza kumteka na kumtesa kama yule kijana wa Kiroma ili naye apate shika adabu yake?" Ndipo wazee wa baraza wakamwambia "humuwezi mtu huyo maana anatumia vifungu vya sheria za wayahudi" basi Bashite akagadhabika na kuwaamuru mafalisayo wakaking'oe hicho kibao, nao kama walivyoagizwa wakaking'oa hukuwakijisifu "hakika tumemuweza bwana huyu(meya)" lakini cha ajabu mpaka mwana wa Mungu anarudi hicho kitongoji kikaendelea kuitwa jina la VICTORIA CHUI huku Daudi akiendelea kutafta kiki kwa pikipiki iliyoisha mafuta.(wivu wa Mwana wa mfalme 1;1_15)
 
Na jogoo akawika kwa mara ya tatu..Kiparangoto 21:5
 
Hahahaaaa umevunja mkuu nilihisi nasoma holy bible daah bila shaka umetokea galilaya mwana wa uzao wa wadanganyika
 
Aisee weye Mkuu utatuvunja mbavu kwa kucheka huku lol! Hahahahahahahaha

Ndipo makada wakajipiga vifua na kugalagala kwenye mavumbi kama chatu huku wakisema, "ewe Sizonje tuchukue utumwani milele"
Lumumba 4 : 5-13
 
"Muujiza Mkubwa Ulitendeka Katika Nchi Ya Bandari Ya Salama Ndipo Toashi Akakimbia Kwa Haraka Kubwa Mpaka Katika Hekalu La Mfalme, Kwa Hofu Akamwambia Ewe Mfalme Tazama Vichwa Vya Treni Vimeshushwa Bandarini Kutoka Mbinguni, Bila Kuchelewa Mfalme Akafuatana Pamoja Na Waandishi,Mafarisayo Na Masadukayo Walipofika Mfalme Akapaza Sauti Akisema Kwa Hakika Muujiza Huu Unathibitisha Kwamba Nchi Hii Bwana Ameichagua Kuwa Ya Viwanda" Miujiza 70:12-20
 
Tena amini nawaambieni yeye aliyepokea kwa mkono wa kulia atatoa kupitia tundu lolote.Na haya nimewaambieni mbele ili wakati atoapo muwe tayari kushuhudia.Naye aliyeko wodini asitoke hapo mpaka kesi yake iishe kusomwa. Mbagala 6:5.
Amini amini nawaambia ufalme wangu si wa mafisadi na wala rushwa bali nita hakikisha wanaishi kama mashetani
Fentifodi 2:1-7
 
 
Hahahahaaa Umetisha Mkuu Nimecheka Mpaka Majirani Wameamka
 
Sauti ikasikika ikisema sitakula unga wa maharage tena ona mali tulizo wapola washami zinarudi sisi tunajutia hapatakuwa shujaa tena wa kutuletea unga tutengeneze chapati (kazi kazi 8:4-6)
 
"Ndipo bwana yule akamwamuru mkolomije-'Inua fimbo yako juu', na bahari ikagawanyika mara mbili ili kuruhusu vichwa vya treni vipite mahali salama." Ugonjwa mpya 12:31,32
 
Kwa kuwa mwanasizonje alijipenda yeye na maisha yake ndipo alipoamua kumtuma muongoza kwata wa pekee ili kwa yoyote mdanganyika aaminiyee kuwa kule kibeat si salamaa ....ndipo mwanakwata huyo alipokumbuka kuwa wadanganyika wengi wanapotea kwa kukosa ujasiriii wa kumpinga sizonje..kibeat 9-12
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…