Mitume walikuwa wanaomba kuombewa na wafuasi kipindi wanafanya huduma. Kwanini mwingine anaombewa hata baada ya kufa?

Mitume walikuwa wanaomba kuombewa na wafuasi kipindi wanafanya huduma. Kwanini mwingine anaombewa hata baada ya kufa?

Baraka inatoka kwa Mungu kupitia baba mzazi, sasa baba mzazi tayari alishadanganywa na akatoa baraka kwa kudanganywa, maana yake process nzima imejaa ubatili na baraka zimejaa ubatili, vip Mungu atie mkono wake kwenye ubatili wa namna hii?
Mungu anafanya kazi kwa kanuni zake. Mfano kuna kanuni ya kupanda na kuvuna au kanuni ya nguvu ya uvutano. Ukifuata kanuni hata kama ni mwenye udhaifu na wakati mwingine mwenye dhambi bado unaweza kupata matokeo yanayohusiana na ile kanuni.

Mtakatifu na mwenye dhambi wote wakipanda mbegu wanavuna. Wote wakijiachia kutoka juu ya jengo la ghorofa kumi wataumia vibaya na pengine kufa.

Kanuni za Mungu zinaweka usawa.
 
Hatujachoka na hatuchoki, ukiona vyaelea vimeundwa, wacha tuwaombee wazazi wetu na waalimu wetu walio tufanya tukatoa ujinga
Usipotafuta utakatifu hapa duniani sahau kufanywa mtakatifu kwa maombi ya wengine.
 
Sisi Waislamu tunawatakia amani Mitume Wote (nafikiri hicho ndicho alichomaanisha mtoa uzi kuwa ni kumuombea).

Kwa hiyo
Tunawatakia amani kuanzia Mtume Adam (Amani iwe juu yake) mpaka Muhammad ( Swala na Amani ziwe juu yake).

Kama mtoa uzi ulikuwa haufahamu basi fahamu hivyo kuanzia leo.
 
Mungu anafanya kazi kwa kanuni zake. Mfano kuna kanuni ya kupanda na kuvuna au kanuni ya nguvu ya uvutano. Ukifuata kanuni hata kama ni mwenye udhaifu na wakati mwingine mwenye dhambi bado unaweza kupata matokeo yanayohusiana na ile kanuni.

Mtakatifu na mwenye dhambi wote wakipanda mbegu wanavuna. Wote wakijiachia kutoka juu ya jengo la ghorofa kumi wataumia vibaya na pengine kufa.

Kanuni za Mungu zinaweka usawa.
Umeanza kuchanganyikiwa sasa, wote wanapanda ardhini , sio kazi yao kuchepusha mazao ni kazi ya ardhi, rudi kwenye hoja Mungu kaweka utaratibu lazima baraka baba atoe kwa mtoto wake wa kwanza, Mzee Isiaka akiamini kuwa anatoa kwa Essau kumbe kuna mtu na mama yake wamemdanganya , process nzima imekuwa batili , vip output iwe safi? ni ubatili mtupu na Mungu wao aliupitisha bila wasiwasi
 
Mtume Paulo aliyaomba makanisa ya Rumi, Efeso na lile la Korintho yamuombee ili injili iweze kufika mbali zaidi kwa kinywa chake.

Alipomaliza huduma aliaga katika barua kwa Timotheo kwamba ameilinda imani na kwamba anaenda zake kwenye taji aliyowekewa.

Mtume Petro naye alikumbusha kuombea huduma na alipomaliza aliwaambia waumini kwamba wakati umefika kwake kuondoka tena itakuwa kutundikwa juu ya msalaba kichwa kikiwa chini na miguu juu.

Hawa wote wawili walikuwa na furaha na kuondoka duniani kwa uhakika na ushindi. Walikuwa wakiwasisitiza waumini wafuate mfano wao.

Sasa nashangaa kuna nabii eti ni wa mwisho na ndio mkuu kwa wote lakini mpaka sasa anaombewa akiwa amefariki.

Alikwama wapi na nini kimemfanya yeye asiwe na uhakika wa kuingia mbinguni mpaka aendelee kuombewa?
Umeishia kuandika tu kwamba anaombewa bila kutuonyesha anaombewaje, maana sisi ndiyo waislamu wenyewe tunaishi katika Uislamu na tunausoma ila hatujaona hizi habari. Wewe umezipata wapi za Mtume kuombewa.

