Miti inakua kutoka wapi? Mbona hatuoni shimo pale ulipotoka?

Miti inakua kutoka wapi? Mbona hatuoni shimo pale ulipotoka?

Nywele zote ni protini. Ukinyoa hata moja, basi volume yako na protini zako, na uzito wako unakuwa umepungua. Ukinyoa nyingi ndiyo itaonekana zaidi. Sasa fikiria mti wa kilo milioni moja kutoka ardhini?
Vizuri sana Sasa mti ndo protini ya Ardhi kama unabisha njoo nkupe aftatu njomba.
 
Mizizi inachukua nafasi ya udongo (minerals, nutrients) unaobadilishwa kuwa mti.

Kwani hujawahi kukuta mti umeng’olewa (kuanzia miziz yake), then ukaona BONGE la shimo utadhani pameangukiwa na kimondo cha Mbeya?
Na minerals na nutrients zinazoenda kuunda shina nafasi yake inachukuliwa na nini? Maana tambua kuwa mizizi nayo imetoka kwenye hizo nutrients na minerals. Miti ingekuwa haitoki juu point yako ingekuwa valid.
 
Watu naona wanambeza mleta uzi ila naona ana hoja fikirishi. Sishangai maana hata Newton alivoshangazwa na apple kukatika kwenye kikonyo chake likashuka chini badala lipande juu najua kuna walalahoi walimbeza ila leo tunajua matokeo ya kushangazwa kwake
 
Kama hizo elements hazinanuzito, mti wenye kilo laki tano unatoka wapi?
Uko familiar na tissue formation kwenye plants,,, mitosis kwenye meristem na from meristems to permanent tissues,, and primary, secondary, lateral and horizontal growth pattern kwenye plants?
 
Na minerals na nutrients zinazoenda kuunda shina nafasi yake inachukuliwa na nini? Maana tambua kuwa mizizi nayo imetoka kwenye hizo nutrients na minerals. Miti ingekuwa haitoki juu point yako ingekuwa valid.
Replacements za components zingine za udongo kutokana na soil cycle.
 
Not true. Elements na molecules zina uzito. Molecular weight, molecular mass. Atomic weight, atomic mass. Remember?
Consumption ya hizo elements by tree hata kwa course ya miaka 100 can affect ujazo wa Udongo?? Hyo botany umeitolea wapi?? Hatukatai zina uzito but it's on molecular level and by the way kitu ambacho tunaweza ona kama kimepungua au kimeongezeka ni moisture level na sio uzito wa Udongo
 
Mkuu kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba unajaribu kufananisha ujazo/ukubwa wa shimo la mti mkubwa na kitu kilichojengwa na binadamu. Mti unatumia mizizi kuweza kusimama na hiyo mizizi inaota kwa kulala si kwa kwenda chini sana ni tofauti na jinsi binadamu tunavyojenga, sisi inabidi kuwe na shimo refu kwenda chini kuweka msingi wa kile tunachojenga. Mti ni kiumbe chenye mfumo unaoweza kutafuta njia bora zaidi ya kusimama ardhini. Kwa utafiti mdogo nilofanya mtandoni unaonyesha kwa miaka mingi wanasayansi wamekuwa wakichunguza miti ili kuweza kuelewa zaidi njia bora za kusafirisha maji na hata kusimamisha majengo. Natamani wataalamu wa Architecture na Civil Engineering wangetupia jicho hapa ili kuendeleza huu mjadala.


Unaweza kusoma:



View attachment 2418100View attachment 2418101
Wewe ujamuelewa anacho uliza mleta uzi[emoji1787]
Ila wacha nimjibu mleta uzi swali lake ...mti unapo jitengeneza unakuwa kama sponji au ugali wa amira hivyo ukitaka kujua hilo usage kuwa vumbi kisha ushindilie na mashine ya kukandamiza ...utagundua kuwa ni mdogo sana huo mti
 
Miti ni viumbe hai tu kama ulivyo wewe (botany and zoology) sasa hujiulizi wewe unavyokua hizo nyama, damu, mifupa inayoongzeka mwilini kwako vinatoka wapi ?

Mti (mimea) Unaanzia kwenye surface kuelekea juu. Na Mizizi yake inakua kuelekea chini. Sema ndo kuna mimea ambayo shina linakua kwa rate kubwa kuliko mizizi wakati mingine ni vice versa
Mleta uzi anajua hivyo yeye anacho uliza ni ujazo wa mti mzima na ujazo wa shimo lililo kuza huo mti, yeye anaona mbona shimo ni dogo kuliko ukubwa wa mti zaidi ya mara 10 hivi ....jibu ni kwamba mti upo kama sponji hivyo ukitaka kujua kuwa ujazo wa mti mkubwa ni mdogo tu ukaushe huo mti kisha usage na kushindilia vumbi lake kwa mashine ...utapata jibu
 
Consumption ya hizo elements by tree hata kwa course ya miaka 100 can affect ujazo wa Udongo?? Hyo botany umeitolea wapi?? Hatukatai zina uzito but it's on molecular level and by the way kitu ambacho tunaweza ona kama kimepungua au kimeongezeka ni moisture level na sio uzito wa Udongo
You’re outrageously lying. Unajua just per day, mti unasharabu nutrients, mineral salts, water kiasi gani ambazo ni equivalent na volume ama uzito wa udongo?

Uelewa wako wa sayansi ni kiduchu sana.
 
