Miti inakua kutoka wapi? Mbona hatuoni shimo pale ulipotoka?

Nywele zote ni protini. Ukinyoa hata moja, basi volume yako na protini zako, na uzito wako unakuwa umepungua. Ukinyoa nyingi ndiyo itaonekana zaidi. Sasa fikiria mti wa kilo milioni moja kutoka ardhini?
Vizuri sana Sasa mti ndo protini ya Ardhi kama unabisha njoo nkupe aftatu njomba.
 
Mizizi inachukua nafasi ya udongo (minerals, nutrients) unaobadilishwa kuwa mti.

Kwani hujawahi kukuta mti umeng’olewa (kuanzia miziz yake), then ukaona BONGE la shimo utadhani pameangukiwa na kimondo cha Mbeya?
Na minerals na nutrients zinazoenda kuunda shina nafasi yake inachukuliwa na nini? Maana tambua kuwa mizizi nayo imetoka kwenye hizo nutrients na minerals. Miti ingekuwa haitoki juu point yako ingekuwa valid.
 
Watu naona wanambeza mleta uzi ila naona ana hoja fikirishi. Sishangai maana hata Newton alivoshangazwa na apple kukatika kwenye kikonyo chake likashuka chini badala lipande juu najua kuna walalahoi walimbeza ila leo tunajua matokeo ya kushangazwa kwake
 
Kama hizo elements hazinanuzito, mti wenye kilo laki tano unatoka wapi?
Uko familiar na tissue formation kwenye plants,,, mitosis kwenye meristem na from meristems to permanent tissues,, and primary, secondary, lateral and horizontal growth pattern kwenye plants?
 
Na minerals na nutrients zinazoenda kuunda shina nafasi yake inachukuliwa na nini? Maana tambua kuwa mizizi nayo imetoka kwenye hizo nutrients na minerals. Miti ingekuwa haitoki juu point yako ingekuwa valid.
Replacements za components zingine za udongo kutokana na soil cycle.
 
Not true. Elements na molecules zina uzito. Molecular weight, molecular mass. Atomic weight, atomic mass. Remember?
Consumption ya hizo elements by tree hata kwa course ya miaka 100 can affect ujazo wa Udongo?? Hyo botany umeitolea wapi?? Hatukatai zina uzito but it's on molecular level and by the way kitu ambacho tunaweza ona kama kimepungua au kimeongezeka ni moisture level na sio uzito wa Udongo
 
Wewe ujamuelewa anacho uliza mleta uzi[emoji1787]
Ila wacha nimjibu mleta uzi swali lake ...mti unapo jitengeneza unakuwa kama sponji au ugali wa amira hivyo ukitaka kujua hilo usage kuwa vumbi kisha ushindilie na mashine ya kukandamiza ...utagundua kuwa ni mdogo sana huo mti
 
Mleta uzi anajua hivyo yeye anacho uliza ni ujazo wa mti mzima na ujazo wa shimo lililo kuza huo mti, yeye anaona mbona shimo ni dogo kuliko ukubwa wa mti zaidi ya mara 10 hivi ....jibu ni kwamba mti upo kama sponji hivyo ukitaka kujua kuwa ujazo wa mti mkubwa ni mdogo tu ukaushe huo mti kisha usage na kushindilia vumbi lake kwa mashine ...utapata jibu
 
You’re outrageously lying. Unajua just per day, mti unasharabu nutrients, mineral salts, water kiasi gani ambazo ni equivalent na volume ama uzito wa udongo?

Uelewa wako wa sayansi ni kiduchu sana.
 
Basi wakuu yaishe. Juzi kati nilisoma kitabu Chuo cha ustaarabu. Kiliandikwa na mzungu mmoja Kenya mwaka 1935. Na mimi swali hilo lilinishtua. Alilijibu. Ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya mti inatoka hewan. Mti unavyobadili carbondioxide kuwa cellulose ndiyo unavyojijenga hasa.

Asilimia 95 ya mti umetokana na carbondioxide na maji. ukitoa maji, zaidi ya 60% ya mti hutoka hewani kwenye carbondioxide. Ni vitu vichache sana(micronutrients+Nitrogen) ndivyo hutoka ardhini. Kwa hesabu hizo, ni kuwa mti hautoki ardhini ndiyo maana hatuoni shimo ulipoota.

Waliofanya utafiti, walipanda mmea kwenye kopo lenye udongo wa kilo kadhaa. Baada ya kutoa ule mmea, wakagundua kuwa kilo za udongo ule hazijabadilika. Hata ukichoma mti mkubwa, utaona sehemu kubwa inapotelea angani.

Pengine watu wa kabla ya uhuru walikuwa na maarifa kuliko sisi leo.

 
Tunafanyaje kilimo na hata hatufahamu mimea tunayopanda inatoka wapi?
 
Na minerals na nutrients zinazoenda kuunda shina nafasi yake inachukuliwa na nini? Maana tambua kuwa mizizi nayo imetoka kwenye hizo nutrients na minerals. Miti ingekuwa haitoki juu point yako ingekuwa valid.
Ukitaka kuelewa vizuri hili, fikiria chini ya ardhi kama sehemu yenye mifereji mingi sana midogo midogo inayosafirisha maji, hewa, mineral elements kutoka juu ya ardhi na sehemu zingine za mbali ardhini.

Mti unakusanya dutu hizo zote kutoka sehemu mbalimbali, kama ziwa linavyofanyika kutokana na kunyweshwa maji ya mito mingi itokayo mbali.
 
Hapana. Namaanisha kama mti unatoka ardhini, basi kuwe na shimo kubwa pale ulipotoka.
Labda kwa kuchimba visiki mkuu ndipo shimo hutokea tofauti na hapo ni sawa na useme mtu akiota kipele then kikapona basi awe na kishimo sawa na uzito wa kipele 😂
 
Mmmmmh, imbombo ingalipo. Kweli udongo ni somo pana. Tunakushukuru kwa elimu hii; inaonekana umebobea kwenye fani hii. Hongera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…