Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Pamoja na kutengeneza backyard yenye ubora wa kupumzika na kutafakari mambo yako ila maeneo ya wazi ya kiserikali ni muhimu sana sana. Sisi hatuna maeneo ya kukutana na kuongea, mkiwa na miadi lazima mkutane bar na sio kila mtu anapenda kwenda kuongelea bar.

Huwa nawaambia jamaa zangu, pale mbezi..front view ya Magufuli stand pangewekwa Park moja matata sana, pangependeza sana.
 
Me nasogeaga lerini au eneo lilikopita bomba la songas.
 
Huku mbeya tunaenda mitoni au milimani unakaa juu ya mawe ukiyafakari hili na lile, tunabadilisha tu vijiwe
 
Bar
 
Huku mbeya tunaenda mitoni au milimani unakaa juu ya mawe ukiyafakari hili na lile, tunabadilisha tu vijiwe
Hii changamoto ya kupata mahali pa kupumzika inawakumba wanaokaa miji mikubwa hasahasa Dar! Dar katika kipenyo cha hadi kilometer 20 unaweza ukakosa garden zaidi utaenda bar
 
Uk kwenye appartments nyingi lazma kuwe na park. Bongi yes. Nadhani maisha haayaruhusu sehemu kuachwa wazi haswa zenye watu wengi.
 
Hii kitu nilikua naongea na mtu Jana, Yani hata mazoezi vitu ambavyo ni vya muhimu serikali ilishashindwa kutenga maeneo, ukitaka kufanya jogging labda ufanyie barabarani bodaboda wakupapue
Maeneo yapo kwenye Shule ZOTE za Serikali kumetengwa eneo la wazi lenye kiwanja cha mpira HAPO km hakuna uzio unaweza kwenda kula POZI KIDOGO zamani nilikua naona wazee wanajazana kunywa kahawa na KUPIGA story za hapa na pale mida ya JIONI baada ya mpira kuisha wanakaa HAPO chini ya Mwembe wanabadirishana mawazo mawili matatu Ila Siku HIZI wale wazee siwaoni tena naona wengi tumeshawafukia hata Ile Miembe ilishakatwakatwa mingi kwa HIO eneo limekua la wazi zaidi siku hizi wanapaki bodaboda tu
 
👍💯umeongea point! Yaani sijui hii aibu kama jamii tuifiche wapi? Yaani kama una maongezi na mtu mpaka uende Bar! Huna sehemu nyingine ya kwenda! Open space au garden za ummma hakuna! Watu wa oysterbay, masaki, wanakwenda beach! Sisi wengine twende wapi?
 
Hata hivyo nyumbani ni nyumbani ningependa niende sehemu nyingine remote!
 
Hatari sana!
 
Naona wote Ni watu wa daslaam humu weng,Emu njooni Tanga mjionee garden ambazo unaweza ukatulia uka-enjoy upepo na kuwazua mambo yako.
Forodhani garden, garden ya mabanda ya papa,garden iliyopo taifa road mkabala na shule ya old Tanga, garden iliyopo Toyota,nenda jet -raskazone ufumweni Kuna makochi na upepo mwanana.
Tanga Raha, mji umepangika hatarii sidhani Kama Kuna mji unafikia Tanga kwa mpangilio.
 
Sasa hivi maeneo hayo ni either vijiwe vya mateja, au kuna mlinzi wa shule, au akina mama wanauza kachori na vyakula, n.k kwa ufupi sio sehemu rafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…