Mitego ya Mitandao: Changamoto za Online Dating ukiwa Mtu Mzima (Umri 30+)

Mitego ya Mitandao: Changamoto za Online Dating ukiwa Mtu Mzima (Umri 30+)

Watu hawataki kugandana, sisi wengine tukiamka asubuhi na kukuta "morning love" na makopakopa tunafurahi sana. Kuna wengine hawataki hizo mambo, anavaa gwanda anakula mzigo anavua gwanda tukutane na mwingine siku kibbutz kikijaa.
Ndio mtu anakwambia no strings attached! Lol ila hayo sio maisha mzee bora ukae zako single tu! Haina maana yoyote ile kujiongezea nafsi chafu tu!
 
Acha tu broski! 2022
Niliachwaga nikawa na stress ya kimbwa! Ndio mpaka leo nimekuwa sugu..

Nikasema hapa kupoza haya maumivu nidownload tinder then nichat na vijana nitakaa sawa, lol!

Unakutana na mkaka anakwambia umfanyie pegging akulipe!

Lesbian naye anataka akuhamishie huko na akulipe!

Wala visamvu sasa mtu yuko tayari kutoa hata laki3 mwingine anakuahidi gari.. (sijui siri hapa ni nini🤦🏽‍♀️)

Mwingine anataka kukuomba pesa tuu

Mwingine anakulazimisha akununue

Bado kuna wale the wanna be’s( wanajifanyaga wapo tu kule hawana mambo mengi watakuahidi hata ndoa, kumbe wana hook vizuri tu)

Ila, all in all sitotumia tena hii mitandao!🙌🏾
Sera pole kumbe usha wahi kuumizwa na siku zote hizo sikia na taarifa pole sana dear, Kuna dada angu aliolewa na jamaa wakawa wanaishi poa tu badae yule jamaa akapata mzungu hajamkimbia sista inasikitisha sana, alafu sista ana trako sura ipo umbo lipo, maisha ukisimiliwa ni tofauti na yenyewe yalivo
 
Nimejaribu kapokea mbibi anaongea kisukuma non stop😁🙌🏿

Alooo? Amwene mjukuu wane! Ulihola? Nene ndi nhola sana hano kaya. Nshosile gukugunila ungi simu gubwela igolo, lakini inamba yakwe yandya gushiga. Ndaga sana, nuyela ungi kela iyo watumile ungi simu. Natola isukali na majani a chai, nene nagwila chiza sana. Umbe, lini ukwiza gubisula hano ng'walo? Ukize gung'wambilija ungi gubaba, uje na lile joti lyane lya mbeho. Haya mjukuu wane, Isamalilage chiza, nikuwone!"
nitafsirie nicheke
 
Sera pole kumbe usha wahi kuumizwa na siku zote hizo sikia na taarifa pole sana dear, Kuna dada angu aliolewa na jamaa wakawa wanaishi poa tu badae yule jamaa akapata mzungu hajamkimbia sista inasikitisha sana, alafu sista ana trako sura ipo umbo lipo, maisha ukisimiliwa ni tofauti na yenyewe yalivo
Kwani we hujawahi umizwa? Pole kwa sistaako kuwa na tako au sura sio kigezo cha kupata ndoa!
 
Zamani, watu wazima walikuwa wanakutana sokoni, kanisani, misikitini, au kupitia marafiki.
Lakini leo, kupata mwenza kumehamia kwenye mitandao kama Tinder, Badoo, DM za Instagram, na makundi ya WhatsApp.

Ukiwa mtu mzima mwenye majukumu yako, unatafuta mtu makini wa kutulia naye. Hata hivyo, ulimwengu huu wa mtandaoni una mitego mingi sana.

Hapa kuna changamoto chache ambazo wengi wanakutana nazo:

Profaili feki (Catfishing): Unazungumza na mtu picha yake inaonyesha ni mtanashati au mrembo, lakini mkikutana live ni mtu mwingine kabisa.

Matapeli wa mapenzi (Romance Scammers): Watu wanaojifanya wako siriaz, kumbe lengo lao ni kuomba mizinga ya hela baada ya wiki mbili tu.

