James Comey
JF-Expert Member
- May 14, 2017
- 8,759
- 14,831
Ni wachache sana wataelewa maana iliyobebwa na hii reply.Ushauri:
Haya mambo ya kukashifiana dini ningeshauri yaishe tu kwa sababu zifuatazo;
1. Haiwezekani tena kuufuta Uislamu au Ukristo. Mamia ya miaka ya mashindano kati ya dini hizi mbili bila mafanikio ya upande wowote, ni ushahidi tosha. Tuchape kazi katika kuzitafutia familia zetu na wenye shida (sadaka) mahitaji muhimu......hiyo ni ibada nzuri, kwa upande wowote wa imani uliopo, na yenye maana kuliko kutafuta shari na migongano.
2. Ni ukweli kuwa kwa kizazi cha sasa akili za kuweza kuua Uislamu au Ukristo HATUNA! Sana sana tutaishia kutukanana n.k. Vyakula vya chips, mayai tvs n.k vimedororesha pakubwa uwezo wetu wa kufikiri. Kujaribu kutikisa hoja za Qur'an au Biblia kwa kizazi hiki ni kupoteza muda tu......tumeisha; tufuate tu kila mmoja wetu anakotaka kufuata tupite tuwapishe wengine!
Kuna watu wanajiita wasomi humu lakini hawataki kupata maana ktk hii reply yako.