Mission za Umoja wa Mataifa na Harakati za kulinda amani: Baraza la Ulinzi la UN kuwa kama Circus

Mission za Umoja wa Mataifa na Harakati za kulinda amani: Baraza la Ulinzi la UN kuwa kama Circus

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Tathmini ya kina ya mfumo wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (UN) inapofanyika katika maeneo yenye migogoro mikali duniani, sura halisi inayojitokeza sio ile ya alama ya tawi la mzeituni au kofia ya bluu inayowakilisha matumaini na uokozi.
rdctanzaniecasquesbleus_0.jpg

Badala yake, ukweli mchungu unaodhihirika ni kwamba Operesheni za Ulinzi wa Amani za UN (UN Peacekeeping Operations) zimekuwa muundo wa udanganyifu mkubwa wa kisiasa, huku Makao Makuu ya baraza la UN yaliyopo New York yakionekana kama kumbi za vituko kwa nchi zingine- sawa na kusema mbwa asiye na meno anayebweka bila kung'ata.
President Jakaya Kikwete handle flag to Leader of Tanzania Troops head to DRC.jpg

Hali hii inajidhihirisha wazi katika maeneo ya Afrika yaliyokumbwa na vita vya muda mrefu, kama vile Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo Ujumbe wa MONUSCO umehudumu kwa zaidi ya miongo miwili, ZAIDI YA MIAKA 20.
images - 2026-10-25T153809.073.jpeg

Licha ya uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa kimataifa na mabilioni ya dola zinazotumika kila mwaka, makundi ya waasi kama M23 na CODECO yameendelea kushambulia na kuua raia bila tatizo lolote. Raia wa DRC wameshuhudia jinsi vikosi vya kofia za bluu vinavyojifungia ndani ya kambi zao zilizojengwa kwa ngome imara (Company Operating Bases - COBs) huku vijiji vyao vikiteketezwa kwa moto.
images - 2026-10-25T153818.292.jpeg

Swali ambalo kila mwananchi wa kawaida anajiuliza ni: Lengo hasa la hizi mission ni nini ikiwa hauwezi kuwalinda raia wanaouawa mbele ya macho yao?
image1024x768 (1).jpg

Kihistoria na Kimfumo, ulinzi wa amani wa UN umegawanyika katika ngazi kuu tatu za kiutendaji: Ngazi ya Kimkakati (Strategic Level) ambayo hii ipo pale New York inayosimamiwa na Baraza la Usalama (UNSC) na Idara ya Operesheni za Amani (DPO); Ngazi ya Uendeshaji (Operational Level) kwenye nchi husika chini ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu (SRSG) na Kamanda wa Kikosi (Force Commander); na mwisho ni Ngazi ya Mbinu (Tactical Level) kule mtaani ambapo makomando na vikosi vya miguu vinapiga doria.
Untitled-picture-8.png

Hata hivyo, kuna urasimu na ukiritiba uliokithiri kati ya ngazi hizi tatu ambao umekwenda kuunda mnyororo wa amri wa ajabu wenye ukiritimba sana. Wakati raia wakishambuliwa, Kamanda wa Uwanja wa Vita (Sector Commander) lazima aombe kibali New York kupitia mchakato mrefu wa kidiplomasia kabla ya kuruhusiwa kutumia risasi za moto ama nguvu ya ziada.
images - 2026-10-25T154120.962.jpeg

Mbaya zaidi ni uwepo wa mifumo inayoitwa "National Caveats" au miongozo ya kitaifa. Kila nchi inayochangia wanajeshi (Troop Contributing Country - TCC) kama vile Tanzania, basi hutoa masharti ya siri kwa wanajeshi wake ni kawaida kabsa.
images - 2026-10-25T154220.158.jpeg

Kwa mfano, India inaweza kukubali kutuma wanajeshi wake DRC lakini ikapiga marufuku kushiriki kwenye mapigano ya usiku au kuingia kwenye misitu minene, hili watu hawalifahamu ila ndio uhalisia. Matokeo yake, Kamanda Mkuu wa UN anakuwa na wanajeshi zaidi ya elfu kumi machoni pake, lakini pindi dharura inapotokea, anagundua kuwa nusu ya wanajeshi hao wamekatazwa na serikali zao za nyumbani kuingia uwanja wa vita moja kwa moja.
images - 2026-10-25T154539.598.jpeg

Hii ndiyo sababu mission kama MINUSMA nchini Mali na MINUSCA nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati zilishindwa kuzuia mapinduzi na hata zilishindwa pia kuzima makundi ya kigaidi, na hatimaye serikali za nchi hizo zikalazimika kuzipiga ban au kutaka ziondoke kwa sababu ya kutokuwa na msaada wala manufaa yoyote yale.
image1024x768 (1).jpg

Tofauti ya kikanuni kati ya "Peacekeeping" (Ulinzi wa Amani) na "Peace Enforcement" (Ushurutishaji wa Amani) pia imekuwa kichaka cha kujifichia, hizi ni dhana mbili tofauti kabsa.
images - 2026-10-25T153818.292.jpeg

Mfumo wa zamani wa sura ya sita ya Mkataba wa UN (Chapter VI) ulitaka pande zote zinazopigana zikubali uwepo wa UN na kuwe na hali ya kulindwa. Lakini katika maeneo ya vita kama Kivu Kaskazini ama Sudan Kusini (UNMISS), hakuna amani wala haki yoyote ya kulinda. Ili kukabiliana na changamoto hii, UN ililazimika kuunda Kikosi Maalum cha Kuingilia Kati cha FIB (Force Intervention Brigade) chini ya mission ya MONUSCO kikijumuisha wanajeshi shupavu kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Pamoja na Malawi chini ya sura ya saba yaani Chapter VII.
rdctanzaniecasquesbleus_0.jpg

