Daaah, mkuu uko vizuri kwenye soil chemistry. Umetusaidia na sisi wengine ambao hatukuelewa mambo hayo. Lakini nina swali kuhusu hapo uliposema udongo kujizalisha; tunaonaga mara nyingi mahali pengi panachimbwa udongo either kwa ajili ya kutengeneza barabara au vinginevyo. Sasa mbona maeneo yaliyotolewa udongo yanabaki hivyohivyo (no recovering) kwa miaka na miaka?
Hapo kuna mambo mawili.
Kuna udongo na Ardhi.
Udongo ni sehemu ya Ardhi, au tuseme Layer ya juu ya Ardhi.
Udongo unamatabaka yake "Soil Profiles"
Pia katika uzalishaji WA udongo "Soil Formation" kuna Stage of soil formations ambazo stage hizi zinaratibiwa na Factors za soil Formation.
Mambo haya ni muhimu katika utengenezaji/uzalishaji WA udongo
1. Nature of Rock / Mwamba asilia.
Hapa itategemea na eneo lililochimbwa ni Aina gani ya kwamba. Tunafahamu miamba ipo ya Aina nyingi lakini Aina kuu Kulingana na namna ya utokeaji wa miamba hiyo ni tatu, nazo ni Igneous rocks (miamba migumu ambayo pia ndio mama aliyezaa miamba mingine) miamba hii utokeaji wake unatokana na ujiuji uliopo kwenye tabaka la Kati la dunia(molten material from Mantle) ambayo ikitokea kwenye tabaka la nje la dunia(Crust) huitwa Magma au lava.
Metamorphic rocks, na Sedimentary Rock.
Kama eneo lililochimbwa kwamba wake ni mgumu itachukua muda mrefu Kwa udongo kuzalishwa. Maana kuna Michakato kama yA Weathering inatakiwa itokee kuuvunja vunja mwamba into small fragments/sediment ambayo hizo kokote baada ya muda nayo huvunjika huvunjika vunjika na kuwa small particles mpaka kufikia level ya udongo.
2. Tabia ya nchi (Climate conditions)
Tabia ya nchi ni moja ya mambo yanayopelekea uzalishaji WA udongo kuwa haraka au kudorora.
Ishu za Aina zote za precipitation ikiwemo Mvua, manyunyu,umande, ukungu, n.k Jotoridi (temperatures) upepo/Wind n.k
Ni moja ya factory zinazopelekea na kuathiri uzalishaji WA udongo Kwa haraka au polepole.
3. Altitude/ tambarare au mwinuko.
Eneo la lililochimbwa endapo lipo bondeni au kwenye tambarare ni rahisi ku-recovery Kwa muda mfupi ukilinganisha na eneo ambalo lipo kwenye mwinuko. Kutokana na factory mbalimbali Kama masuala ya Erosion/mmomonyoko na Accumulation (kutuama) Kwa vitu vilivyochukuliwa kwenye milima au miinuko mikali.
iii. Living organisms (uwepo wa viumbe hai) vyote/both Mimea na wanyama.
Eneo lililo na uhaba wa viumbe hai ni ngumu udongo wake ku-recovery.
Ukienda kuchimba msituni shimo ni rahisi shimo Hilo kujaa harakaharaka takataka iwe majani au vipande vya miti na magogo ambazo baadaye zita-decompose/decaying au kuoza na kuunda udongo