Kingine aya yako ya kwanza inaonyesha wazi Paulo hakuwa Mtume, sasa najiuliza utume wa Pauolo na Petro wameupata wapi, isiwe hata maana ya Utume pia huijui. Naomba ujibu swali nililo kuuliza.

Shukrani.
 
Usipotafuta utakatifu hapa duniani sahau kufanywa mtakatifu kwa maombi ya wengine.
Dunian utakatifu natafuta ndio maana nafundisha watu mambo mema, hata nikifa wale watu wanikumbuke kwa wema kwa kutenda sawa na elimu nilio wafundisha ili thawabu zangu ziongezeke
 
Fuatilia baadhi ya sala/swala. Lazima aombewe.
Sala gani kijana, si utuambie ? Kuna Wakristo wenzako naona wamekuunga mkono, hata kukuuliza mwenzao wanashindwa, yaani Wakristi vilaza sana. Wamekaa kishabiki shabiki mno.

Sasa wewe ndiyo umeanzisha mada, ajabu unashindwa kuitetea mada yako, shida nini ?
 
Ukiwa huna uhakika na unachoandika ni BORA KUTOANZISHA UZI....

kwenye Uislam ukisikia anatajwa Mola Mlezi utasikia kwa mfano Allah Subhanah Wataala, akitajwa Mtume utasikia Rehema na Amani ziwe juu yake, wakitajwa mitume wote waliobakia aliwemo mtume wa Allah Issah utakisikia Alayh Salam, wakitajwa maswahaba utasikia Radhiallah Anhu, Waja wema waliotangulia Rahmahullah au waliopo HAI utasikia hafidhallah

Kwa hiyo siyo kweli UNACHOKISEMA KUWA KWENYE UISLAM MTUME ANAOMBEWA MSAMAHA.....

MOLA MLEZI ameweka utaratibu wa kumtukuza YEYE kila anapotajwa au unapotaja jina la Mola Mlezi, kuwatakia salama na amani Waja wema waliotangulia kwa maana waliishi na kumridhisha YEYE na YEYE amewaridhia na wanaombewa mpaka na malaika...

KINYUME CHAKE kwa kila aliyeishi kwa UJABARI NA KUMUASI MOLA MLEZI KAMA FIRAUNI na wote wanaomfuatia basi utasikia yakitamkwa MKASIRIKO YA MOLA MLEZI NA KUWEKWA MBALI NA REHEMA ZAKE baada ya majina yao!!!!

Kwa aliye hai ataombewa UONGOFU ila akifa mwanadamu kati uasi basi hadi Malaika watamwombea Makasiriko ya Mola Mlezi....

HUJAWAHI ONA MTU ANAFARIKI NA WATU WANAFURAHI KUWA WATAPUMZIKA KUTOKANA NA MAUDHI AU DHULMA ZAKE???? Au MWINGINE ANAFARIKI KILA YUALIA KUTOKANA NA WEMA WAKE KWA WATU???

Basi jua vivyo hivyo kwa wanadamu na Mailaka kumwombea aliyefariki au hata aliye HAI...
Bibie samahani lakini, hivi umeolewa ?

Umeandika vya maana sana, halafu kuna nilikuwa sikijui toka kwako...saza nimekijiua.
 
Umeanza kuchanganyikiwa sasa, wote wanapanda ardhini , sio kazi yao kuchepusha mazao ni kazi ya ardhi, rudi kwenye hoja Mungu kaweka utaratibu lazima baraka baba atoe kwa mtoto wake wa kwanza, Mzee Isiaka akiamini kuwa anatoa kwa Essau kumbe kuna mtu na mama yake wamemdanganya , process nzima imekuwa batili , vip output iwe safi? ni ubatili mtupu na Mungu wao aliupitisha bila wasiwasi
Yakobo alikuwa na haki na ndio maana Mungu akampa baraka.
 
Yakobo alikuwa na haki na ndio maana Mungu akampa baraka.
Mwenye haki hawezi mdanganya baba yake mzazi , yule alikuwa na mashaka kuwa haki aliipata kwa utapeli, ndio maana akaamua kufanya ule uhuni mbele ya baba yake mzazi, ule ni ubatili
 
Umeishia kuandika tu kwamba anaombewa bila kutuonyesha anaombewaje, maana sisi ndiyo waislamu wenyewe tunaishi katika Uislamu na tunausoma ila hatujaona hizi habari. Wewe umezipata wapi za Mtume kuombewa.

