Ila watu wa humu, aiseeee🙌🙌🙌🙌
Anyway, turejee uzi wangu huu
Habari wana Jf kwa ujumla. Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max. Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha. First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi...
Kiufupi wengi walikuwa pamoja nami katika kipindi kifupi kilichopita cha msoto wa kutafuta kazi na mengineyo.
Wapo walionisaidia kwa moyo mmoja (hawa nawashukuru sana sana)
Na wapo waliotaka mambo yao binafsi (Mungu awasamehe).
Kiufupi nimepata kazi baada ya kupita vizuri kwenye interview (sisemi kazi gani maana humu wachawi wa maendeleo mmejaa kibao)
Na kuhusu nyumba yangu, nimepata mtu ambaye kasema ataimalizia kwa gharama zake kisha atapanga ili kufidia gharama alizotumia kuimalizia, nimeona sawa na tumeandikishiana na sasa ameshaanza kuikamilisha.
Ninachotaka kuwaambia tu wana JF
Msikariri maisha na msijaribu hata siku moja kumkatisha mtu tamaa kwa hali aliyoipitia au anayoipitia.
Mungu ndiye agawaye na apokonyae riziki.
Mlinisimanga sana na kunipa kila aina ya matusi ila yote niliyapokea na kuyafanyia kazi ili kuona wapi panahitaji marekebisho.
Wanakwambia tumia dharau zao kujifunza zaidi ulipokosea...pia hawa nao nawashukuru kwani walinipa chachu ya kuendelea kupambana.
Na lingine la mwisho, nimempata mzee mwenzangu, na Mungu akijalia kheri mwezi wa 6 nafunga ndoa takatifu ya kikristo.
Na nilishamueleza maisha niliyopitia huko nyuma, hivo sitaki kukumbushwa.
Ila kikubwa ninachowaambia wanawake wenzangu MSIKATE TAMAA, Jf wapo watu wengi sana sana sana wenye mioyo ya huruma na upendo wa kusaidia wengine ila tu, huwezi kuwaona kwa macho mpaka upate shida.
Nimepata kazi
Nimepata mume
Na nyumba yangu inakamilishwa.
WAKATI WA MUNGU, NI WAKATI SAHIHI.
NITALISIFU JINA LAKE MILELE.
MHUBIRI 3:1
View attachment 3218096View attachment 3218095