Basi wakuu yaishe. Juzi kati nilisoma kitabu Chuo cha ustaarabu. Kiliandikwa na mzungu mmoja Kenya mwaka 1935. Na mimi swali hilo lilinishtua. Alilijibu. Ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya mti inatoka hewan. Mti unavyobadili carbondioxide kuwa cellulose ndiyo unavyojijenga hasa.

Asilimia 95 ya mti umetokana na carbondioxide na maji. ukitoa maji, zaidi ya 60% ya mti hutoka hewani kwenye carbondioxide. Ni vitu vichache sana(micronutrients+Nitrogen) ndivyo hutoka ardhini. Kwa hesabu hizo, ni kuwa mti hautoki ardhini ndiyo maana hatuoni shimo ulipoota.

Waliofanya utafiti, walipanda mmea kwenye kopo lenye udongo wa kilo kadhaa. Baada ya kutoa ule mmea, wakagundua kuwa kilo za udongo ule hazijabadilika. Hata ukichoma mti mkubwa, utaona sehemu kubwa inapotelea angani.

Pengine watu wa kabla ya uhuru walikuwa na maarifa kuliko sisi leo.

New Doc 2022-10-03 222515-1_page-0001-1.png
 
Tunafanyaje kilimo na hata hatufahamu mimea tunayopanda inatoka wapi?
 
Na minerals na nutrients zinazoenda kuunda shina nafasi yake inachukuliwa na nini? Maana tambua kuwa mizizi nayo imetoka kwenye hizo nutrients na minerals. Miti ingekuwa haitoki juu point yako ingekuwa valid.
Ukitaka kuelewa vizuri hili, fikiria chini ya ardhi kama sehemu yenye mifereji mingi sana midogo midogo inayosafirisha maji, hewa, mineral elements kutoka juu ya ardhi na sehemu zingine za mbali ardhini.

Mti unakusanya dutu hizo zote kutoka sehemu mbalimbali, kama ziwa linavyofanyika kutokana na kunyweshwa maji ya mito mingi itokayo mbali.
 
Hapana. Namaanisha kama mti unatoka ardhini, basi kuwe na shimo kubwa pale ulipotoka.
Labda kwa kuchimba visiki mkuu ndipo shimo hutokea tofauti na hapo ni sawa na useme mtu akiota kipele then kikapona basi awe na kishimo sawa na uzito wa kipele 😂
 
Hapo kuna mambo mawili.
Kuna udongo na Ardhi.

Udongo ni sehemu ya Ardhi, au tuseme Layer ya juu ya Ardhi.

Udongo unamatabaka yake "Soil Profiles"

Pia katika uzalishaji WA udongo "Soil Formation" kuna Stage of soil formations ambazo stage hizi zinaratibiwa na Factors za soil Formation.

Mambo haya ni muhimu katika utengenezaji/uzalishaji WA udongo
1. Nature of Rock / Mwamba asilia.
Hapa itategemea na eneo lililochimbwa ni Aina gani ya kwamba. Tunafahamu miamba ipo ya Aina nyingi lakini Aina kuu Kulingana na namna ya utokeaji wa miamba hiyo ni tatu, nazo ni Igneous rocks (miamba migumu ambayo pia ndio mama aliyezaa miamba mingine) miamba hii utokeaji wake unatokana na ujiuji uliopo kwenye tabaka la Kati la dunia(molten material from Mantle) ambayo ikitokea kwenye tabaka la nje la dunia(Crust) huitwa Magma au lava.
Metamorphic rocks, na Sedimentary Rock.

Kama eneo lililochimbwa kwamba wake ni mgumu itachukua muda mrefu Kwa udongo kuzalishwa. Maana kuna Michakato kama yA Weathering inatakiwa itokee kuuvunja vunja mwamba into small fragments/sediment ambayo hizo kokote baada ya muda nayo huvunjika huvunjika vunjika na kuwa small particles mpaka kufikia level ya udongo.

2. Tabia ya nchi (Climate conditions)

Tabia ya nchi ni moja ya mambo yanayopelekea uzalishaji WA udongo kuwa haraka au kudorora.
Ishu za Aina zote za precipitation ikiwemo Mvua, manyunyu,umande, ukungu, n.k Jotoridi (temperatures) upepo/Wind n.k
Ni moja ya factory zinazopelekea na kuathiri uzalishaji WA udongo Kwa haraka au polepole.

3. Altitude/ tambarare au mwinuko.
Eneo la lililochimbwa endapo lipo bondeni au kwenye tambarare ni rahisi ku-recovery Kwa muda mfupi ukilinganisha na eneo ambalo lipo kwenye mwinuko. Kutokana na factory mbalimbali Kama masuala ya Erosion/mmomonyoko na Accumulation (kutuama) Kwa vitu vilivyochukuliwa kwenye milima au miinuko mikali.

iii. Living organisms (uwepo wa viumbe hai) vyote/both Mimea na wanyama.
Eneo lililo na uhaba wa viumbe hai ni ngumu udongo wake ku-recovery.
Ukienda kuchimba msituni shimo ni rahisi shimo Hilo kujaa harakaharaka takataka iwe majani au vipande vya miti na magogo ambazo baadaye zita-decompose/decaying au kuoza na kuunda udongo
Mmmmmh, imbombo ingalipo. Kweli udongo ni somo pana. Tunakushukuru kwa elimu hii; inaonekana umebobea kwenye fani hii. Hongera.
 
Back
Top Bottom