Ingawa FIB ilionyesha uwezo mkubwa na kuwashinda waasi wa M23 mwaka 2013, uwezo huo ulidhoofishwa baadaye na uingiliaji wa kisiasa kutoka New York na migogoro ya kisiasa, na kuirudisha mission nzima kwenye hali ya kupooza na kukosa nguvu kabsa.
President Jakaya Kikwete handle flag to Leader of Tanzania Troops head to DRC.jpg

Kwenye hii mbanga unawazungumzia majitu ya miramba minne, kulikuwa na mwamba anaitwa Lieutenant General Babacar Gaye kutoka Senegal ambaye alikuwa Force Commander kuanzia 2005 mpaka 2010 na ndiye aliyehusika na mission kubadilishwa kutoka mission ya MONUC kuwa MONUSCO.
9363633167_a9de33d2b8.jpg

Lakini kulikuwa na njemba moja, kidume cha shoka Lieutenant General Derrick Mgwebi kutoka Jeshi la Afrika Kusini ama South African National Defence Force, huyu alikuwa kamanda mkuu wa MONUSCO kuanzia mwaka 2015 mpaka 2018, huku akihusika na kuwanyoosha waasi waliokuwa maeneo ya Kivu Kusini na Kaskazini pamoja na maeneo ya Ituri.
5660504056_8dfb7c2298_b.jpg

Tanzania tuliwahi kuwapoteza mashujaa wetu Private Rajabu Mlimo alipoteza Maisha kwneye shambulizi la waasi wa M23, Private Khatibu Shaaban Mwasimbi alipoteza Maisha pale Kivu Kaskazini, Corporal Maselino P. Msekwa, Private Paschal P. Kitalima, Corporal Ramadhani A. Mwangalaba, Private Abdallah A. Mchimbi, Private Said J. Kakolanya, Pamoja na Private Joseph P. Loishiye, yaani tulipoteza mashujaa sita kwenye Shambulio la Semuliki lilitokea tarehe 7 Desemba 2017 katika eneo la Beni, Jimbo la Kivu Kaskazini (DRC), shambulio ambalo lilitekelezwa na kundi la ADF (Allied Democratic Forces).

Jenerali Roméo Dallaire kutoka Canada, aliyekuwa Kamanda wa Vikosi vya UN nchini Rwanda (UNAMIR) wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, aliandika kitabu chake maarufu cha "Shake Hands with the Devil". Sasa Jenerali Dallaire anakwambia kwa uchungu jinsi alivyopiga simu mjini New York kuomba kibali na zana za kuzuia mauaji ya watu zaidi ya 800,000, lakini Baraza la Usalama likamwamuru apunguze idadi ya wanajeshi na asiingilie kati.
Untitled-picture-8.png

Madeleine Albright Kutoka Marekani ambaye alikuwa ni chawa kindakindaki wa Uongozi wa Bwana Clinton, pia kulikuwa na kizee kimoja kwa jina la Sir David Hannay kutoka Uingereza ambaye ndio alikuwa mjumbe wa kwanza kuweka wazi kuwa Umoja wa Mataifa wapunguze hizi harakati za kulinda amani. Jean-Bernard Mérimée wa Ufaransa, Yuli Vorontsov wa Urusi, Li Zhaoxing wa China), yaani akili za watu watano zikashindwa kuelewa kuwa Rwanda kinakwenda kuumana ile mbaya.
rdctanzaniecasquesbleus_0.jpg

Baraza la Usalama lilipigwa kitu kizito sana kiasi kwamba walibadilisha maraisi wanne ndani ya mwaka mmoja, Colin Keating (New Zealand), baadaye akaingia Ibrahim Gambari (Nigeria) ambaye huyu ndio aliwachana makavu super powers kuwa wana mambo ya KIS****E.
images - 2026-10-25T153818.292.jpeg

Mwezi wa sita Balozi Salim Bin Mohammed Al-Kussaiby, mwakilishi kutoka nchi ya Oman, kisha mwezi Julai wakamuweka Jamsheed Marker kutoka Pakistani, kiufupi ndani ya miezi minne Baraza lilipigwa kitu Kizito sana.
images - 2026-10-25T154539.598.jpeg

Kadhalika, aliyekuwa Balozi wa Marekani katika Baraza la Umoja wa Mataifa, Samantha Power, kwenye kitabu chake "A Problem from Hell: America and the Age of Genocide", anaonyesha jinsi mataifa makubwa yanavyotengeneza makusudi mission dhaifu za UN ili kutoa taswira ya uwongo kuwa wanatoa msaada, wakati halisi ni kwamba wanakimbia kuwajibika.
images - 2026-10-25T154220.158.jpeg

Ukitazama filamu kama "Quo Vadis, Aida?" ya mwaka 2020 inayoonyesha mauaji ya kimbari ya ,Srebrenica nchini Bosnia mwaka 1995, na makala ya "The Peacekeepers" (2005) iliyorekodiwa ndani ya mission za MONUC/MONUSCO nchini DRC Congo, Makala zote hizi mbili zinathibitisha ukweli mmoja: mfumo wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ni mfumo mmoja kubwa sana wa ukiritimba unaotumia mabilioni ya dola za walipa kodi duniani huku ikiwaacha raia wanyonge wakiteketezwa na mtutu wa bunduki na makundi ya waasi.

SEHEMU YA PILI INAFUATA.....
 
Back
Top Bottom