Watafuta burudani ya muda mfupi:
Kupata mtu anayetaka uhusiano wa kudumu (ndoa/uchumba) ni ngumu; wengi wanatafuta michepuko au starehe za usiku mmoja.

Uongo wa umri na hadhi: Watu kudanganya kuhusu kazi zao, umri, au hata kama wameoa/kuolewa.
Hebu tushirikiane uzoefu wenu:

1.Je, umewahi kujaribu kutafuta mwenza mtandaoni ukiwa mtu mzima?

2.Ilikuwaje?

3.Ni mtego gani mkubwa zaidi uliowahi kukutana nao au kuusikia kwa rafiki yako?
Unafikiri ni mbinu gani bora ya kumtambua mtu muongo au tapeli kabla hamjakutana ana kwa ana?View attachment 3648487
Tumia datting za kulipia boss, takriban 80% zinakuwa za uhalisia
Hizo za bure 75% ni feki
 
Kwani we hujawahi umizwa? Pole kwa sistaako kuwa na tako au sura sio kigezo cha kupata ndoa!
Nisha umizwa ndo mana nakomalia mashangazi, ipo hivi 2019 nilichaguliwa chuo Dom, nikiwa chuo nilikua mtanashati balaa, nilipendwa na mademu kibao niliongelewa sana na mademu wote wananitaka, nikamchagua demu alitwa Lena, huyu demu nilimpenda sana alikua mfupi mdogo kiumri sura Kali, shepu balaa trako usiseme, nikakushia wengine kama siwaoni, 2020 nika disco, nilikua naishi uzunguni karibu na jengo la Vodacom au karibu na kilimani, au Kwenye jengo la mkuu wa mkoa wa zamani, nikaamtafuta Lena baada ya kurudi geto zilikua zimepita siku kadhaa tangu nisimamishwe, nilipo mcheki pisi Lena alinipokea Kwa shangwe nilijihisi mtu, tulichati sana ila nilipo mkumbusha kuwa NAMPENDA na Niko tayari kumuoa kimbembe kikaanzia hapo akanambia, Alex pole eti SIPO tayari kuwa na wewe tena tafuta mwingine bye, dah niliumia sana but sikumbembeleza nika futa NAMBA zake maisha yanaendelea japo Kwa stress ila sasa hivi simuwazii Wala nini
 
Tulikula sana nauli za Wasukuma enzi hizo, mambo ya wrong numbers, lakini tulikua tunabuni namba tunapiga tunajifanya tumekosea,
Kuna siku tumepiga kapokea muhindi, akatuambia twende steers enzi hizo makumbusho, tumefika tunapiga simu akaja libaba refu boooooonge, we acha tutoke ndukiiiii
 
Nisha umizwa ndo mana nakomalia mashangazi, ipo hivi 2019 nilichaguliwa chuo Dom, nikiwa chuo nilikua mtanashati balaa, nilipendwa na mademu kibao niliongelewa sana na mademu wote wananitaka, nikamchagua demu alitwa Lena, huyu demu nilimpenda sana alikua mfupi mdogo kiumri sura Kali, shepu balaa trako usiseme, nikakushia wengine kama siwaoni, 2020 nika disco, nilikua naishi uzunguni karibu na jengo la Vodacom au karibu na kilimani, au Kwenye jengo la mkuu wa mkoa wa zamani, nikaamtafuta Lena baada ya kurudi geto zilikua zimepita siku kadhaa tangu nisimamishwe, nilipo mcheki pisi Lena alinipokea Kwa shangwe nilijihisi mtu, tulichati sana ila nilipo mkumbusha kuwa NAMPENDA na Niko tayari kumuoa kimbembe kikaanzia hapo akanambia, Alex pole eti SIPO tayari kuwa na wewe tena tafuta mwingine bye, dah niliumia sana but sikumbembeleza nika futa NAMBA zake maisha yanaendelea japo Kwa stress ila sasa hivi simuwazii Wala nini
Kama 2019 ndio ulikuwa unaanza masomo basi una muda mwingi wa kusaka umpendaye usijali kabisa mdogoangu alex! Vzr ulifanya maamuzi ya kiume ukamove on..
 
Back
Top Bottom