Mitandao ya kijamii siku hizi imekuwa chanzo kikubwa cha stress na msongo wa mawazo kwa vijana

Sasa mtu umeshaachana nae unamfatilia wa nini??

Ukiona mtu mmeachana nae ila we bado unamfatilia kwa kila anachofanya basi we bado unamtaka wakati ye ameshakusahau na anaendelea na maisha yake

Kwahiyo stress za hivi ni za kujitakia tu wala hazina mantiki
 
Inatokea sana tu hasa pale ambapo wewe ndiye ambaye umeachwa?

BTW habari yako Jimena .
 
Kula supu ya kongoro nakuja kulipa
 
Kama hapa jf ndo kiboko unaeza kuta unatoleana povu na mkeo,mmeo au x wako bila kujua na mkikutana home una kile kinyongo cha mtandaon bila kujua aliekupa hiko kinyongo ndo huyo unalala nae usiku๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Kuna watu ukiwaona mitandaoni unaweza kusema dah..mbona mie nimechelewa..Lakini sasa kutana nae Live hahahahahah utabaki unajichekea tuu..๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Hahahahaha
 
Niliteseka sana mwaka miaka ya nyuma enzi za JK nikiona watu wanapost wako kwenye ndege siti ya dirishani. Nikasema ee Mungu niwezeshe na mimi siku moja nipande ndege ila kwa mara ya kwanza isiwe Bombardier wala hizi ndogo za kina Coastal aviation (nilikuwa specific kwenye maombi)... na pia niliomba ikiwezekana iwe nje ya nchi. Miaka kadhaa mbele siku ikafika baada ya majaribio kadhaa ya kutaka kukata tiketi fastjet kutofanikiwa. Siku hiyo nakumbuka nilikata tiketi ya fastjet kutoka Dar - KIA nililipia Tsh 77,000/= taslimu. Ndege ya saa moja jioni. Kuanzia saa 8 mchana nilianza kuaga watu wangu wote muhimu pia kuwajulisha wenyeji wangu kwamba nitatua na mwewe. Nikafika JNIA mapema kabisa ila kilichotokea kilinisikitisha sana.. nilidhani ndege ni unapanda tu kama basi. Nikajiambia nitaenda kupanda dakika 15 kabla ya ndege kuondoka. Huo muda mwingine nikawa bize kuchukua selfie na video clip maeneo ya airport kwa kumbukumbu. Sikuamini nilivyoambiwa muda ushapita hata milango ya ndege ishafungwa kwahiyo nikate tu tiketi nyingine ya kesho saa 4. Ilibidi nifanye hivyo. Bahati nzuri baada ya hapo nikaanza kusafiri nchi mbalimbali. Kwa kifupi picha za mitandao zilinisaidia kunipa machungu na kufanya kazi kwa bidii zaidi
 

Sasa mkuu ukiwa na njaa utaiyoneshaji fb nikitu ambacho nikama Imani unais ni njaa ambayo mtu hawez kuiyona utawezaje kupost njaa fb[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kuna siku nilitaka kujipindua hivyo hivyo hapo Dar.Nilikuwa nakwenda Mwanza.

Nimekaa nasikiliza mziki mkubwa kwenye headphones, nikajisahau.Kuja kustuka dakika chache tu zimebaki milango ya ndege ifungwe.

Ilibidi niharakishe kuingia kwenye ndege, nafikiri nilikuwa mtu wa mwisho.

Sasa kuingia kwenye ndege, air hostess alikuwa kashatoa matangazo watu wazime simu, mimi sikusikia, kwa sababu yalitolewa kabla sijapanda nafikiri.

Nikawa nawapigia simu wenyeji wangu Mwanza kuwajulisha nitatua muda gani.

Huo mzozo uliozuk hapo ilibidi mpaka mzee mmoja wa usalama aingilie.Maana hatukuelewana na air hostess, yeye alifikiri mimi nimesikia tangazo nafanya ukaidi tu, wakati tangazo lilitolewa kabla mimi sijaingia kwenye ndege.

Habari hii inatufundisha tuwahi kupanda kwenye vyombo vya usafiri kuepuka usumbufu.
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Kuna watu ukiwaona mitandaoni unaweza kusema dah..mbona mie nimechelewa..Lakini sasa kutana nae Live hahahahahah utabaki unajichekea tuu..[emoji1787][emoji1787]
[emoji23]ni kweli kabisa mkuu,kuna watu wanajua kweli kuigiza
 
Kikubwa kujikubali, kuna best friend wangu nilisoma nae primary na maisha kiasi ya o level nilipata kukaa kwao, hakunahatika kupata nafasi ya kwenda high school. Nipo mwaka wa tatu ndio kaenda chuo cha ualimu. January kanipigia alipata nafasi ya ualimu na Mungu kamjaalia mtoto.
I mean, kila jambo lina wakati wake. Hakuna maisha ya โ€œgroup โ€œ binafsi sipendi kushika life theories za life begins at 40s etc, hakuna fixed guarantee ya kuwa pahala kutokana na level ya elimu au umri ulonao au jamii/ matafiki walokuzunguka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