Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Kwa hiyo kila wakati ukitaka kutafakari utakuwa unaenda central park?

Jitahidi mnunue maeneo makubwa ndani ya backyard unaweza kuplan maeneo kama hayo ya kupumzika na kutafakari (backyard rest area)

Wakati fulani unaweka BBQ grill yako na vinywaji ukawa unafanya tafrija na familia au ndugu, jamaa na marafiki
Pamoja na kutengeneza backyard yenye ubora wa kupumzika na kutafakari mambo yako ila maeneo ya wazi ya kiserikali ni muhimu sana sana. Sisi hatuna maeneo ya kukutana na kuongea, mkiwa na miadi lazima mkutane bar na sio kila mtu anapenda kwenda kuongelea bar.

Huwa nawaambia jamaa zangu, pale mbezi..front view ya Magufuli stand pangewekwa Park moja matata sana, pangependeza sana.
 
Nimekaa mitaa mingi maeneo ya kipato cha kati na cha juu hata kufikia kupata kwangu. Changamoto nyingi niliyokumbana nayo ni wakati unatafuta sehemu ukakae peke yako ukatafakari hili na lile. Nyumbani wakati fulani panakuwa na miingiliano mingi ya wife, watoto, jamaa na marafiki au wewe kama baba wakati mwingine unawaachi space wajibinafasi (si unajua dingi akiwepo panakuwa na nidhamu ya woga).

Sasa Bwana nimekuja kuona wengi uishia Bar. Tatizo la Bar lazima uwe na hela ya kukalia siti ya eneo la biashara, hiki ni kipengere wakati mwingine hauko vizuri. Sehemu nyingine ni viwanja vya mipira ambapo hujaa wahuni na teenagers wanaoishi maisha yao panakuwa hapakufai.

Sehemu nyingine zinakuwa mbali na nyumbani ambapo utalazimika kutumia usafiri! Sasa kwa changamoto hii wanajamvi huwa mnafanyaje? Nadhani stress nyingi na maugonvi usababishwa na mtu kukosa mahali pa kupumua! Kwangu anagalau nina "Pub" ambayo sikosi mtu mpya wa kuchill naye kwa kupiga story nikiwa nimeboreka! Wewe huwa unafanyaje?
Me nasogeaga lerini au eneo lilikopita bomba la songas.
 
Huku mbeya tunaenda mitoni au milimani unakaa juu ya mawe ukiyafakari hili na lile, tunabadilisha tu vijiwe
 
Bar
 
Hii changamoto ya kupata mahali pa kupumzika inawakumba wanaokaa miji mikubwa hasahasa Dar! Dar katika kipenyo cha hadi kilometer 20 unaweza ukakosa garden zaidi utaenda bar
 
Uk kwenye appartments nyingi lazma kuwe na park. Bongi yes. Nadhani maisha haayaruhusu sehemu kuachwa wazi haswa zenye watu wengi.
 
Hii kitu nilikua naongea na mtu Jana, Yani hata mazoezi vitu ambavyo ni vya muhimu serikali ilishashindwa kutenga maeneo, ukitaka kufanya jogging labda ufanyie barabarani bodaboda wakupapue
Maeneo yapo kwenye Shule ZOTE za Serikali kumetengwa eneo la wazi lenye kiwanja cha mpira HAPO km hakuna uzio unaweza kwenda kula POZI KIDOGO zamani nilikua naona wazee wanajazana kunywa kahawa na KUPIGA story za hapa na pale mida ya JIONI baada ya mpira kuisha wanakaa HAPO chini ya Mwembe wanabadirishana mawazo mawili matatu Ila Siku HIZI wale wazee siwaoni tena naona wengi tumeshawafukia hata Ile Miembe ilishakatwakatwa mingi kwa HIO eneo limekua la wazi zaidi siku hizi wanapaki bodaboda tu
 
Pamoja na kutengeneza backyard yenye ubora wa kupumzika na kutafakari mambo yako ila maeneo ya wazi ya kiserikali ni muhimu sana sana. Sisi hatuna maeneo ya kukutana na kuongea, mkiwa na miadi lazima mkutane bar na sio kila mtu anapenda kwenda kuongelea bar.

Huwa nawaambia jamaa zangu, pale mbezi..front view ya Magufuli stand pangewekwa Park moja matata sana, pangependeza sana.
👍💯umeongea point! Yaani sijui hii aibu kama jamii tuifiche wapi? Yaani kama una maongezi na mtu mpaka uende Bar! Huna sehemu nyingine ya kwenda! Open space au garden za ummma hakuna! Watu wa oysterbay, masaki, wanakwenda beach! Sisi wengine twende wapi?
 
Kama una eneo kubwa basi haujalitumia kikamili kwa matumizi kama hayo. Waite watu wakupe plan.

Huko utaenda mara chache kumbuka familia yako inakuhitaji zaidi, sasa tena wewe unapata nafasi unaikimbia?

Au eneo umelimaliza kwa kujenga nyumba za wapangaji?
Hata hivyo nyumbani ni nyumbani ningependa niende sehemu nyingine remote!
 
Point mkuu hasa mkoa wa Dar uko ovyo sana.

Mm naishi mwananyamala kwa kopa yaani useme utoke home ukapunge japo upepo utaishia Bar au pale kiwanjani makaburini .

Mambo ya sehemu za kupumzikia utawapenda wazazibar Huwa hawana stress kabisa na hivi vitu maana Kuna sehemu nyingi sana iwe za private ama public unaenda unatulia zako fresh tu na hulipii hata senti ila kwa bongo serikali wakiona eneo liko wazi utafikir paka kaona samaki lazima amnyakue tu.
Hatari sana!
 
Naona wote Ni watu wa daslaam humu weng,Emu njooni Tanga mjionee garden ambazo unaweza ukatulia uka-enjoy upepo na kuwazua mambo yako.
Forodhani garden, garden ya mabanda ya papa,garden iliyopo taifa road mkabala na shule ya old Tanga, garden iliyopo Toyota,nenda jet -raskazone ufumweni Kuna makochi na upepo mwanana.
Tanga Raha, mji umepangika hatarii sidhani Kama Kuna mji unafikia Tanga kwa mpangilio.
 
Maeneo yapo kwenye Shule ZOTE za Serikali kumetengwa eneo la wazi lenye kiwanja cha mpira HAPO km hakuna uzio unaweza kwenda kula POZI KIDOGO zamani nilikua naona wazee wanajazana kunywa kahawa na KUPIGA story za hapa na pale mida ya JIONI baada ya mpira kuisha wanakaa HAPO chini ya Mwembe wanabadirishana mawazo mawili matatu Ila Siku HIZI wale wazee siwaoni tena naona wengi tumeshawafukia hata Ile Miembe ilishakatwakatwa mingi kwa HIO eneo limekua la wazi zaidi siku hizi wanapaki bodaboda tu
Sasa hivi maeneo hayo ni either vijiwe vya mateja, au kuna mlinzi wa shule, au akina mama wanauza kachori na vyakula, n.k kwa ufupi sio sehemu rafiki
 
Back
Top Bottom