Watu ni walalamishi Sana,kuzidi siku moja tu tayari watu mshaanza kumtoa kasoro rais,Mimi mwenyewe ninaishi kwa kutegemea salary lakini simlaumu rais ,ni kawaida tu,tujifunze kuwa na vipato mbadala hii itatuondolea Hali za stress.mimi hapa hata Kama mshahara utachelewa siku kumi na tano mbele bado naweza ishi bila shida kwa sababu licha ya kuwa mtumishi bado Nina kazi nje ya utumishi ambayo nikiifanya siwezi kosa laki tatu kwa mwezi hapa lazima maisha yasonge.
Watumishi wenzangu tujitume tuache kukishi kwa kutegemea mshahara tutajikuta na tutaishia kuwa watu wa lawama tu.