Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Mitaa yetu mingi haina nafasi za wazi kwaajilli ya kupumzika. Huwa unaenda wapi kupunga upepo?

Asubuhi tuu hapa nilikuwa nawaza sehemu ya kwenda kwa ajili ya kukaa pekee yangu hata kwa saa 5 kwa siku nadhani kwa mwezi mzima 😔 mana kuna hali ngumu nnayoipitia kwa sasa hvy nahitaji kuwa pekee yangu.

Nnaishi Manzese sasa huku ni kivumbi, hapa itabidi mpaka niende coco beach.
 
Naona wote Ni watu wa daslaam humu weng,Emu njooni Tanga mjionee garden ambazo unaweza ukatulia uka-enjoy upepo na kuwazua mambo yako.
Forodhani garden, garden ya mabanda ya papa,garden iliyopo taifa road mkabala na shule ya old Tanga, garden iliyopo Toyota,nenda jet -raskazone ufumweni Kuna makochi na upepo mwanana.
Tanga Raha, mji umepangika hatarii sidhani Kama Kuna mji unafikia Tanga kwa mpangilio.
Ukiongea hivyo nasisi tutakwambia tuna mwambao wa beaches kwa wakazi O'bay, masaki, Mikocheni, kawe! Tunaongelea walio wengi kwenye viunga vya jiji!
 
Sisi hatuna maeneo ya kukutana na kuongea, mkiwa na miadi lazima mkutane bar na sio kila mtu anapenda kwenda kuongelea bar.
Kinachofanya mkutane bar ni ufinyu wa backyard. Ukiwa na eneo kubwa kama mna ishu ya kuongea ya maana hamhitaji kukutana bar. Unafikiri madon huwa wanakutana bar kupanga mbanga zao?
 
Asubuhi tuu hapa nilikuwa nawaza sehemu ya kwenda kwa ajili ya kukaa pekee yangu hata kwa saa 5 kwa siku nadhani kwa mwezi mzima 😔 mana kuna hali ngumu nnayoipitia kwa sasa hvy nahitaji kuwa pekee yangu.

Nnaishi Manzese sasa huku ni kivumbi, hapa itabidi mpaka niende coco beach.
😂😂😂😂! Ebu jaribu kuwaza mtu anayeishi manzese!
 
Sasa hivi maeneo hayo ni either vijiwe vya mateja, au kuna mlinzi wa shule, au akina mama wanauza kachori na vyakula, n.k kwa ufupi sio sehemu rafiki
Bodaboda wanapaki alafu kuna wale wana MAOMBI wanatumia uwanja kuendeshea maombezi yao ya ibada
 
Kinachofanya mkutane bar ni ufinyu wa backyard. Ukiwa na eneo kubwa kama mna ishu ya maana hamhitaji kukutana bar, backyard inatosha kabisa na kama kunywa mtakunywa na nyoma choma mtatengeneza
Mkuu! Nyumbani hata umeweka nini kunaboa! By the way! Sio kila mtu utamleta kwako ingawa unaweza kuwa maongezi muhimu naye! Hapo mpeleke bar hamna namna shehkhe!
 
Mkuu! Nyumbani hata umeweka nini kunaboa! By the way! Sio kila mtu utamleta kwako ingawa unaweza kuwa maongezi muhimu naye! Hapo mpeleke bar hamna namna shehkhe!
Sawa

Hivi kweli mna issue ya maana ya maongezi ndio mkazungumzie bar?

Hata kama sio nyumbani kuna maeneo mengine ya kufanya mazungumzo kama hayo
 
Park inatakiwa kuwa kwenye walking distance kutoka kila nyumba. Hivyo kila kata au mtaa inatakiwa kuwa na park. Uroho umefanya tusitenge na tupore maeneo hayo.

Kijiwe cha drafti ni mtoko mzuri sana
Sure! Lakini vijiwe vya draft kumejaa porojo na mizaa na matusi! Sio sehemu ya staha!
 
Hapa kimara Mida ya jioni, naenda pale darajani napata upepo kidogo
 
Sahv watu wanajenga sehemu za michezo nk lkn ndy unalipia
Wale watoto familia za wenzangu na mimi kwenda shuguli

Ova
 
Nakaa karibu na baharini, nikiona hovyo naenda ufukweni... Japo nina muda sasa sijaenda huko.
Ikiwa nyakati za jioni nachukua viatu vyangu naenda uwanjani kucheza mpira.
Huwa naenjoy mnoo kucheza na vijana, nikifika wananipokea kwa shangwe, naburudika, najisikia faraja kubwa mnoo.
Ongera yako huko karibu na ufukwe raha kama zoote! Ukitoka hapo stress zote zimeisha! Mtu huko kinyerezi au tabata utaenda wapi zaid ya bar?
 
Baadhi ya wapumbavu wamegawa na kuuza au kujigawia swhemu zote za mapumziko, unafikiri kulikuwa hakuna?
Sehemu zingine zilikuwa ni garden kabisa ila ndio hivyo tena
Maeneo ya shule zote kulikuwa na viwanja mpaka vya mipira tena kuanzia football, volleyball lakini leo hakuna tena
Wazee wengine wana laana sana
Hao ni wazee sasa waliotoa viwanja wakiwa serikalini
Wazungu enzi hizo kabla ya Uhuru waliweka maeneo makubwa kuanzia Shule, Mahospitali yote, magereza na polisi wote walikuwa na maeneo makubwa sana hata Makanisa na Misikiti

Leo wengi walioviuza wamekufa wametuachia mtihani huu
 
Huku mbeya tunaenda mitoni au milimani unakaa juu ya mawe ukiyafakari hili na lile, tunabadilisha tu vijiwe
Wakati niko mbeya block t,udogoni tukitaka kucheza tulikuwa tunaenda ndani ya eneo
La Monrovian mule kulikuwa na uwanja mpira

Ova
 
Back
Top Bottom