Kingine aya yako ya kwanza inaonyesha wazi Paulo hakuwa Mtume, sasa najiuliza utume wa Pauolo na Petro wameupata wapi, isiwe hata maana ya Utume pia huijui. Naomba ujibu swali nililo kuuliza.

Shukrani.
Paulo na Petro ni watume wa Yesu Kristo.

Mswalie mtumeee.. allah akbar. Watukufu waislamu, tumswalie mtume na kumuombea rehma za mwenyenzi mungu.

Haya maneno kila siku nayasikia msikitini wa jirani hapa.
 
Sala gani kijana, si utuambie ? Kuna Wakristo wenzako naona wamekuunga mkono, hata kukuuliza mwenzao wanashindwa, yaani Wakristi vilaza sana. Wamekaa kishabiki shabiki mno.

Sasa wewe ndiyo umeanzisha mada, ajabu unashindwa kuitetea mada yako, shida nini ?
Wapi hujapata mwongozo kwenye hii mada? Wakristo unawapa kashfa bila sababu yoyote.
 
Mwenye haki hawezi mdanganya baba yake mzazi , yule alikuwa na mashaka kuwa haki aliipata kwa utapeli, ndio maana akaamua kufanya ule uhuni mbele ya baba yake mzazi, ule ni ubatili
Haki Ile aliinunua kihalali na akafanya mbinu kuhakikisha baba yake hamfanyii fitna kumnyima kisa chakula cha Esau.
 
Paulo na Petro ni watume wa Yesu Kristo.

Mswalie mtumeee.. allah akbar. Watukufu waislamu, tumswalie mtume na kumuombea rehma za mwenyenzi mungu.

Haya maneno kila siku nayasikia msikitini wa jirani hapa.
Tuwekee ushahidi wapi Yesu aliwapa utume sababu utume hauji kwa ndoto au kama kupewa pipi au kupokezana vijiti.

Sababu inaonyesha Paulo alikuwa Myahudi kiasili na hajawahi kuonana na Yesu, utume aliupata wapi na lini ?
 
Dunian utakatifu natafuta ndio maana nafundisha watu mambo mema, hata nikifa wale watu wanikumbuke kwa wema kwa kutenda sawa na elimu nilio wafundisha ili thawabu zangu ziongezeke
Utakatifu unaompa mtu uzima wa milele unatokana na imani kwa Yesu Kristo ili kupata msamaha wa dhambi. Nje ya hapo hakuna utakatifu wowote.
 
Wapi hujapata mwongozo kwenye hii mada? Wakristo unawapa kashfa bila sababu yoyote.
Umesahau mada yako inaongelea nini ? Hivi Wakristo wenzako wamehmshindwa kukuhoji ? Kwamba unaandika jambo ambalo huna elimu nalo ? Au kwasababu nyote mazwazwa ndiyo maana hili liko hivi ?
 
Tuwekee ushahidi wapi Yesu aliwapa utume sababu utume hauji kwa ndoto au kama kupewa pipi au kupokezana vijiti.

Sababu inaonyesha Paulo alikuwa Myahudi kiasili na hajawahi kuonana na Yesu, utume aliupata wapi na lini ?
Paulo kaonana na Yesu akiwa njiani kwenda Damascus. Akapewa utume.
 
Umesahau mada yako inaongelea nini ? Hivi Wakristo wenzako wamehmshindwa kukuhoji ? Kwamba unaandika jambo ambalo huna elimu nalo ? Au kwasababu nyote mazwazwa ndiyo maana hili liko hivi ?
Sijaona hoja yoyote uliyoileta ambayo haijapata majibu mujarabu.
 
1. Wote wanakubali kuwa Allah ni Mungu
2.wote wanakubali mohamadi ni nabii
3.wote wanakubali kuwa Isa bin Maryamu ni nabii sio Mungu
Hayo mengine yote sio tatizo kutofautiana, sasa watu wanatofautiana kwenye mwezi muandamo hivi ni vitu vidogo ambavyo haviwezi mtoa mtu katika Uislam
UNAKWEPA MASWAL KIJANA

NAKUJA HAPA NA MISIMAMO YA MADHEHEBU YOTE YA UISLAMU ,HALAFU UNIAMBIE LIPI NDIO TULIFATE AU LIPI NDIO UISLAMU HALISI
 
Back
Top Bottom